Natafuta mtu mwenye asili ya Kihindi kumuajiri au kufanya naye biashara

Natafuta mtu mwenye asili ya Kihindi kumuajiri au kufanya naye biashara

Muhindi kwa mtaji wa milioni 70 utakuwa unamlipa bei gani? unamtoa India au waliozaliwa hapahapa?

Biashara kama huwezi kuisimamia mwenyewe mda wote hata ungemuajiri mke wangu itakufa tuu.

Watanzania wengi hawana exposure mtu ana milioni 70 ila bado anawaza biashara za uchuuzi? sasa mwenye milioni mbili atawaza nini?

Man up, you can do better.
Come on.
Wahindi ni cheap labour nilikuwa Advent mwaka 2014 na engineer wa kihindi walikuwa wanalipwa 250k kwa mwezi.
 
Jaman mimi ni muajiriwa nafasi fulani ya juu kidogo hapa nchini. Nimeweza kupata mil 70 ambayo ni matokeo ya SAVING ya muda mrefu na hela zangu fulani nilikuwa nazidai kulipwa.

Mpango nilionao ni kuanzisha biashara ya spears za pikipiki na tri cycles (guta au Toyo). Changamoto niliyonayo ni kuwa mimi muda mkubwa wa usimamizi sina, nimewaza kumuweka wife naye kasema hawezi acha ajira yake aingie kwenye biashara ambayo hata haijui (in short wife sio mtu wa biashara).

Nikawaza nipate hata msichana mmoja wa Kichaga mwenye uwezo wa kutumia computer kwa sababu nimepanga niweke CCTV CAMERA na MFUMO WA MAUZO WA KIDIGITAL ila bado imani na hawa watu weusi sina kabisa. Nilishafungua ka biashara cha hizi simu ndogo maarufu kama viswaswadu nikaweka mtoto wa Aunt alichonifanya sina hamu hata ya kuhadithia.

Nirudi kwenye mada iliyonifanya nifungue uzi huu sasa. Nimewaza nipate Muhindi ili nimuajiri au tufanye kama partnership, i mean yeye awekeze kwenye Management mimi CAPITAL kwa sababu target yangu mimi ni kuua biashara za wenye viduka vidogo vidogo vya spear hapa wilayani ili nitawale soko kwa mikakati ifuatayo:

1. Kuteka mafundi wazuri wa injini, umeme na mechanics wazuri wenye jina kwa kuwalipa kukaa mbele ya duka langu ambalo lipo hapa city center.

2. Nimepata eneo ambalo lipo kando kando ya barabara hapa mjini ambalo kwa mbele lina uwazi mkubwa kiasi cha kuweza ku accomodate mafundi wengi mbele.

3. Kazi yangu nadeal sana na watu wa nje i mean wazungu,wachina Waindi n.k hivyo nina rafiki zangu wachina huwa wanaagiza na kufuata containers za spears huko china na wana duka la jumla KKOO hivyo wameniambia kwenye order zao wata include na yangu ili nipate kwa bei nzuri.

4. Kuuza kwa bei ya vunjabei kwa sababu mimi nitapata kwa bei ya chini sana hivyo ni rahisi kunifikia mzigo kwa bei ndogo sana.

5. Kuwa na offer kila jumamos kila ataekuja pale dukani kufanya services na maintenance atajaziwa mafuta nusu lita kama offer kila mmoja.

Anyway nimewaza ili mipango yangu iende sawa nahitaji mtu wa kusimamia alie serious ila wabongo siwataki kwa sababu za tabia zetu za WIZI, UMALAYA, UVIVU, EXCUSES NA UJINGA UJINGA AMBAO BILA KUPATA WA KUVICONTROL HULETA HASARA KWENYE KAMPUNI.

NB: Mwenye jamaa mwenye asili ya INDIA 🇮🇳 anaejielewa aje inbox please usiniletee WAPEMBA nataka Muindi nitamlipia PERMIT ili tufanye kazi ili tunyanyuke wote.
Labda makaburin utampata wanavyoogopa mitandaoo
 
Muhindi atakuibia akaanzishe duka au kampuni yake.
Mbongo atakuibia apate pesa ya kwenda kuhonga mademu wenye matako makubwa bar na kununua ist.
Chaguo ni lako
 
Una mawazo ya kitumwa Bado.

Wahindi walisifiwa sababu ya ELIMU ya biashara ambayo zamani haikuwepo kwetu.

Sasa Maarifa yapo na wahitimu Toka VYUO vya ndani ni wengi,

Ikiwa tatizo la wengi ni kukosa Maadili, basi Tafuta msomi aliyeokoka Kweli Kweli muweke hapo.

Pia ml 70 ni pesa ndogo sana kuwekeza kwenye biashara ya spea.

Kwa mipango uliyonayo, inahitaji milioni 200 na kuendelea, hivyo unahitaji milioni 140 ingine.

Ni hayo tu.
Wewe hiyo M200 unayo? Hata hiyo 70M unayo? Acha kumkatisha tamaa kijana wakati hapo ulipo mdomo unanuka kwa njaa.
 
Back
Top Bottom