Natafuta rafiki wa kike

Kichwa chajieleza.

Mimi ni Male.

Naitaji rafiki wa kike, anayependa kusoma na mwenye mawazo makubwa sana ya kimaendeleo, uwezo mkubwa wa kung'amua mambo sio story za paka kala mkate.

Note. nahitaji rafiki sio mpenzi.
 
SIFA ZAKE
Anajitegemea kiuchumi na hapigi vizinga
Asiwe mke au mchumba wa mtu
Asiwe na wivu kupitiliza
Awe anajiheshimu (Sio kicheche)
Awe amepevuka kimaisha
Awe tayari kupima VVU

SIFA ZANGU
Najitegemea kiuchumi
Mstaarabu na muelewa
Umri nipo btn 35 and 40
Sina wivu wa kijinga
Ninajiheshimu
Nipo tayari kupima VVU
Status ya mahusiano nitakueleza.
 
Mie nipe namba ya Sister hapo niwe rafiki yake.
 
Mkuu mbna pm hujibu?? Au umemptaaa
 
ngoja watakuja duu just a friend je badae mki fall in ....itakuwaje would u take it like for real
 
Habari!
Mimi ni mwanaume wa miaka 28,najitokeza kwenye jukwaa hili kutafuta rafiki wa kike ambaye baadaye tutakuja kuanzisha mahusiano ya kimapenzi kama tutaridhiana.Nimeleta bandiko hili hapa kutokana na utayari wangu wa ku-date kwa sasa lakini nipo katika mazingira magumu kiasi ya kukutana na watu wapya ama watu sahihi.

Mimi ni mwajiriwa serikalini,elimu yangu ni diploma na Dini yangu ni mkristo wa KKKT.Mambo mengine kuhusu mimi nitayajibu PM kwa kadri mtu atakavyoniuliza.
Sifa za mwanamke ninayemtaka awe mkristo umri kuanzia miaka 19 mpaka 24,level yeyoye ya elimu ila certificate au diploma napendelea zaidi,nahitaji mwanamke wa kumpenda kwa moyo wangu wote na nijaribu kumpenda yeye pekee

So nazingatia sana uzuri wa sura na umbo pia,navutiwa na wanawake warefu wenye maumbo namba nane,asiwe mnene.Mimi ni mwaminifu sana na naheshimu sana miongozo ya dini so nahitaji mwanamke mwenye hofu kubwa sana ya

Mungu na asiyechukulia ngono kama ni kitu cha kawaida tu,mwanamke mwenye clean history ataniteka zaidi.Naishi Dar es salaam kwa sasa so aliye jirani ni vizuri zaidi japo sitajali umbali kama atapatikana mtu sahihi.

Sijui niweke vipi hili la mwisho ila kuna makabila kama wachaga,wahaya na wazaramo wamekuwa wakichukuliwa kwa mtazamo hasi sana na jamii kwenye mambo kadhaa,nimejikuta tu sina amani na hayo makabila sababu ya mapokeo japo najua sio busara kujaji mtu kwa sababu ya matendo ya watu wengine.

Naelewa masharti niliyoweka ni mengi,lakini nimeona ni heri niwe muwazi,niseme ninachojisikia na niombe ninachotaka ila Mungu atimize sawa sawa na haja za moyo wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…