Jaribu kuchunguza,kiburi cha huyo binti kinasababishwa na nini? Kingine hii kesi tumeisikia upande mmoja tu,pengine huyo binti nae anayo ya kusimulia kuhusu wewe,
Miaka 20 ni binti mdogo,hajajua bado ndoa ni nini,jaribu kutumia wazee ili wamuweke sawa au aeleze tatizo lake ni nini au anataka nini?
Maisha ya ndoa sio rahisi kama unavyofikiria,maisha ya ndoa ni mtihani mgumu sana,utaacha wangapi na kuoa wangapi?
Kitendo cha huyo Baba kutokutaka kupokea mahari kinasababishwa na ugomvi na chuki aliyojijengea dhidi ya huyo mkewe aliyeachana nae,mzee anaonekana ana nongwa sana na amejenga kama uadui na mtalaka wake na akawaingiza na wanae pia kwenye hiyo chuki,
Usikurupuke kuchukua maamuzi,jaribu kwanza kutafuta solution,maisha ya ndoa yana mengi sana,wengi wapo kwenye ndoa zao coz ya uvumulivu tu.