Nataka kuachana na mwanamke

Sikiliza ndugu maisha hayapo programmed kwamba kipato chako kitakua constant kadri upendavyo, kuna kutetereka na mengine mengi, tunazungumzia uhalisia hapa sio nadharia.
 
Ni wazo pia ila nadhani hiyo 2500000 ya enzi hizo ya babaako ilikuwa na thamani mara 2 ya 900000 ya sasa, hebu twende pamoja
Hiyo 250000 iliendana na maisha ya wakati ule, na hata hiyo 900,000 ya sasa inaendana na Hali ya sasa. Kwa hiyo hakuna utofauti. Aliekupa huo mfano yupo sahihi kabisa.
 
Ja
Sana tu yaani vitu vya nyumbani kama vyakula vinakomba pesa yote.

Anabaki kusubiria mwisho wa mwezi tena,😳 huu si ni utumwa?
Jamaa Hana akili....jogoo hafi kwa utitiri
Moja ya vitu alitakiwa kujipanga before kuoa ni pamoja na:
Uchumi na kipato cha Familia
Imani
Elimu ya watoto
Akiba
N.k
Then hakikisha mwenzi wako naye Ana kipato na muwe na bajeti
 
Nilimshauri awali hakuamini eti laki tisa ni kubwa aiseee 😅😅😅😅...ngoja ncheke kama mazuri.. hebu mnisaidie nimshauri vipi? 😳😳
Msidhani humu wote ni watoto, kama ni mtu wa starehe hata m5 utasema hazitoshi lakini kwa familia yako ni pesa nyingi sana kama si mutu wa starehe kubwa.
 
Duh any way
Tatizo linaweza kuwa kwake mwenyewe wakati anaoa aliwai kushirikisha mke wake juu ya hizo biashara?

Kama Duka na vitu vinakwama amuulize huyo mke wake kama anapenda hiyo biashara SASA kama mke wako maono yake yalikuwa ni kuwa na saloon unampatia Duka ndugu Yangu unatafuta lawama

Kaa chini na mke wako muyajenge mjue wapi mlikosea pia mueleze ukweli juu ya changamoto unazokutana nazo lakini mwambie anataka kufanya shughuli gani ? Pia angalia na uwezo wake pia sio kila MTU anaweza kufanya biashara hapo ndipo tunakosea sio kile unachopenda ni lazima mwenzako akipende

Mwisho mwanaume hautakiwi kukimbia majukumu na wala kufikiria kurudi ujana miaka inakwenda kubaliana na changamoto na songa mbele

Wanasema kipimo cha ubaba sio kukimbia majukumu ni namna ya kukutana na changamoto na kukabiliana nazo , jifunze Kwa waliofanikiwa Ila usirejee nyuma tunaelekea kanaani misri Kwa nini ?
 
mke ndiye mpanga bajeti...
Wewe ukipata mshahara nunua mahitaji muhimu mke hawezi kukataa kuyapokea, akisema hapokei eti hakushirikishwa ujue ana mambo yake. Vitu muhimu vikiwepo vinavyofuatia ni leo mboga gani ambazo hazizidi elfu tano, achana na mtindo wa kinunua roborobo mpaka mwenye duka anakuwa kama mjomba wako, kila siku mnaonana mara tatu, asubuhi sukari robo, mchana unga robo na jioni unga tena robo!
Ukweli ukila kwa mamantilie acha hoteli ni aghari zaidi mara nne. Hivi ni watanzania wangapi wenye familia wanapata 900,000/= kwa mwezi, au hapo anapofanya kazi wote wanapata hizo, tuache kujikuza.
 
narudia tena, achana na nadharia za tamthilia, zinakuharibu
Wewe hutaki kuniamini ila nachokuambia ni kweli,mimi mke wangu kila nikihamka asubuhi ananihamkia shikamoo baba.
Akikosea kitu ananiomba msamaha akiwa amepiga magoti.
Nadhani wako anakusimamia kope juju juu na kutaka kupgana nawe au sio
 
Wewe hutaki kuniamini ila nachokuambia ni kweli,mimi mke wangu kila nikihamka asubuhi ananihamkia shikamoo baba.
Akikosea kitu ananiomba msamaha akiwa amepiga magoti.
Nadhani wako anakusimamia kope juju juu na kutaka kupgana nawe au sio
Duuuuh, kumbe kuna watu mna bahati hivyo? 😳😳😳
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…