Natafuta mke tutakaye-adopt watoto pamoja naye

Natafuta mke tutakaye-adopt watoto pamoja naye

Mmm! Ila hata na ww Doris, nakuombea kwa Mungu akuhifadhi na kukulinda kwenye kiganja chake cha mkono wake. Nikisomaga michango yako, naona umeonewa sana katika mahusiano, Mungu akupe uvumilivu na hitaji la moyo wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Zinc my brother asante kwa kuligundua hilo nashukuru pia kwa maombi yako nafurahi kuona kumbe unafwatilia comments zangu asante kwa jua machungu ya moyo wangu ubarikiwe[emoji120] [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHUKUA HUU USHAURI.
1/Tatizo la mwanaume kuwa na Low Sperm count ni suala la mpito sio jambo la kudumu, ni kitu kinachotibika kitaalamu kwa 100%. Fanya uchunguzi upya katika kituo kingine cha Afya, pia tafuta tiba. Tiba ipo.

2/Kama wewe haujaoa au kama umeoa lakini hukutani na mkeo at least wastani wa mara tatu kwa wiki mfululizo kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, huwezi kusema wewe ni Mgumba. Kikubwa uume unasimama na unaweza kumwaga manii za kutosha, basi uwezo wa kumpa msichana mimba upo kwa zaidi ya 80%.

3/Tatizo la Low sperm count ni dogo sana linapokuja suala la kumpa mtu mimba, kwa sababu mara nyingi ni tatizo la mpito na linatibika kwa 100%.

4/Kama kweli imethibitika au itathibitika kwa namna zote kitaalamu kuwa wewe hauna uwezo wa kumpa msichana mimba, basi fikiria kuoa msichana mwenye mtoto tayari kuliko kutaka kuoa msichana Tasa ili kuja kufanya adoption. Kwa sababu zifuatazo...

¡/Suluhisho la ndoa yenu kuwa na mtoto litakuwa limepata suluhu tayari. Maana tayari mtoto yupo.

¡/Upendo wa dhati kwa huyo mtoto utakuwepo kwa sababu amezaliwa na mkeo.

¡¡¡/Wapo wasichana wengi sana waliozalishwa watoto na kukimbiwa na wavulana, hivyo wanalea watoto wasiokuwa na baba wanaofahamika, wasichana hao hitaji lao kubwa ni kutaka tu kuolewa na kufurahia maisha ya ndoa na wala sio kuzaa tena. Hivyo ukimpata huyo utakuwa umepata dhahabu.

¡v/Kumpata msichana ambaye hajaolewa kabisa
na asiyeweza kuzaa kabisa, akiwa na umri chini ya miaka 35 huku akijua kabisa hana uwezo wa kuzaa na akaikubali hiyo hali ni jambo gumu sana. Narudia tena, ni jambo gumu sana. Kwanini? Hawezi kujijua, hawezi kujikubali, haachi kujaribu tena na tena kulala na wanaume tofauti tofauti ili kutafuta mimba nk. Ukioa huyo mwanamke cha moto utakipata tu. Utaumizwa sana.

vi/Suala la kuasili mtoto(Adoption) lina michakato yake kisheria na changamoto zake huko mbele ya safari. Hivyo linaweza pia kukuzingua hapo mwanzoni au huko siku za usoni. Ni last option kwa wale wanandoa walioshindwa kabisa kuzaa. Sio kitu cha blah blah. Ushauri nasaha huwa unatumika sana kabla ya kuamua hilo.

v/Huenda huko mbele ya safari mambo yako yakakaa vizuri na ukaweza kumpa mimba pia. Mambo yote yanawezekana tu, kikubwa hujakata tamaa.
Dah! Hongera kwa ushauri bora kabisa. Umemaliza. Aoe mwenye mtoto/watoto ili apate upendo wa dhati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mie naamini utakuja mpa mimba tu mkeo !KUWA NA IMANI ! sitak hata kukupa pole !huna shida sana kwakweli !kila la heri kwa kutafuta TIBA
 
The best option ambalo litakulindia heshima yako ni Wewe kuruhusu either Mzazi wako wa kiume au ndugu yako kulala na mke utakae muoa, Ni gumu sana hili ila litakueka Huru na maneno maneno, Wazungu ku adopt mtoto kwao ni possible kwa vile family zao nyingi Nuclear baba mama na watoto sasa sie Africans ni extended tuna mlolongo wa ndugu watakunyima tu raha mkuu, Wachana na Mambo ya pepo au sijui Mungu, Kama kweli anakupenda Mungu Kwanini asikujalie capability ya kubebesha Mimba, BTW mkuu luse ameeleza professional kuwa tatizo lako linatibika i mean liko ndani ya uwezo don't give to early mkuu hakuna msaada wowote kutokea mawinguni huko utakaokuja kukunasua ni Wewe mwenyewe Kuamka na kuamua kutatua changamoto inayokusibu, Uniwie radhi kama ntakuwa nimeongea baadhi ya kukukera
Du! Imani aliyonayo mhusika nikubwa sana kumhusu Mungu, yupo sahihi sana. Nawe tena umeniongezea kitu fikirishi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naheshimu sana mawazo yako Ndugu yangu. Lakini naomba nieleze wazi kuwa NAKATAA KWA NGUVU ZANGU ZOTE (100%) AINA HII YA USHAURI.

Msingi wa kukataa kwangu unajengwa juu ya imani ya kiroho niliyonayo. Kuruhusu au kuridhia mke wangu alale na mwanamume mwingine tena ndugu yangu ni LAANA ISIYOFUTIKA kizazi hata kizazi. Elewa kuwa nikiwa mwafrika halisi naijua sana njia hiyo lakini nimeikataa. Naomba niseme pia naijua ile njia ya IVF ambapo unanunua mbegu za kiume za mwanaume mwingine. Nayo nimeikataa 100%

Kwangu mimi, mustakabali wangu mbele za Mungu unakuja kwanza kabla ya maslahi yangu binafsi ya kulinda jina langu, au ukoo. Wala fahari zangu binafsi hazina maana kabisa kama maana yake eti ni kulinda the so-called jina la ukoo wakati najidhalilisha mimi mwenyewe na mke wangu na huyo ndugu yangu. Never! Only over my dead body will even even be possible!

Katika njia hiyo, ku-adopt watoto ni njia nyoofu zaidi isiyo na makando-kando mbele za Mungu wala kunidhalilisha au kumdhalilisha mke wangu. Ni bora nisiwe na jina chini ya jua lakini nitunze watoto ambao hata kama hawatakuwa na jina langu lakini nitakuwa na jina mbinguni.

Na vile vile, Mungu akinijalia watoto wangu mwenyewe nitaendelea kuwalea hao yatima kama wa kwangu 100%. Nadhani tatizo hapa ni unyanyapaa tulionao juu ya watoto yatima (stigmatization).

Naomba niseme, mimi nimeishinda vita hiyo katika akili yangu na sina hata chembe ya wasi wasi ninaweza kuwalea watoto yatima na tena wakaja kuwa watu wa muhimu sana kwa ufalme wa Mungu na nchi ya Tanzania. Ninachohitaji ni kumpata mwanamke ambaye na yeye ana mawazo sawa na ya kwangu.

BUT GOD FORBID, siwezi kukubali njia ulishauri hapo juu hata kidogo!!!

As My God Lives I shall Sing of His Love Forever !!!
Mungu akujalie hitaji la moyo wako. Maneno uliyoandika kwenye thread hii yamenitia uchungu sana nikakumbuka Kaka mmoja aliyetoa shukrani jpili iliyopita kanisani kwa kupata mtoto baada ya miaka mingi na mengi kuibuka juu ya familia yake.
Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho. Wee bado ni kijana mdogo huna haja ya kukata tamaa. Najua changamoto uliyonayo na inayokusumbua ni kupata mwanamke ambaye atakubaliana na hali uliyo nayo kwani dada zetu akili zao wanazijua wenyewe. Ila nakusihi usikate tamaa maadam unatambua Mungu yupo, endelea kumuomba njia ipo nawe utafika.
 
Mungu akujalie hitaji la moyo wako. Maneno uliyoandika kwenye thread hii yamenitia uchungu sana nikakumbuka Kaka mmoja aliyetoa shukrani jpili iliyopita kanisani kwa kupata mtoto baada ya miaka mingi na mengi kuibuka juu ya familia yake.
Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho. Wee bado ni kijana mdogo huna haja ya kukata tamaa. Najua changamoto uliyonayo na inayokusumbua ni kupata mwanamke ambaye atakubaliana na hali uliyo nayo kwani dada zetu akili zao wanazijua wenyewe. Ila nakusihi usikate tamaa maadam unatambua Mungu yupo, endelea kumuomba njia ipo nawe utafika.


hapana kuna wanawake weng sana wenye kuhitaj mume dizain ya huyu mkuu ! usigeneraize mambo !
 
pole sana bro ingawa mi navyo fahamu tatizo lako linatibika mbona au ndio umeshakata tamaa mkuu?
 
Pole lkn usikate tamaa,kumbuka Millen Magese aliambiwa hatoweza kubeba mimba lkn kwa Mungu hakuna kukata tamaa,maana yeye ndio muamuzi wa mwisho sasa Millen ana mtoto wa kiume alibeba mimba
Wengi tu wanapewa majibu na madr ya kukatisha tamaa lkn wenyewe wanamgeukia Mungu na wanafanikiwa
Nione PM nikupe zaidi ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za leo wana JF.

Mimi ni kijana wa kiume rijali kabisa mwenye umri wa miaka 36. Nina elimu nzuri, mcha Mungu, nimeajiriwa, na nina ndoto za maisha vile vile. Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimethibitishiwa na madaktari kuwa nina low sperm count kiasi ambacho siwezi kumpa mwanamke mimba.

Kwa hali hiyo basi nimebakiwa na option moja ya kuasili watoto yatima. Lakini siwezi kufanya jambo hilo peke yangu. Lazima niwe na mke. Nami sikutaka kuoa mke ambaye hata kubalina na matakwa hayo.

Nimeamua kuwa sasa ni wakati mwafaka wa kutangaza nia yangu hii kwa mwanamke ambaye pengine kwa sababu moja au nyingine naye yuko katika hali ngumu kama yangu kwamba naye hawezi kubeba mimba.

Kwa aliyetayari tafadhali niPM.

Sihitaji message zozote za maudhi ambazo hazinisaidii chochote. hujafa hujaumbika. hebu usiniongezee machungu bure wakati tayari nina machungu ya kutosha. kama haikuhusu pita kimya kimya na endelea na maisha yako. Najua kuna watu katika jukwaa hili lazima wacomment kila kitu tena kwa lugha za matusi, kejeli na kukatisha tamaa. kumbuka, kile upandacho utavuna hicho hicho. Tafadhali nyamaza.

Aliyeserious tu aje PM
Mhuuuu tatizo dogo utazalisha tu usiwaze sana
 
Back
Top Bottom