Nataka kuachana na mke tuliyezaa naye watoto watatu. Amenishinda tabia!

Nataka kuachana na mke tuliyezaa naye watoto watatu. Amenishinda tabia!

Mkuu tunaishi kwa malengo mfn kujenga na kuboresha nyumba, kununua asset na kula vizuri pamoja na mipango mingi. Kama ni hela anapeleka wapi na vyote anapata?
Mifumo yenu dume hiyo ndomana wanawakimbia ,anandugu kama ulivo wewe pia bank.anatamani awe na akaunt yake ,jiulize ukifa wewe familia ataendesha nani
 
Ndio maana huwa tunaambiwa tuangalie sana nasabu ya mwanandoa lengo ni kujua tabia za familia yao

Ukiona familia inamtetea mwanandoa bila sababu za msingi ujue hapo kuna tatizo,familia makini haiwezi kulea huo ujinga

Marehemu mkwe wangu alikuwa hataki ujinga kabisa,,binti akienda kwake bila taarifa maalum ujue lazima atarudishwa

Nilipo mwacha mke wangu pamoja na kutoa talaka kwa maandishi lkn bado alinipigia na kuniuliza baba "umetoa talaka kwa hiari yako mwenyewe" nikamjibu ndiyo ndio akaridhika

Lakini hawa wazazi wanao sema kwani mwanangu kwenu umeua mpaka uogope kurudi hawa wabaya sana
 
Mifumo yenu dume hiyo ndomana wanawakimbia ,anandugu kama ulivo wewe pia bank.anatamani awe na akaunt yake ,jiulize ukifa wewe familia ataendesha nani
Suala la kufa ni mtu yeyote anatangulia jamii nyingi sasa wanaaminishana mme huanza kufa ndio maana baadhi ya wanawake huwanyamazisha waume zao milele
 
Wana jamvi,

Kama bado hujawahi kukutana na changamoto ya familia unaweza kudhani watu humu wanaleta stori za kusadikika!

Mimi na mke wangu tumeishi naye kwa miaka nane sasa na kwa kipindi hicho chote nimejitahidi kuwa mwaminifu na kuhudumia familia vizuri.

Sasa vituko vya huyu mwanamke anagawa vitu vya ndani kama mafuta, mchele, maharage na hata mkaa. Vitu vinaisha kabla ya muda hata sehemu ninapofanya manunuzi huwa wanashangaa, husema huenda nina nyumba ndogo ila mimi ni mwaminifu kwa huyu mwanamke.

Kituko kikubwa alichokifanya ni kutoroka nyumbani akiwaacha watoto hivi sasa kamaliza miezi yapata mitatu taratibu mawazo ya kuoa mwanamke mwingine yanakuja ili kusaidiana maisha. Isitoshe mwanamke huyo hana elimu kubwa na hana ajira japo mimi ni payee sijawahi kumdharau kwa hali yake zaidi ya kumrekebisha pale anapokesea.

Sasa nimeona hali imekuwa climax na ninataka kuachana nae na watoto nitalea mwenyewe. Ushauri wenu wakuu 🤔
Umesema kwa upande wako, yeye naye anazo sababu za msingi kutoroka.
Sikubaliani na suala la mwanamke kugawa kwa ndg au majirani mahitaji ya ndani kwa kuzingatia yamenunuliwa kwa fedha
Nilishawahi kukutana na kadhia hii, makusudi ya yule wa kwangu alikuwa anataka niwe nampa pesa mwenyewe ili ajibalance (nadhan na kufanya mambo yake nje na mahitaji hayo)
Wanawake wa namna hiyo, wa kwako na wa kwangu ni ngumu kuisho nao. Ni wajinga sana, ni wapuuzi mno, hudhamilia kumkomesha mwanamme, mi tuliachana tu na kuwa kama mwizi vili.

Mwanamke anabeba gunia la mkaa na kumpa jirani, aisee sikuwwza hayo maisha hata kidogo
 
Mkuu tunaishi kwa malengo mfn kujenga na kuboresha nyumba, kununua asset na kula vizuri pamoja na mipango mingi. Kama ni hela anapeleka wapi na vyote anapata?
Pesa ndogo ndogo labda za kujihudumia yeye nguo zake mambo yao ya mwezi n.k..

Na kwanini aende kwao bila kukutaarifu hao wazazi wake mbona hawamwambii arudi. Au wamepanga huo mpango? Haiwezekani mke wa mtu aende kwa wazazi miezi 3 na mzazi wake akae kimya tu

Au ni mpango wa wao uoe mke mwingine waje wachukue mali.. hakikisha kabla haujafanya maamuzi hakikisha assets zako zina majina yako yote..
 
Ndio maana huwa tunaambiwa tuangalie sana nasabu ya mwanandoa lengo ni kujua tabia za familia yao

Ukiona familia inamtetea mwanandoa bila sababu za msingi ujue hapo kuna tatizo,familia makini haiwezi kulea huo ujinga

Marehemu mkwe wangu alikuwa hataki ujinga kabisa,,binti akienda kwake bila taarifa maalum ujue lazima atarudishwa

Nilipo mwacha mke wangu pamoja na kutoa talaka kwa maandishi lkn bado alinipigia na kuniuliza baba "umetoa talaka kwa hiari yako mwenyewe" nikamjibu ndiyo ndio akaridhika

Lakini hawa wazazi wanao sema kwani mwanangu kwenu umeua mpaka uogope kurudi hawa wabaya sana
Naunga mkono hoja. Hasa baba yake nimegundua sio mtu mzuri, huenda anataka tuachane amsaidie mwanae kugawana mali. Bush lawyer wanachekesha sana
 
Ukioa mwanamke halafu kwao kuna wanao muunga mkono umekwisha,hizi ni zile familia ambazo kila kukicha,kila mnalofanya anatoa taarifa kwao,na ndio maana alipoamua kurudi kwao wamempokea....
 
Sijaona mahala kanyimwa kufungua bank akaunt.
angefungua na nini hana biashara hana zaidi ,ya aamke asbuhi afagie nyumba ,aioshe mumewe asije rudi dharula ili akitaka kukanda amkande ,Dunia imegeuka tujiongeze wanaume muda mwingine turuhusu hawawatu wafanye biashara tusiwaze sana juu ya kugongewa
 
Ukioa mwanamke halafu kwao kuna wanao muunga mkono umekwisha,hizi ni zile familia ambazo kila kukicha,kila mnalofanya anatoa taarifa kwao,na ndio maana unao alipoamua kurudi kwao wamempokea....
Hata mimi naona ni hivyo.. maana sio kirahisi hivi miezi 3 nje na mbali na familia halafu wazazi wasikuhoji ahahah wanasubiri aingie kwenye mfumo wamkomoe...
 
angefungua na nini hana biashara hana zaidi ,ya aamke asbuhi afagie nyumba ,aioshe mumewe asije rudi dharula ili akitaka kukanda amkande ,Dunia imegeuka tujiongeze wanaume muda mwingine turuhusu hawawatu wafanye biashara tusiwaze sana juu ya kugongewa
Kuna aina ya wanawake hata biashara hawawezi. Sasa kama anauza vitu vya ndani ataweza fanya biashara anunue hata unga wa ngano?
 
Back
Top Bottom