Natafuta sehemu nzuri ya kuishi ndani ya Tanzania

Habari zenu wakuu

Sehemu ninayoitafuta iwe na huduma za muhimu karibu kamavile MAJI, HOSPITAL, UMEME NA MTANDAO WA SIMU UWE UNAKAMATA 4G BILA USUMBUFU

Sehemu hiyo isiwe mkoa wa Dar, Kilimanjaro au Arusha!

Karibuni wadau mtiririke
Nakutajia miko ambayo huwezi shindwa ishi hata kama huna hela
1.mbeya
2.iringa
3.morogoro
4.ruvuma
5.njombe
6.rukwa
Mkuu umeisahau mwanza
Mwanza hapana kuna ukame pamoja na kwamba mpunga upo lakini sehemu kubwa ya mkoa wa mwanza ni kame ndio maaana asilimia kubwa wasukuma wamekuwa wahamiaji mkoa wa morogoro.
 
Mkuu dar sio pakame mkuu.... Mbona watu wamejazanaaa
 
4G isiyokata?

Hadi hapa hakuna
 
1. Hata Ileje?
2. Hata Kilolo?
3. Hata Mahenge?
4. Hata Namtumbo?
5. Hata Waging'ombe?
6. Hata Tanganyika?
 
Nyumba nzima nzuri kupanga shilingi ngapi?
 
Sehemu yoyote ambayo ardhi ni mali ya ukoo na hupeana law kurithisha na sehemu yenye makao ya kudumu shambani hapamfai mtu zaidi ya mwenyeji
 
Huko panatajwa sana
Lushoto na njombe ni mapacha ingawa njombe barid imezid kidogo ,lakin kilakitu unacho pata njombe basi na lushoto unapata kuanzia aina za vyakula , matunda na mimea mingine yaan kifupi hapana ukame wa chukula ingawa mzunguko wapesa wa lushoto hutegemea sana tanga mjini tofauti na njombe ambayo hata mzunguko wa pesa wa ndani ni mkubwa
 
Sehemu yoyote ambayo ardhi ni mali ya ukoo na hupeana law kurithisha na sehemu yenye makao ya kudumu shambani hapamfai mtu zaidi ya mwenyeji
Wee unaongelea bukoba vijijini huko,muleba,misenyi na karagwe kwenye vijiji.huko hata sikishauri.


Bukoba mbona KUna viwanja kibao. Nenda manispaa utafute kiwanja hutakosa kamwe. Mbona kumejaa wasukuma waha na wakurya kibao bukoba?
Lakin hata pembeni ya miji kama bukoba kuna viwanja zaidi ya 5000 vimepimwa 2012 vinasubiri wateja.


Mbona kuna mashamba kibao ya miti ya watu kutoka mikoani?
 
Habari zenu wakuu

Sehemu ninayoitafuta iwe na huduma za muhimu karibu kamavile MAJI, HOSPITAL, UMEME NA MTANDAO WA SIMU UWE UNAKAMATA 4G BILA USUMBUFU

Sehemu hiyo isiwe mkoa wa Dar, Kilimanjaro au Arusha!

Karibuni wadau mtiririke
Nenda Ndala kule Tabora.
 
Ntarudi tena bukoba miaka mi3 ilitosha sana kuenjoy maisha na kuijua bkb.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…