Nataka kuachana na Mwanamke niliyemtolea mahari

Nakubaliana na yote uliosema ila kipengele cha umri wa miaka 20 kuwa ni mdogo hilo nakataa.
 
Mkuu zungumza na mama yake mzazi mwambie amuache mtoto wake aishi maisha yake ya ndoa aache kbs kumchunguzachunguza na kumshauri, awambie ndugu zake waache kumfuatilia mkeo ili aishi maisha yake bila majungu ya kijijini.
Mwambie mkeo haya ni maisha kati yako wewe na yeye asiyasimulie kwa mtu yoyote wala kutaka ushauri kwa mtu yoyote kwa mambo madogomadogo ya ndani ya nyumba, mweleweshe kuachana kwenu ndani ya kipindi kifupi kutamchafulia jina yeye zaidi kuliko wewe na anaweza asiolewe tena.
Mzee wake kukataa mahari pengine alikuwa anamjua bint yake kitabia au wazazi wengine hukataa mahari ili usiende kumnyanyasa mtoto wao kwa ng'ombe wa laki tatu kwa jina la mahari.
Wakati mwingine usiharakie jambo kwa kasi hiyo, ulitakiwa kuwapa muda ndugu zako wakutafutie mke walau kwa uchache mwaka mmoja hata vijiji vya jirani, hata gari huwezi nunua kwa haraka namna hiyo lazima upate washauri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…