Natafuta mtu anayeweza kuwekeza kwa mtaji wa milioni 50 na kupata faida ya hadi milioni 70

Natafuta mtu anayeweza kuwekeza kwa mtaji wa milioni 50 na kupata faida ya hadi milioni 70

Ndugu wadau habari zenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, Mimi nipo Geita najishughulisha na biashara ya madini ya dhahabu offisi ni ya watu so Mimi ni msimamizi na wakati mwingine natoa ushauri pale inapobidi, ili kazi iwe yenye tija zaidi. Kwa upande wangu huwa tu nalipwa mshahara Kila mwezi na kama mnavyojua wadau mshahara huwa haukidhi mahitaji so utaendelea kumtumikia mtu yeye anaendelea we Bado uko pale pale.

Hivyo basi nimeamua kuandika post hi kwa mwenye kujaaliwa na Mwenyezi mtaji angalau si chini ya milioni 50 namkaribisha tufungue offisi Kwan ukiwekeza mtaji kama huwo ndani ya miezi 4 kwakuwa ndo tumeanza mauzo ni tshs 80,000,000/= hivyo ukitoa matumizi yaani mtaji faida ni tshs milioni 30.

Hivyo kwakuwa tulisharudisha gharama yaani milioni 50 kwa muhusika(mtoaji wa mtaji) haitampasa kutoa Tena hela yake kwakuwa faida ndio itakayoendesha kwa shughuli zote za uendeshaji wa kiwanda

Ambapo baada Tena ya miezi 4 kiwanda kitakuwa kimeuza madini yenye thamani ya si chini ya tshs milioni 89-120 hivyo ukitoa matumizi ya milioni 30 faida ni kuanzia milion 59 na kuendelea.

Na hiyo faida inakuwa imepatikana ndani ya miezi 4, napenda kuongezea faida itakuwa kubwa kutokana na ukubwa wa mtaji,
Mfano sisi labda tuliwekeza hiyo tshs milion 50 na faida ndo kama hyo niliyotaja hapo juu, mwingine anaweza kuwekeza labda tshs milioni 100 hvyo faida yke itakuwa mara 2.5 ya tuliyopata sisi

Mwingine anaweza kuwa amewekeza labda tshs milioni 100 na pia pembeni ana kitendea kazi kama excavator huyo huwezi kushindana nae kwakuwa faida atakayopata yeye kwa miezi 4 si chini ya milioni 500 hadi billion 1, kutokana tu na akili anavyozichezesha kwa kujiongeza kununua labda kama advanced equipment kama Trommel screen, centrifugal concentrator au anaweza kuwa na shaking table na hammer Mill ambapo akiwa navyo hvyo huku pembeni ana excavator tunaita mnyama basi anauwezo wa kupata milioni 100 Kila baada ya wiki 3.

Na kama ni mtu wa kujiongeza na kwakuwa aliwezeshwa na mnyama excavator kupata material ya kutosha Hana budi kuitumikisha excavator yaani mnyama impatie material yatakayomwezesha kupata angalau dollars za kimarekani 150000 ili aweze kuagiza toka nje CIL PLANT 200 t/d ambayo itamuwezesha kuchenjua tani 200 kwa siku.

Ngoja niweze kuwapa mchanganuo wa tani 200 kwa siku anaweza kuingiza tshs ngapi kibindoni Kila siku
Tuseme material yake yanasoma 2.2ppm( Kila tani moja in gram 2.2 za dhahabu)
Hivyo 2.2*tani 200=440gm za dhahabu

Uwezo wa CIL PLANT mara nyingi ni 94% hadi 96%, hvyo chukua gm 400 zidisha × labda tuchukue 94%
400×0.94=376gm
Uwezo wa carboni kuiachia dhahabu huwa mara nyingi haichengi 96%

376gm×0.96=360
Hivyo hiyo plant atakayonunua ataweza kupata gm 360 za dhahabu labda kwa Kila baada ya siku 2

360×15=5414.40gm
Tuangalie thamani ya gm 5414 ukiipeleka sokoni utapewa shs ngapi

Tuseme labda bei ya leo tola/ yaani gram 12 ni tshs 1400000 na material ya sehemu aliyopo labda yanasoma ubora wa dhahabu 93%

Hivyo chukua 5414.40gm×93%÷1200×1400000=587,462,400
Toa vat ambayo ni 7%(41,122,368)

587,462,400-7%=546,340,032

Hivyo atakuwa ana uwezo wa kuingiza tshs 546,340,032

Hivyo kama ni mtu wa kujiongeza atatakiwa mwenye excavator (mnyama) akodi au anunue mobile crane ya angalau si chini ya 50ton kwakuwa mnyama hatoweza kuchimba material yenye gredi nyingi za dhahabu kudeep kwenda chini hvyo mobile crane itabidi asogee eneo la tukio aweze kumnyanyu mnyama na kumdumbukiza ndani na mnyama atakuwa anachota na kupakia kwenye labda mini contena ambalo likipakizwa lisizidi tani 50 za ore, na Kila baada ya mwisho wa kazi mnyama atakuwa anatolewa ndani na mobile crane na kuwekwa nje akajipumzishe.

Nyongeza iwapo eneo ambalo mnyama(excavator) atakuwa anafanya kazi yaani ndani ya open cast kumetokea maji na material ya hapo ni tope mnyama hatoweza kufanya kazi kwa ufanisi labda kwakuwa itakuwa open cast ipo deep sana so haitatusumbua akili kwakuwa pesa ipo tutaagiza au kununua mnyama mwingine aliyetengenezwa kwa ajili ya eneo la tope na maji maji (amphibious).
Nyongeza, amphibious excavator tunaweza kutumia double girder over head crane kwa ajili ya kuidumbukiza na kuitoa.

Wakuu hayo ni mawazo yangu kwenda kwenu kwa kuwafungua macho kwa wale wenye pesa zao zimekaa tu na hawajui wafanye biashara gani au ana miliki excavator na imekaa haimuingizii hela na ameamua kuingiza sokoni na huu mwaka wa pili unaenda wa tatu na hakuna mteja aliyepatikana kwa ajili ya kuinunua na mda unaenda.

Kwa mwenye kutaka ushauri anaweza kunicheki WhatsApp no. 0754028641
Mateli kama nyinyi nawaambiaga muende benk mkakope maana mabenki wana tafuta kukopesha biashara zinazilipa kama hizo
 
Hahhaaa utanikuta..naukumbuka ule mpango mkakati wa kuzuru kaburi😀😀
Yaan Jf wakigoma mie nitafanya mpango na wadau wachache hata Mia hvi kwa niaba ya JF tukazuru na kutembelea hiyo bustani ya wanyama pori chato maana siku hizi wanaiita hivyo lakini t- shart zote lazima ziwe na chata ya Jf na bendera Fulani hivi wewe utakuja kutupokelea tinde
 
Hahhaaa utanikuta..naukumbuka ule mpango mkakati wa kuzuru kaburi😀😀
Wangari mtoto wa kisukuma mzima?
Muanzisha mada ametiririka ukweli.
Tatizo watz kila kitu tunawaza kupigwa.
Mimi kuna dogo alikataa fursa ya bure ya kuwa right hand man wa mzoefu wa madini ili apate kujifunza. Sasa hivi analialia. Angechota uzoefu. Maana huyo mwamba nguli hasa mnyamwezi wa Unyanyembe. Siku hizi yupo zake Uswisi.
 
Mkuu...ukiwa na 50m ukaamua kuwa na jiko..yaan.hapo usiinyofoe sijui ulipie pango sijui ununulie mzan wa dhahabu hiyo 50m ukiingiza yote ukawa unanunua kwa makota..yaan makota wanakuletea ww..uhakika wa kupata 20m kwa mwez kama faida ni mkubwa...unaangalia wenzako wananunulia kwa shilngi nhap..mfano wanunue kwa 115,000/ wewe nunulia kwa 116,000! Utawapata wanyantuzu kibao .ila na ww unawaminya kwenye purity..kama dhahabu yake ni safi tuseme inasoma 92 ww hakikisha inasoma 88%( faulo)! Ndo wanavyofanya .hapo umekula ganji ndefu sana! So buku yako inarudi mara 4! Ukitaja upotee uweke hisa maduarani ..! Hiyo huwa 50/50! Lakini wapo wanaopata hela mtakato kupitia hayo maduara
Inaonekana unaielewa sana hii busness
 
Wangari mtoto wa kisukuma mzima?
Muanzisha mada ametiririka ukweli.
Tatizo watz kila kitu tunawaza kupigwa.
Mimi kuna dogo alikataa fursa ya bure ya kuwa right hand man wa mzoefu wa madini ili apate kujifunza. Sasa hivi analialia. Angechota uzoefu. Maana huyo mwamba nguli hasa mnyamwezi wa Unyanyembe. Siku hizi yupo zake Uswisi.
Nipo mzee baba...aliogopa nn sasa? Kama hujawah kusikia figures kubwa kubwa lazima huku ushangae..hahaa! Majitu yanakula kimya kjmya kule aise tena ss hv list wa matajiri itashoot...maana jemadari amekwenda...ss hv zitasafirishwa balaa
 
Yaan Jf wakigoma mie nitafanya mpango na wadau wachache hata Mia hvi kwa niaba ya JF tukazuru na kutembelea hiyo bustani ya wanyama pori chato maana siku hizi wanaiita hivyo lakini t- shart zote lazima ziwe na chata ya Jf na bendera Fulani hivi wewe utakuja kutupokelea tinde
😀😀😀 mm nimo kwa hiyo list...mie ntawapokea mkuu hata hapo tinde si mbaya!
 
Mkuu...ukiwa na 50m ukaamua kuwa na jiko..yaan.hapo usiinyofoe sijui ulipie pango sijui ununulie mzan wa dhahabu hiyo 50m ukiingiza yote ukawa unanunua kwa makota..yaan makota wanakuletea ww..uhakika wa kupata 20m kwa mwez kama faida ni mkubwa...unaangalia wenzako wananunulia kwa shilngi nhap..mfano wanunue kwa 115,000/ wewe nunulia kwa 116,000! Utawapata wanyantuzu kibao .ila na ww unawaminya kwenye purity..kama dhahabu yake ni safi tuseme inasoma 92 ww hakikisha inasoma 88%( faulo)! Ndo wanavyofanya .hapo umekula ganji ndefu sana! So buku yako inarudi mara 4! Ukitaja upotee uweke hisa maduarani ..! Hiyo huwa 50/50! Lakini wapo wanaopata hela mtakato kupitia hayo maduara
to be honest wew ni mmoja wa wanawake 10 ndani ya jf ambao i wish nikutane nao japo dakika 10 tu maishani mwangu
 
Maelezo ya mkuu hapo juu yameelezea mradi timilifu bila kuorodhesha changamoto zinazoweza kutokea kwenye huo mradi, maana kama ni kweli hiyo kitu inafaida hivyo naamini kundi kubwa la wawekezaji lingeshajazana huko kama kawaida yetu ya kuigana kwenye maswala ya ujasiliamali.
 
Back
Top Bottom