Natafuta Santuri (CD kubwa za zamani aina ya Gramophone)

Natafuta Santuri (CD kubwa za zamani aina ya Gramophone)

halafu unazipigia kwenye nini sasa wakati redio zake hakuna?
Machine yake inaitwa gramophone ndugu, unaiona hapo kwenye picha? Mie natafuta hizo santuri. Machine zake ziko nyingi sana na katika pita pita zangu nimezikuta sana mkoani Kilimanjaro shida kubwa ni kupata pin zake. Pin zake zinawahi kuchoka. Unaweza piga nyimbo moja tu pin ikafeli huo ndo mtihani mkubwa. Ila kuna wadau wanazisakanya Kenya. Kwa yeyote anayetaka pin unaweza mcheki huyu mzee wa Kimakonde yuko gerezani k/koo anazo 0713 848682 (anajulikana kwa jina maarufu BONGE).

IMG-20170429-WA0018.jpg
 
View attachment 1846132
Ndugu hii ni ya kuendesha kwa mkono au inatumia umeme?
 
Duuuh mkuu nilikuwa nazo nyingi Sana pamoja na limaashine lake lilikuwa kubwa Kama kabati panya walikuwa wamelishambulia mwezi uliopita nikalichoma moto pamoja na santuri zake zaidi ya 200 yaani ningekupa bure kabisa.
 
Umeharibu mie ningekupa hela kwa kuzitunza tu. Unajua wengi huwa wanazitupa hawana kazi nazo kabisa. So sad
 
Aisee mbona kama unajichosha sana kutafuta hayo masanturi ya zamani! Hizo nyimbo za zamani baada ya kuzipata unazifanyia nini?

Au una kipindi cha redio unakiendesha?
Kikubwa kwenye uandishi huwa tunaandika vitabu vya historia ya wasanii
Mfano Shaban Robert aliandika shairi la kiswahili 1922, kwa mda huo teyari kiswahili kilikuwa maarufu sana. Kuna watu wengi wanaamini kiswahili kulikuja na mwalimu Nyerere.

Mie nina santuri zaidi ya elfu 3 huwa nanunua zile ambazo sina au ambazo zinakuwa haziimbi vizuri. Kuna vitabu vingi vimeandikwa hususani vya wasanii wakubwa kwa mfano Siti Bin Saad. Ndani ya vitabu vyake unaweza ona shuguli zilizokuwa zinafanywa na waafrica na alitembelea maeneo mengi nje ya nchi na hiyo ilikuwa kabla ya uhuru.

Nyimbo hizi zimeimbwa kwa lugha mbalimbali, na kuna nyimbo za kuabudu, nyimbo za kusifu, nyimbo za kuhamasisha nk. Tuna mengi ya kujifunza na historia ya mtu mweusi kabla ya ukoloni haijulikani sana. Kwenye hizi santuri kunaweza kupatikana historia mfano nina santuri linamzungumzia Mangi Horombo, (wilaya ya Rombo Kilimanjaro imetokana na huyu mangi Horombo). Katika hii santuri ambayo imeimbwa kichaga inamsifia mangi Horombo kwa kuua tembo mwenyewe bila msaada akiwa kijana tu na mapambio mengi tu

Sijui kama nitakuwa nimekujibu vya kutosha kama hujaelewa na hapa nitakupigia simu nikufafanulie. Shukran..
 
Unakusanya kitu usichojua! Hizo sio CD! Ni LP (vinyl)
Aisee ndugu yangu mie nazijua kushinda unavyojua wewe

LPs kuna 45 rpm na 33 1/3 rpm na ninazo ila sizihitaji hizi. Kwa kiswahili cha kipindi kile hizi ziliitwa maplayer na zilikuja na miziki ya album.

Binafsi natafuta mziki kablsa ya LP, uko kwenye santuri na sio maplayer. Kwa jina la kizungu nazotafuta mimi zinaitwa Gramphone Records. Nafanya hizi kazi za santuri for more than eight years nazijua sana kushina unavodhani. Mie nafanya kazi na hizi kwa nini nisijue kazi yangu?

Nadhani utakuwa umenielewa. Kama hujanielewa notakupigia nikufahamishe. Shukran. .
 
umenikumbusha Lp ya Sam Mangwana- maria tebola
LP ni za karibuni hapa, mie natafuta zile za udongo sijui kama ulizikuta. Nadhan ziliishia mwanzoni wa miaka 70. Ndio zikaja hizo LP zinakuwa album. Ila zile za santuri inakaa nyimbo moja tu one side
 
Nanunua hizo 78 rpm (zinajulikana kama santuri). Sizihitaji LP (maplayer) ambazo ni 45 rpm na 33 1/3 rpm. Naweka tofauti kwenye picha hapo chini
1626118236341.jpeg
 
Back
Top Bottom