Mkuu kuhusu ubia h
Mkuu kuhusu ubia hili sio wazo zuri.. mimi sio mfanya biashara lakini elimu ya biashara naijua kiasi, ubia sio mzuri kwa maisha yako hata kwa familia yako hapo baadae siku ambazo wewe utakuwa haupo, ubia una changamoto nyingi, migogoro mingi sana ikiwemo changamoto kwenye suala la utoaji maamuzi, kutofautia kimawazo, visasi vya ajabu ajabu, kukomeshana, ubishi, kutokuwa na uaminifu kwa baadhi ya wamiliki, kuzungukana kwenye biashara, kutengenezeana hasara feki kwenye biashara, kulogana, kila mtu kutaka ubosi, kila mtu anataka awe yeye ndo yeye kwenye biashara e.g CEO pamoja na hayo yote huwezi kumkaripia mmiliki mwenzio, huwezi kumfukuza, huwezi kumshitaki kienyeji huwezi kumhoji hoji hovyo n.k
Haya yote yateleta mkanganyiko kwenye biashara hatimae biashara kufa, suala la ubia lina hitaji umakini sana kuliko kutafuta mfanyakazi unayeweza kumtimua muda wowote lkn pia mfanyakazi atafanya kazi kwa kuogopa kutimuliwa,, Fanya biashara wewe mwenyewe mkuu