Natafuta mtu mwenye asili ya Kihindi kumuajiri au kufanya naye biashara

Natafuta mtu mwenye asili ya Kihindi kumuajiri au kufanya naye biashara

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
13,588
Reaction score
22,752
Jaman mimi ni muajiriwa nafasi fulani ya juu kidogo hapa nchini. Nimeweza kupata mil 70 ambayo ni matokeo ya SAVING ya muda mrefu na hela zangu fulani nilikuwa nazidai kulipwa.

Mpango nilionao ni kuanzisha biashara ya spears za pikipiki na tri cycles (guta au Toyo). Changamoto niliyonayo ni kuwa mimi muda mkubwa wa usimamizi sina, nimewaza kumuweka wife naye kasema hawezi acha ajira yake aingie kwenye biashara ambayo hata haijui (in short wife sio mtu wa biashara).

Nikawaza nipate hata msichana mmoja wa Kichaga mwenye uwezo wa kutumia computer kwa sababu nimepanga niweke CCTV CAMERA na MFUMO WA MAUZO WA KIDIGITAL ila bado imani na hawa watu weusi sina kabisa. Nilishafungua ka biashara cha hizi simu ndogo maarufu kama viswaswadu nikaweka mtoto wa Aunt alichonifanya sina hamu hata ya kuhadithia.

Nirudi kwenye mada iliyonifanya nifungue uzi huu sasa. Nimewaza nipate Muhindi ili nimuajiri au tufanye kama partnership, i mean yeye awekeze kwenye Management mimi CAPITAL kwa sababu target yangu mimi ni kuua biashara za wenye viduka vidogo vidogo vya spear hapa wilayani ili nitawale soko kwa mikakati ifuatayo:

1. Kuteka mafundi wazuri wa injini, umeme na mechanics wazuri wenye jina kwa kuwalipa kukaa mbele ya duka langu ambalo lipo hapa city center.

2. Nimepata eneo ambalo lipo kando kando ya barabara hapa mjini ambalo kwa mbele lina uwazi mkubwa kiasi cha kuweza ku accomodate mafundi wengi mbele.

3. Kazi yangu nadeal sana na watu wa nje i mean wazungu,wachina Waindi n.k hivyo nina rafiki zangu wachina huwa wanaagiza na kufuata containers za spears huko china na wana duka la jumla KKOO hivyo wameniambia kwenye order zao wata include na yangu ili nipate kwa bei nzuri.

4. Kuuza kwa bei ya vunjabei kwa sababu mimi nitapata kwa bei ya chini sana hivyo ni rahisi kunifikia mzigo kwa bei ndogo sana.

5. Kuwa na offer kila jumamos kila ataekuja pale dukani kufanya services na maintenance atajaziwa mafuta nusu lita kama offer kila mmoja.

Anyway nimewaza ili mipango yangu iende sawa nahitaji mtu wa kusimamia alie serious ila wabongo siwataki kwa sababu za tabia zetu za WIZI, UMALAYA, UVIVU, EXCUSES NA UJINGA UJINGA AMBAO BILA KUPATA WA KUVICONTROL HULETA HASARA KWENYE KAMPUNI.

NB: Mwenye jamaa m INDIA 🇮🇳 anaejielewa aje inbox please usiniletee WAPEMBA nataka Muhindi nitamlipia PERMIT ili tufanye kazi ili tunyanyuke wote.
 
Kupania kufanya kitu na kuingia mazima ni tofauti kabisa
Unaposema unataka uuwe biashara za watu wadogo hapo ndio umeharibu kabisa
Kwanini usiwe Wholesaler tu na ukashusha container zima ila ukaweka vifaa vinavyoisha haraka kwenye guta na pikipiki?
Hapo utawauzia hao hao unaowapania kabla hujaanza
Wakati mwingine kutenda hayo ya kuwatoa sokoni mara nyingine yanakugeukia wewe na unajikuta senti zako hizo zinayeyuka na hapo kuwa chanzo cha kuanza kumtafuta mganga

Kuweka mafundi mbele ya duka ni sawa ila wao watapatana? Na je unafikiri watanunua kila bidhaa kwako?

Maana kama wewe unawaza hivi na wao wanawaza vile
Nakuombea kila la kheri ila kama hukai mwenyewe bora uache tu
 
Uaminifu -na management ndo msingi wa biashara na mafanikio.

Ukikosa muhindi wapo waswahili pia waaminifu sema mpaka umpike aelewe kuwa wizi haufai.

Wahindi huwa wanaamini ukiiba umejiibia wewe mwenyewe mambo ya karma wanayajua Sana so wana embrace honest .

Niseme umewaza sahihi mkuu mchakato wa kuwa tayari kuinuka na MTU ni mchakato ambao upo attached spirituality.
 
Hata mbongo unaweA muweka chamsingi hakikisha stock unaimonitor kila siku ukitoka kazini na kuhakikisha unakagua hesabu kila siku.

Anyway kwa muhindi landa uingie nae patnaship tu
Hiyo ukaguzi wa kila siku ndo kazi ngumu kwangu kwa sababu vifaa vya pikipiki ni vidogo vidogo na pia mimi huwa nasafiri sana nataka kumuacha mtu huku nyuma ninaemuamini ambae anaweza jisimamia
 
Muhindi kwa mtaji wa milioni 70 utakuwa unamlipa bei gani? unamtoa India au waliozaliwa hapahapa?

Biashara kama huwezi kuisimamia mwenyewe mda wote hata ungemuajiri mke wangu itakufa tuu.

Watanzania wengi hawana exposure mtu ana milioni 70 ila bado anawaza biashara za uchuuzi? sasa mwenye milioni mbili atawaza nini?

Man up, you can do better.
Come on.
 
Unaanzia kwenye uchuuzi ndio unakua mkubwa..., hakuna substitute ya experience ndio maana nawaambia watu kila siku wekeza kwenye hobbie au jambo kitu unachokifanya / unachokifahamu au kukipenda.... Pesa ni ingredient pia lakini inaweza isiwe nguzo kuu...

Aanze kidogo na kukua gradually (learning from experince)
 
Kupania kufanya kitu na kuingia mazima ni tofauti kabisa
Unaposema unataka uuwe biashara za watu wadogo hapo ndio umeharibu kabisa
Kwanini usiwe Wholesaler tu na ukashusha container zima ila ukaweka vifaa vinavyoisha haraka kwenye guta na pikipiki?
Hapo utawauzia hao hao unaowapania kabla hujaanza
Wakati mwingine kutenda hayo ya kuwatoa sokoni mara nyingine yanakugeukia wewe na unajikuta senti zako hizo zinayeyuka na hapo kuwa chanzo cha kuanza kumtafuta mganga

Kuweka mafundi mbele ya duka ni sawa ila wao watapatana? Na je unafikiri watanunua kila bidhaa kwako?

Maana kama wewe unawaza hivi na wao wanawaza vile
Nakuombea kila la kheri ila kama hukai mwenyewe bora uache tu
Umesomeka ndugu hii ni mikakati maana biashara ni kama vita nimekosea ku expose hii mikakati ila nimefurahi kunionesha upande wa pili wa mipango yangu
 
Kupania kufanya kitu na kuingia mazima ni tofauti kabisa
Unaposema unataka uuwe biashara za watu wadogo hapo ndio umeharibu kabisa
Kwanini usiwe Wholesaler tu na ukashusha container zima ila ukaweka vifaa vinavyoisha haraka kwenye guta na pikipiki?
Hapo utawauzia hao hao unaowapania kabla hujaanza
Wakati mwingine kutenda hayo ya kuwatoa sokoni mara nyingine yanakugeukia wewe na unajikuta senti zako hizo zinayeyuka na hapo kuwa chanzo cha kuanza kumtafuta mganga

Kuweka mafundi mbele ya duka ni sawa ila wao watapatana? Na je unafikiri watanunua kila bidhaa kwako?

Maana kama wewe unawaza hivi na wao wanawaza vile
Nakuombea kila la kheri ila kama hukai mwenyewe bora uache tu

Aachane na story za kuua biashara za watu, cha msingi kama anaweza kupata vifaa kwa bei cheap, awe whole seller.
Hiyo garage iweke kwingine na duka liweke kwingine, ziwe biashara 2 tofauti
 
Una mawazo ya kitumwa Bado.

Wahindi walisifiwa sababu ya ELIMU ya biashara ambayo zamani haikuwepo kwetu.

Sasa Maarifa yapo na wahitimu Toka VYUO vya ndani ni wengi,

Ikiwa tatizo la wengi ni kukosa Maadili, basi Tafuta msomi aliyeokoka Kweli Kweli muweke hapo.

Pia ml 70 ni pesa ndogo sana kuwekeza kwenye biashara ya spea.

Kwa mipango uliyonayo, inahitaji milioni 200 na kuendelea, hivyo unahitaji milioni 140 ingine.

Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom