Mkuu pole sana na masahibu yote unayopitia. Sijui kama utaupenda ushauri wangu, ila acha nikuambie kitu.
Waganga utapoteza pesa, kuendelea kujiwekea nuksi. Nachokushauri kwa Imani yako, mrudie Mungu omba toba/msamaha kwa kuamini binadamu, ndiye anayeweza kukutatulia shida zako.
Baada ya hapo mwamini yeye, kama ameweza kukuumba hashindwi jambo dogo kama kukupatia kazi na kutoa hiyo mikosi unayohisi.
Hayo ni mapito na majaribu ya dunia, kila mtu anapitia kwa aina yake. Mwisho wa siku Imani yako itakuokoa.
*Kuna kitu nitakutumia pm ufanye, utaleta mrejesho.