mambo_safi
Senior Member
- Jul 22, 2019
- 176
- 440
- Thread starter
-
- #21
Nafikiri ukilinganisha na malipo wanayopewa wengine hii ni fair. Hapo hujauliza chakula, malazi, maradhi.Saa 15 za kazi na malipo ya 3,500!
Hakika umaskini ni mbaya mno!
Kweli kabisa! Hili tangazo ungelipeleka kwa walimu wa shule za sekondari!Hila naona walengwa wengi hawapo hapa jukwaani kwasababu hawana simu janja! Kama unaye au unamuona mtaani niunganishe tafadhari! Alafu nasikia kuna madalali wa wasichana wa kazi za ndani? Nawapataje ili niangalie jinsi ya kunisaidia!
Kwenye kazi zisizo na maslahi na za kitumwa huwezi kuajiri ndugu unaogopa maneno ila zile zenye maslahi mshahara mzuri utatafuta nduguUnadhani watu wote wanandugu wa kuajiri? Hata kama wapo unadhani wanaajirika? Hata kama wanaajilika wakati mwingine unaleta maneno kwa ndugu na malalamiko kibao ya kujihesabia haki na kutojituma na kuwa mwaminifu! Siwezi kuajiri ndugu
Hii sio kazi ya kitumwa! Kazi zenye maslahi zinamfumo ambao inabidi wote waufuate! Akizingua anatimliwa kazi kwa mjibu wa mkataba wa ajira! Kazi za ndani ni kama kazi za family members! Unamchukulia kama mwanafamilia na ukiajili ndugu ataharibu!Kwenye kazi zisizo na maslahi na za kitumwa huwezi kuajiri ndugu unaogopa maneno ila zile zenye maslahi mshahara mzuri utatafuta ndugu
Hizo ni kazi mbili tofauti, chagua moja auze duka au afanye kazi za ndani na muda wa kazi kisheria kwa Tanzania ni masaa nane yakiongezeka ni overtime sasa mshahara wa binti hapo ni shilingi ngapi na OT ni ngapi? Mimi sio mhasibu ndio maana nimeuliza hilo swali kwa mhasibu analo jibu. Wengi mnapenda kuangalia mlipoangukia hamuangalii mlipojikwa nimeeleweka kwa walio nielewa ahsante sanaAwe bado ni binti ambaye hana mambo mengi na ni Mkristo! Kama atakuwa kamaliza kidato cha nne itapendeza zaidi! Ndio nasema kidato cha nne kwasababu wengi unakuta wako nyumbani hawana issue mwisho wa siku wanaenda kuuza Baa au kudanga wapate hela ya kula.
Kazi kuu itakuwa kuuza dukani! Akiamka asubuhi saa 11 na kuweka nyumba katika hali ya usafi, anaenda kuuza dukani mpaka saa 3 usiku! Duka liko hapo nyumbani hila limejitenga na nyumba. Mshahara laki moja! Ukiwa interested njoo PM! Usidanganywe na avatar yangu mimi ni 'me'
Baadhi yenu Mnataka watoto wa watu wengine na siyo watoto wa ndugu zenu ili mkawanyanyase vizuri umfanyishe kazi kama punda asubuhi awahi kuamka kabla ya wote na usiku alale wa mwishoHii sio kazi ya kitumwa! Kazi zenye maslahi zinamfumo ambao inabidi wote waufuate! Akizingua anatimliwa kazi kwa mjibu wa mkataba wa ajira! Kazi za ndani ni kama kazi za family members! Unamchukulia kama mwanafamilia na ukiajili ndugu ataharibu!
Ni kweli ndugu yangu ni fair sana, kuna watu wanalipwa 30,000 kwa mwezi!Nafikiri ukilinganisha na malipo wanayopewa wengine hii ni fair. Hapo hujauliza chakula, malazi, maradhi.
Vyote hivyo nadhani ni juu ya mleta mada. So I think hiyo ni fair. Halafu pia kazi ya dukani kama ni binti mwenye akili anaweza kujilipa mshahara hapo hapo shop [emoji41]
Pole ndugu yangu, binafsi ningeweza kukuunganishia na ninao wajua wanaweza hio kazi lakini kwa kilicho nipata hivi karibuni hapana kwa kwakweli.Walengwa hata hapa hawapo zaidi nitaishia kwa wenye kunikatisha tamaa!
Hahahahah
Nafahamu wanapitia magumu mno, kuna mtu anatafuta hata kazi ya kufagia tu anakosa sembuse hio! Sijaibeza ofa yako hio au mimi sio kwamba nina malipo ya maana kwenye kazi yangu hapana ila ni ile value ya mtu inayopelekea kulipwa , hebu fikiria milioni moja laki mbili kwa mwaka kuna siku atatoka kwenye umaskini kweli?Unaona umasikini kwa kuwa maisha unayamudu! Hiyo ni hela nyingi kwasababu anaweza kuitunza yoote! Nyie acheni wadada wanapitia magumu!
Kuna mmoja yupo hapa ila sidhani kama ataruhusiwa kuweka makazi kwako, unapatikana wapi?Walengwa hata hapa hawapo zaidi nitaishia kwa wenye kunikatisha tamaa!
Hahahahah
Kwa kipindi hiki ukipata binti asiye na mtoto shukuru Mungu maana 99.9% wana watoto tena ni chini ya miaka 18 sasa ukimpa ajira mawili aje aishi na mwanae kwako labda hiyo kidogo itakuwa salama yako au amuache kwao kila baada ya siku mbili ruhusa ya wiki, mtoto mgonjwa, mama anaumwa na ndiye anakaa na mwanae, baba wa mtoto "kaniita kasema tukayamalize'" na mwisho unamkuta kanuna ukimuuliza jibu "nimemmisi mwanangu" kwa uzoefu wangu nawaza kwa sautiUnadhani watu wote wana ndugu wa kuajiri? Hata kama wapo unadhani wanaajirika? Hata kama wanaajirika wakati mwingine unaleta maneno kwa ndugu na malalamiko kibao ya kujihesabia haki na kutojituma na kuwa mwaminifu! Siwezi kuajiri ndugu.
Kama unataka matatizo na ndugu sawa mchukue.Kwanini hujamchukua mtoto wa ndugu yako akufanyie kazi zako za ndani umlipe?
Achana na madalali, watakuletea wasichana wa mchongo.Hila naona walengwa wengi hawapo hapa jukwaani kwasababu hawana simu janja! Kama unaye au unamuona mtaani niunganishe tafadhali! Halafu nasikia kuna madalali wa wasichana wa kazi za ndani? Nawapataje ili niangalie jinsi ya kunisaidia!
Watanzania tuna maneno mengi! Huyo binti anayetafutwa unaye wewe hapo? Ili atoe maelezo ya moja kwa moja kwa mhusika mwenye uhitaji! Zaidi ya hapo ni kuchoshana! Unakuta binti hana mbele wala nyuma kapata mahali pa kujishikisha alafu unaingiza mambo ya ILO Labour law ya mwaka 1954! Be serious broh! naiman64Hizo ni kazi mbili tofauti, chagua moja auze duka au afanye kazi za ndani na muda wa kazi kisheria kwa Tanzania ni masaa nane yakiongezeka ni overtime sasa mshahara wa binti hapo ni shilingi ngapi na OT ni ngapi? Mimi sio mhasibu ndio maana nimeuliza hilo swali kwa mhasibu analo jibu. Wengi mnapenda kuangalia mlipoangukia hamuangalii mlipojikwa nimeeleweka kwa walio nielewa ahsante sana
Asante sana umenisaidia! Kama anayemuhusika aniunganishe naye ndo tuanze kupatana au kushindwana!Watanzania tuna maneno mengi! Huyo binti anayetafutwa unaye wewe hapo? Ili atoe maelezo ya moja kwa moja kwa mhusika mwenye uhitaji! Zaidi ya hapo ni kuchoshana! Unakuta binti hana mbele wala nyuma kapata mahali pa kujishikisha alafu unaingiza mambo ya ILO Labour law ya mwaka 1954! Be serious broh! naiman64
Niletee basi mkuu!Achana na madalali, watakuletea wasichana wa mchongo.