Natafuta mwenza (Mchaga) wa maisha. Ninaishi hapa Dar es Salaam

Natafuta mwenza (Mchaga) wa maisha. Ninaishi hapa Dar es Salaam

Mr Ballo

Member
Joined
Apr 21, 2024
Posts
43
Reaction score
83
Habari wanajamii, natumaini mnaendelea vyema.

Mimi ni mwanamume mwenye umri wa miaka 38, naishi hapa Dar es Salaam.
Natafuta mwenza wa maisha mwenye malengo ya dhati na uhusiano wa muda mrefu.

Mimi ni Mkristo(Lutheran) ninapenda na ninathamini Mahusiano ya kuzingatia Heshima, Upendo wa Dhati na Maridhiano.

Ningependa kufahamiana na mwanamke mwenye umri wa kati ya miaka 25 hadi 35, anayejiheshimu, mwelewa, na mwenye mtazamo chanya wa maisha.

"Nikimpata Mchaga ntashukuru zaidi"

Nimejaliwa kuwa na watoto na ninaishi na wanangu.

Kama unadhani tunaweza kufahamiana zaidi, tafadhali niandikie ujumbe wa moja kwa moja (DM) au tuanze mazungumzo hapa.

Asanteni kwa muda wenu.

Natumaini kupitia nafasi hii nitakutana na mtu maalum na naomba wale wote wenye masihara wajiepushe na andiko hili.(Niko serious)
 
Back
Top Bottom