Natafuta mganga wa kienyeji konki

Natafuta mganga wa kienyeji konki

Binafsi sina conection ya mganga maana niliekutana nae wakati wa matatizo hakuna alichonisaidia zaidi ya kunipa masharti ya kiwaki tu mfano alinambia nisiwe nafagia eneo langu la kazi kwa mafagio haya marefu ya kichina nitumie yale mafagio ya zamanii yanauzwaga Jero,akanipa dawa ya kuchanganya wakati nadeki na ziada alinambia alonicheze ni mwanamke tuliogombana ukicheki sa hiyo mademu ninao zaidi ya mmoja na kuzinguana nishazinguana nao kibao akanambia ndo chanzo cha misala

Ila Hali ndo ilizidi kuwa tete na nyakati hizi mdo niliwaza kujitoa uhai,nilitamani Kifo kije na hakikuja
rozali, mawe na udongo kwa ajiri ya nn kama sio uchawi sasa huo
 
Mtafutie mganga
Unataka Smart911 akamegewe tunda lake "Mahondaw" kimasihara na Mganga wa jadi kama huyu? [emoji116][emoji38]
JamiiForums-1844625321.jpg
JamiiForums233507543.jpg
 
Mkuu hali unayopitia ilinikuta pia
Nilikuwa nafanya biashara na Nilifanikiwa kwa muda mchache sana ndani ya miaka mitatu ya mwanzo nilifanikiwa kuwa na hifadhi ya Hela iliyoniwezesha kujenga nyumba ya ndoto zangu,,kutokana na mafanikio ya hara wapo baadhi ya Wadau walidhani natumia Dawa(ndumba)wengi walikuwa wanaomba niwapeleke nilipoenda hata kuwa tajiri gafla katika umri wa chini ya miaka 30. Ila ukweli sikuwa kumjua mganga kabla wala kutumia ndumba zilikuwa baraka tu za MUNGU baada ya ule ujenzi tu nikaongeza Biashara ingine ya kuuza Mbao nilikuwa nafata mzigo Mafinga shambani nanunua Miti nikifikisha Mkoa ninaoishi nikawa nauza Mbao kwa gharama nafuu mnoo ikapelekea Wauza mbao wengine kuwa matatani maana ilikuwa kila mtu ni kwangu(Navunja Bei) na hili ndo likawa chanzo cha Mkosi,,wale watesi wangu walijaribu kuniangusha mimi wakashindwa nadhani labda Malaika/Mizimu ya ukoo iliamua kunilinda ila wakaagusa biashara nilishangaa tu hela zinapotea bila kujua na cha ziada mimi biashara zangu zipo eneo moja zote nasimamia mwenyewe hela napoweka najua mwenyewe na Siishi na Mwanamke kuwa labda alikuwa ananiibia hela zilipotea ndani ya mwaka mmoja nikajikuta mtaji wa Mbao umekufa nimebakiwa na biashara moja niliyoanza nayo ila nayo ipo hoi nikaingia kwenye madeni makubwa,,nilibahatisha jamaa mganga akanidanganga akanipa vidawa havikusaidia
Kufupisha stori hawa watu ni kama walinifunba macho maana napitia magumu ya kupoteza hela ila simwambii mtu siku hiyo wazo likanijia kuna shangazi yangu mtu wa kanisa sana nikaenda kwke nikamuelezea mwanzo mwisho hadi namaliza machozi yakawa yanamtoka tu alilia sana sababu nilikuwa moja ya wana familia ambao nilikuwa nawasaidai sana baadhi ya ndugu wanapokuwa na matatizo akanambia naomba leo niache nitasali usiku asbuhi nitakupa Jibu asbuhi akaniita kwake akanambia twende kanisani tukakutane na Baba Paroko tukaenda akanambia nimweleze Paroko mwanzo mwisho nikamueleza kila kitu Baba paroko alisikitika akaniambia nimpe siku tisa afunge na kusali novena atakuja na majibu
Baada ya Siku tisa aliinita akanambia ameoteshwa kuwa wakati naanza ujenzi kuna jirani mmoja tulipishana juu mpaka akanishtaki badae nikamshinda aliniwekea kisasi badae kuna biashara nikaanzisha ambayo iligusa maslahi ya watu wengine wakataka kuniangamiza kabisa ikashindikana wakaamua kunitegea kitu cha kuninyonya anadai yule jirani aloniwekea kisasi alishirikiana na jamaa alokuwa ndo Masta wa biashara mpya niliyoanzisha wakafanikiwa hilo

Mimi baada ya kuunganisha doti kweli nikakumbuka kuna Jamaa mmoja Mpare tulizinguana kisa mpaka wakati najenga na Biashara nilioanzisha nikateka Jiji ilikuwa ya Mbao

Baba paroko akanambia hakuna haja ya kugombana nao akanipatia Biblia,Rozari,Maji ya baraka,kuna udongo wa bethelehem,mawe flani ya huko huko bethelehem,na ubani flani akanipa mistari ya biblia ya kusoma kila siku vile vitu akanilekeza pakuwekea nyumbani na kazini pia nikawa na maombi maalumu ya siku 14(mimi,yeye na shangazi)

Aloo hakuna mganga kama MUNGU baada ya pale nilijikuta mambo yanarudi mdogo mdogo kuna deni la Bank nikalipa,kuna jamaa zangu walikuwa wananidai 10M nikalipa biashara ikarudi Kwenye mstari na kama miujiza mingi tu ikanipitia pitia ila nakumbuka kuna wakati ulifikaga nilitamani Kujinyonga nilitamani kifo na hakikuja ila kwa sasa Namwinua Mungu

Pole Sana kaka utafutaji una changamoto nyingi wajasiriamali tuna UpSide down nyingi

NAKUOMBEA UVUKE MAJARIBU SALAMA
Duh ndugu yani nimesoma nimeumia sana, naomba uniruhusu nikufate pm ndugu yangu kama hautojali
 
Before uende kwa mganga jiulize hili, unataka permanent solution au temporary.

Permanent, ---- Mrudie Mungu itachukia muda ila ukiwa mvumilivu utafanikiwa.

Temporary----- Nenda kwa mganga ila jiandae kuwa mtumwa wa mambo hayo na Hali yako in nearest future itakua mbaya kuliko uliyonayo hivi sasa.
Acheni akili mgando hayo masharti yako pande zote,kwa Mungu Nako Kuna Masharti tena makubwa tu! Muhimu ni Yale masharti ambayo yanakupa matokeo chanya kw upande wako.
Babu zetu hawakujua Kuna Yesu na Allah walikuwa na Miungu Yao na walifuata masharti na kufanikiwa!
Pia kama hayajakukuta ya Dunia utapuuza waganga ila kwangu nawaita WATAALAMU WA JADI, kiukweli naamini harakati zao na tangia nimekuanao karibu mambo yangu yanasonga sana tu.

Kwa ufupi ukiwa na Elimu nzuri ya darasani na kufika Elimu ya Juu alafu ukapata MTAALAMU sahihi na mzuri utafurahia matunda ya Elimu Yako na hutozulula na bashasha KAMWE riziki utazipata nyingi sana.
Nasisitiza kupata MTAALAMU SAHIHI.
 
Zamani nilikuwa naona Mfanyabiashara akifirisika labda aliendekeza Starehe au kakosea masharti ya Mganga ila yalivonikuta toka hapo Namuheshimu sana Mjasiriamali alienizidi na ambae anapitia changamoto naamini kabisa kuna mambo mengi hapaswi kulaumiwa au kusemwa vibaya
 
Acheni akili mgando hayo masharti yako pande zote,kwa Mungu Nako Kuna Masharti tena makubwa tu! Muhimu ni Yale masharti ambayo yanakupa matokeo chanya kw upande wako.
Babu zetu hawakujua Kuna Yesu na Allah walikuwa na Miungu Yao na walifuata masharti na kufanikiwa!
Pia kama hayajakukuta ya Dunia utapuuza waganga ila kwangu nawaita WATAALAMU WA JADI, kiukweli naamini harakati zao na tangia nimekuanao karibu mambo yangu yanasonga sana tu.

Kwa ufupi ukiwa na Elimu nzuri ya darasani na kufika Elimu ya Juu alafu ukapata MTAALAMU sahihi na mzuri utafurahia matunda ya Elimu Yako na hutozulula na bashasha KAMWE riziki utazipata nyingi sana.
Nasisitiza kupata MTAALAMU SAHIHI.
Usiite mawazo ya mtu akili mgando, hili ni jukwaa huru sio kila unacho amini wewe ni lazima na mimi nikiamini, we mshauri kila unacho amini ni sawa na mimi nimshauri kile kwangu naona ni sawa.

MWISHO YEYE ATACHAGUA NI LIPI LITAMFAA.
 
Haya mambo yasikie tu,unaweza kutupiwa kitu yani likitoka tatizo moja linaingia lingine kila unachofanya hakiendi,kila kitu kinafeli hadi watu wanakukimbia,kumbe unakuta kuna mtu kafanya yake anacheki movie inavyoendelea.Haya maisha usipopambana binadamu watakufanya kitu kibaya sana!Utasikia ooh alikuwa tajiri akafilisika,mzuri lakini haolewi,ana akili lakini hafanikiwi nk hapo unakuta watu walishafanya yao muda tu
 
Mkuu hali unayopitia ilinikuta pia
Nilikuwa nafanya biashara na Nilifanikiwa kwa muda mchache sana ndani ya miaka mitatu ya mwanzo nilifanikiwa kuwa na hifadhi ya Hela iliyoniwezesha kujenga nyumba ya ndoto zangu,,kutokana na mafanikio ya hara wapo baadhi ya Wadau walidhani natumia Dawa(ndumba)wengi walikuwa wanaomba niwapeleke nilipoenda hata kuwa tajiri gafla katika umri wa chini ya miaka 30. Ila ukweli sikuwa kumjua mganga kabla wala kutumia ndumba zilikuwa baraka tu za MUNGU baada ya ule ujenzi tu nikaongeza Biashara ingine ya kuuza Mbao nilikuwa nafata mzigo Mafinga shambani nanunua Miti nikifikisha Mkoa ninaoishi nikawa nauza Mbao kwa gharama nafuu mnoo ikapelekea Wauza mbao wengine kuwa matatani maana ilikuwa kila mtu ni kwangu(Navunja Bei) na hili ndo likawa chanzo cha Mkosi,,wale watesi wangu walijaribu kuniangusha mimi wakashindwa nadhani labda Malaika/Mizimu ya ukoo iliamua kunilinda ila wakaagusa biashara nilishangaa tu hela zinapotea bila kujua na cha ziada mimi biashara zangu zipo eneo moja zote nasimamia mwenyewe hela napoweka najua mwenyewe na Siishi na Mwanamke kuwa labda alikuwa ananiibia hela zilipotea ndani ya mwaka mmoja nikajikuta mtaji wa Mbao umekufa nimebakiwa na biashara moja niliyoanza nayo ila nayo ipo hoi nikaingia kwenye madeni makubwa,,nilibahatisha jamaa mganga akanidanganga akanipa vidawa havikusaidia
Kufupisha stori hawa watu ni kama walinifunba macho maana napitia magumu ya kupoteza hela ila simwambii mtu siku hiyo wazo likanijia kuna shangazi yangu mtu wa kanisa sana nikaenda kwke nikamuelezea mwanzo mwisho hadi namaliza machozi yakawa yanamtoka tu alilia sana sababu nilikuwa moja ya wana familia ambao nilikuwa nawasaidai sana baadhi ya ndugu wanapokuwa na matatizo akanambia naomba leo niache nitasali usiku asbuhi nitakupa Jibu asbuhi akaniita kwake akanambia twende kanisani tukakutane na Baba Paroko tukaenda akanambia nimweleze Paroko mwanzo mwisho nikamueleza kila kitu Baba paroko alisikitika akaniambia nimpe siku tisa afunge na kusali novena atakuja na majibu
Baada ya Siku tisa aliinita akanambia ameoteshwa kuwa wakati naanza ujenzi kuna jirani mmoja tulipishana juu mpaka akanishtaki badae nikamshinda aliniwekea kisasi badae kuna biashara nikaanzisha ambayo iligusa maslahi ya watu wengine wakataka kuniangamiza kabisa ikashindikana wakaamua kunitegea kitu cha kuninyonya anadai yule jirani aloniwekea kisasi alishirikiana na jamaa alokuwa ndo Masta wa biashara mpya niliyoanzisha wakafanikiwa hilo

Mimi baada ya kuunganisha doti kweli nikakumbuka kuna Jamaa mmoja Mpare tulizinguana kisa mpaka wakati najenga na Biashara nilioanzisha nikateka Jiji ilikuwa ya Mbao

Baba paroko akanambia hakuna haja ya kugombana nao akanipatia Biblia,Rozari,Maji ya baraka,kuna udongo wa bethelehem,mawe flani ya huko huko bethelehem,na ubani flani akanipa mistari ya biblia ya kusoma kila siku vile vitu akanilekeza pakuwekea nyumbani na kazini pia nikawa na maombi maalumu ya siku 14(mimi,yeye na shangazi)

Aloo hakuna mganga kama MUNGU baada ya pale nilijikuta mambo yanarudi mdogo mdogo kuna deni la Bank nikalipa,kuna jamaa zangu walikuwa wananidai 10M nikalipa biashara ikarudi Kwenye mstari na kama miujiza mingi tu ikanipitia pitia ila nakumbuka kuna wakati ulifikaga nilitamani Kujinyonga nilitamani kifo na hakikuja ila kwa sasa Namwinua Mungu

Pole Sana kaka utafutaji una changamoto nyingi wajasiriamali tuna UpSide down nyingi

NAKUOMBEA UVUKE MAJARIBU SALAMA
Ukisoma kisa cha huyu bwana utakubalina na Mimi kwamba hata huko kwa Yesu na Allah Kuna MASHARTI yakufuata ili ufanikiwe. Kwa ufupi tu Mafanikio yeyote lazima yaambatane na MASHARTI OVER.
Muache kubeza MASHARTI ya waganga etii oohhh kwa Waganga Kuna MASHARTI acheni kabisa huo ni upotoshaji.
 
Haya mambo yasikie tu,unaweza kutupiwa kitu yani likitoka tatizo moja linaingia lingine kila unachofanya hakiendi,kila kitu kinafeli hadi watu wanakukimbia,kumbe unakuta kuna mtu kafanya yake anacheki movie inavyoendelea.Haya maisha usipopambana binadamu watakufanya kitu kibaya sana!Utasikia ooh alikuwa tajiri akafilisika,mzuri lakini haolewi,ana akili lakini hafanikiwi nk hapo unakuta watu walishafanya yao muda tu
Inauma sanaaa
 
Back
Top Bottom