Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Hujajua pa kwenda alafu unataka kuachana na ulichonacho ?

Usiache Mbachao kwa Msala Upitao...., Ndege mmoja Mkononi ni Bora kuliko Kumi Mtini....
 
Watu wanadhani kuwa ukisomea ualimu basi ni lazima ukafundishe shule ya msingi na sekondari.

Kada ya education ni Pana na taasisi nyingi ndani yake unaweza kufanya kazi kwenye taasisi nyingine za elimu zenye mshahara na posho za Kila wakati.

Kupanga ni kuchagua.
 
Asante kaka nitafuata ushauli huu maana katika ualimu nahis kukosa amani kabisa ata furaha ya kazi sina
 
Nikweli bro lakin jinsi ya kuingia sasa hko kwenye hizo taasisi ndo kwenyewe
 
Mkuu vipi hukupata tena ajira ya ualimu [emoji22]. Kama ulipata hongera ila kama hukupata pole sana najiskia maumivu makali kuliko anaechomwa na moto wa petrol. Umefight sana kiongozi wangu Mungu yupo
Mpwayungu malizia ile stor basi...
Yaani huwa naiwaza iliishiaje
Hahahaha na viatu vyako vilivyolowa vumbi kule shule ya lindi
 
Why usisome degree ya bios na chem uliyokuwa na diploma level itakuwa rahisi kuwa upgraded na ukalipwa vizuri zaidi kuliko kuhama course yako ambapo utaanza kutafuta ajira upyaa..!! KUANZA UPYA NI NGUMU SANA AISEEE USIJIDANGANYE hata uko AFYA NGOMA NGUMU
 
Kuna taasisi nyingi sana elimu zinatangaza nafasi nza kuhamia huko Kila mwaka

Jamaa atafute bachelor na master na ahamie huko kwingine
 
 
Mku hapo kwenye kuomba kazi upya kupitia ajira.go.tz siku hizi ni impossible kwa entry position
 
Walimu wa sekondari Ni magwiji wa unafiki na majungu Sana ,,,digrii mmepata lkn akili hamna.
Mimi nimefanya kazi na walimu wa primary na secondary nawajua vzuri... Walimu wa primary wanaamin ualimu ndio maisha yao na chuoni wamejifunza ethics za ualimu na utumish wa umma, kwahio wanapoingia kazini hufanyakaz kwa bidii na kufanya maendeleo kama kujenga nyumba na kufungua miradi mbalimbali.... Shida ya walimu wa Secondary wanajiona wamesoma wana degree na wanaamini wao sio walimu bali wanapita tu kwenda ktk kazi/kada nyingine 😅 kwahio miaka inazidi kwenda wanajikuta hawatoki ktk ualimu na hawana nyumba au miradi, wengi wanaanza kushituka baada ya miaka 10 kupita ndio wanaanza kukubali kwamba wao ni walimu. But sikuhiz wameamka wakiingia kazin wanachangamkia fursa wanajenga na kufanya miradi... All in all kwa Tanzania watumish wenye maendeleo walimu wanaongoza, mwalimu lazima umkute amejenga nyumba na ana mradi unamuingizia pesa, japo ndio kazi inayo dharaulika sana ila ukweli ina mishahara mikubwa...
 
Bachelor of science in biology unarudi kuwa mwl . Kasome Bsc Aquaculture au Bsc fisheries Sua au udsm utakuja kunishukuru . Maafisa uvuvi ni wachache Sana. Tafuta wilaya yenye ziwa au baharu ufanyiwe recategirization utakuja kunishukuru. Au nenda kasome masuala ya Procurement and supplies. Watu wa procurement ni wachache walioajiriwa ufanyiwe recategirization uwe procurement officer pia utakuja kunishukuru. Kumbuka unavyoenda kusoma uwe na tricky Kuomba vyuo viwili unapeleka joining instructions ya kwamba unaenda kusoma education. Wewe unaenda kusoma chio kingine ili upewe ruhusa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…