Natafuta viashiria muhimu vya CCM kuanguka uchaguzi unaokuja na upinzani kushinda sivioni

Natafuta viashiria muhimu vya CCM kuanguka uchaguzi unaokuja na upinzani kushinda sivioni

Hili swala Bandari ,watu kuondolewa kwenye makazi yao ya miaka na miaka,vitu kupanda bei kiholela Kila kukicha,kupanda Kodi ya majengo ...##inshort halibua kiuchumi ni mbaya mtaani na inaonekana hali itaendelea kua mbaya zaidi
Uko sahihi kabisa hali ni mbaya na Kuna dalili itakuwa mbaya zaidi ila hata hayo wananchi hawaoni ni nani ana solution ya hizo shida
 
Kama mada inavyojieleza hapo juu na kama waswahili wasemavyo wa kushiba huonekana mezani, awamu hii tofauti sana na hali ilivyokuwa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015, sijaona viashiria vingi muhimu vinavyotoa matumaini ya ccm kuanguka katika uchaguzi unaokuja.

Mwaka 2015 kulikuwa na vuguvugu kubwa sana la kisiasa kiwango cha kushawishi hata baadhi ya waliopata kuwa mawaziri katika serikali ya ccm kuhamia upinzani.

Mbali na hiyo hama hama Toka chama tawala kwenda ccm iliyojulikana kama kimbunga Kila Kona ya nchi kulikuwa na mijadala mingi sana iliyokuwa na mwelekeo wa kuichoka ccm na kuuchoka ufisadi uliokithiri miongoni mwa watawala.

Zaidi ya hayo hata chaguzi ndogo zilizoitishwa kipindi hicho ziliipa wakati mgumu sana ccm hata kama walishinda iliwalazimu kushinda Kwa mbinde sana.

Oparesheni zilizofanywa na wapinzani zilikuwa na mguso na mvuto mkubwa sana Kwa wananchi, hali ni tofauti sana awamu hii, mambo yako baridi sana. Unaweza uliza hata watanzania kumi kati yao asitokee hata mmoja anaejua hali ya vuguvugu la kisiasa nchini.

Zaidi sana mwamko mkubwa wa kisiasa umeibukia kwenye dpw vinginevyo hali kisiasa ingepooza zaidi.
Wazee wa Mafuriko ya watu kwenye mikutano watakushukia kama mwewe 🤣🤣
 
Oparesheni zilizofanywa na wapinzani zilikuwa na mguso na mvuto mkubwa sana Kwa wananchi, hali ni tofauti sana awamu hii, mambo yako baridi sana. Unaweza uliza hata watanzania kumi kati yao asitokee hata mmoja anaejua hali ya vuguvugu la kisiasa nchini.
Unaandika haya ukiwa wapi? Nimezunguka mikoani ifuatayo ndani ya miezi miwili na nimeshuhudia mabadiliko makubwa sana, nimefika Njombe, MBEYA, Kigoma, Shinyanga(Kahama) na ARUSHA. Nimeshuhudia Kwa macho sio Hadith za kukaa nyuma ya keyboard na kuandika, njoo field
 
Mimi sio mwanaccm ila ni mtanzania wa kawaida lakini ukizungumzia hali yangu ikoje! Unataka nijilinganiahe na nani?
Na huyu anayetaka nimchague ameonyesha mfano gani kuwa ana kitu cha tofauti?
Ni nchi gani ilipiga hatua kubwa Kwa kigezo Cha kuondoa chama tawala, au ni kupokezana tu ulaji?
In brief hupendi mabadiliko yoyote.
 
Back
Top Bottom