Nataka kuachana na mke tuliyezaa naye watoto watatu. Amenishinda tabia!

Bembeleza Mke wako murudiane.

Sijaona hata semehemu mlipokosana. Ila mmechokana, ndio maana akaenda kupumzika.

Acha kutafuta matatizo kwenye maisha. Ukitaka hao watoto waishi kwa shida, oa mke mwingine.

Pili, badilisha life style. Mpe kazi ya kufanya, mdungulie genge ili awe busy kidogo.

Pole, ila humu utaambulia hasira za watu.
 
Alienda kwao mkuu. Wakwao wanaingilia familia yangu na ninahisi walimwambia aende. Kuhusu kumpiga muda huu kaondoka bila kumpiga
Kama mkeo aliondoka bila ruhusa yako ina maana kuna mtu/watu wengine anawasikiliza zaidi kuliko wewe,wakati wewe ndio final say kwako,

So,miezi yote hiyo anafanya nini huko? Kwanini harudi kwa watoto wake? Ukipata majibu ya kuridhisha piga chini ila nawahurumia sana hao watoto,

Usije ukashangaa baada ya watoto kukua wakaja kuambiwa ulimfukuza Mama yao,weka kumbukumbu ya kila aina ya ushahidi itakusaidia kuwajulisha wanao huko mbeleni nini hasa kilitokea mpaka Mama yao kuondoka,

Pole sana bro.
 
Yupo kwao mkuu huwa naongea nae ila simuulizi habari ya kurudi kupitia simu ya mama yake
Unakosea sana kuongea nae,ungepiga kimya au ukabadili kabisa namba yako,yeye mwenyewe angekutafuta,

Kitendo cha kuwasiliana nae ni kama umeridhika yeye kua huko,

Piga kimya endelea na maisha yako wala usimuulizie wala asijue habari zako wala habari za watoto,

Mkeo alishakuona kua wewe ni dhaifu sana kwake ndio maana anakuchezea,

Kaza mkuu,kua na roho ngumu na yakikatili,huyo atarudi mwenyewe kisha unamfukuza arudi alipotoka.
 
Kama ni mtu anayegawa vitu kwa friends maana yake ni mtu wa jamii, na hapo yamkini kuna jamii ya wanawake wenzie wamemharibu kwa ushauri mbaya.

Pengine kuna namna anaona humtendi ipasavyo kama wenzie wanavyomtendea, sasa huyo mkuu kumuweka sawa ni ngumu sana, ni ngumu mno mwanamke kubadilika na kwa sehemu fulani lazima atakuwa na mahusiano ya nje, najua utaumia kusikia hivi ila huu mkuu ndo ukweli, kuna mahusiano ambayo anayo.

Mara nyingi wanawake wa hivi wanakuja kujutia makosa yao after years, sasa hivi cha kufanya kaa nae mbali, kata mawasiliano nae kupitia ndugu zake au yeye mwenyewe. Angalia namna nzuri ya kulea watoto, sehemu ambayo utapata urahisi wa kuwaona na kupata ulinzi, chakula na elimu.

Tafuta mwanamke mwingine, mueleze ukweli wa yalotokea ndani ya ndoa yako, ukimuona ana uelekeo na amekuelewa jitulize hapo ila jibane sana mkeo asijue, akijua atapata sababu.

Pole sana.
 
Wazee mnatutishaa sana vijana ambao bado hatujafika stage hiyo ya kuoa kila kukicha mtafaruku kweny secta ya ndoa🙌
Ukiweza kuwa kama mtume Paulo, alisema ukiona huwezi kuoa acha, huo unaoita mtafaruku ipo kila eneo la maisha mzee, kazini utaikuta, nyumbani ndio kama hivi, kwenye familia yenu hukosi mtafaruku kifupi ni kupambana.. La ukiona ya shingo ruksa kubadilisha gear na sio kukwepa pambano, grow up.
 
Kwanza hama huko uswahilini maana nyumba ambazo zimepangwa vizuri na kuna geti ni ngumu mambo yakuombana chumvi sijui mkaa. Alafu kama kaondoka miezi mi3 huyu umemuoa kwa ndoa au ikoje hii? Na nyie ni dini gani?
 
... unapotaka kukosea ni kufanya 'replacement' huku bado una MAKASIRIKO!
CHONDE CHONDE USIJEANGUKIA PABAYA ZAIDI!
😅
 
Lakin hajasema kama alimkataza kufanya biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…