Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Kasome BSc Accounting or Finace then ukiwa college anza kufanya mitihani ya CPA, ukimaliza au kabla hujamaliza anzisha kampuni yako ya accounting & Tax services then work very hard na uwe mwaminifu
Akisoma CPA akiwa chuo itamlazimu kuanzia ATEC I mpaka aje kumaliza inawezekana na chuo chenyewe kikawa kimeisha na Bado asiipate hiyo CPA kwa sababu Hana msingi kwenye Uhasibu.

Bado hujamshauri
 
Bro alaf waalimu wa msingi nimefuatilia nimegundua Wana maisha mazuri kuliko sisi wa secondary, sijui mchawi wetu nani
Mchawi wenu ni kudharau kazi ndogo ndogo. Wale wanauza ubuyu shuleni na kufanya vishughuli vya hapa na pale ambavyo vinawaingizia kipato cha ziada. Nyie mnajiona wasomi siyo...hahahaaaaa
 
Late 2009 kuna Mwl mmoja alifanya uamuzi kama huu unaoutaka wewe, yeye alisoma kozi fupi ya Ualimu wa Sekondari mwaka 2006 kipindi Shule za kata zimeanzishwa. Sasa alimua kwenda kusoma Degree ila aliamua kubadili kozi ya kwenda kusoma chuo, alichagua Accountancy na alifanikiwa kudahiliwa UDOM.

Wakati anaomba ruhusa kwa mwajiri wake(DED) alidanganya kuwa anaenda kusoma Ualimu akapewa ruhusa.

Baada ya kumaliza Chuo akiwa na Degree ya Accountancy akashindwa kurejea kwa mwajiri ili aendelee na kazi maana alidanganya tangu mwanzo. Akaamua kuingia mtaani ili atafute kazi. Aisee mambo yakawa magumu sana akafanya Application nyingi za kazi bila kuitwa hata Interview moja, stress si ikapiga hodi akakondeana hatari maana mwanzoni alikuwa bonge. Wenzio ambao hawakudanganya wakarejea kazini(Ualimu) bila usumbufu wowote tena wengine waliopata GPA kubwa walipangiwa Vyuo vya Ualimu kwenda kufundisha, yeye akaanza kujutia uamuzi wake.

Sasa hivi sijui yuko wapi maana mara ya mwisho nilikutana naye mwaka 2015.

Kwa hiyo binafsi nashauri kama hauna chanzo kingine cha ugali, usiache ualimu ukakimbilia kusoma kozi nyingine tofauti na hiyo Ualimu, imagine walimu wamejaa mtaani wenye degree na wanatamani wakafundishe hata Primary angalau wapate hela ya kusogeza siku
Bonge la ushauri, mm pia mwalimu mwenzako ila mm nafundisha chuo. Nlipanga kufanya kazi 5yrs tu niache ila sasa nina 15yrs, acha kazi uone ilibo ngumu kupata kazi. Saiz ajira zinatangazwa 10 wanaomba 10000. Jiulize why?
Kama unataka kuacha kazi basi weka vyeti kabatini, weka status kabatini ingia mtaani fanya yako. Baada ya miaka michache hutojutia maamuzi yako.
Unavyotaka kufsnya nisawa na kuoga kwenye mvua badala ya kuoga kwenye bomba la mvua.
 
Why usisome degree ya bios na chem uliyokuwa na diploma level itakuwa rahisi kuwa upgraded na ukalipwa vizuri zaidi kuliko kuhama course yako ambapo utaanza kutafuta ajira upyaa..!! KUANZA UPYA NI NGUMU SANA AISEEE USIJIDANGANYE hata uko AFYA NGOMA NGUMU
Ahsante ndugu ntazingatia
 
Mimi nimefanya kazi na walimu wa primary na secondary nawajua vzuri... Walimu wa primary wanaamin ualimu ndio maisha yao na chuoni wamejifunza ethics za ualimu na utumish wa umma, kwahio wanapoingia kazini hufanyakaz kwa bidii na kufanya maendeleo kama kujenga nyumba na kufungua miradi mbalimbali.... Shida ya walimu wa Secondary wanajiona wamesoma wana degree na wanaamini wao sio walimu bali wanapita tu kwenda ktk kazi/kada nyingine [emoji28] kwahio miaka inazidi kwenda wanajikuta hawatoki ktk ualimu na hawana nyumba au miradi, wengi wanaanza kushituka baada ya miaka 10 kupita ndio wanaanza kukubali kwamba wao ni walimu. But sikuhiz wameamka wakiingia kazin wanachangamkia fursa wanajenga na kufanya miradi... All in all kwa Tanzania watumish wenye maendeleo walimu wanaongoza, mwalimu lazima umkute amejenga nyumba na ana mradi unamuingizia pesa, japo ndio kazi inayo dharaulika sana ila ukweli ina mishahara mikubwa...
Mishahara mikubwa?? Umeamua kutoa Siri ya waalimu walio apa kufa wakiwa wameificha....kila siku Wanalia kuudhihirishia una kua hawalipwi kumbe wanakunja fedha nzuri tu
 
Bachelor of science in biology unarudi kuwa mwl . Kasome Bsc Aquaculture au Bsc fisheries Sua au udsm utakuja kunishukuru . Maafisa uvuvi ni wachache Sana. Tafuta wilaya yenye ziwa au baharu ufanyiwe recategirization utakuja kunishukuru. Au nenda kasome masuala ya Procurement and supplies. Watu wa procurement ni wachache walioajiriwa ufanyiwe recategirization uwe procurement officer pia utakuja kunishukuru. Kumbuka unavyoenda kusoma uwe na tricky Kuomba vyuo viwili unapeleka joining instructions ya kwamba unaenda kusoma education. Wewe unaenda kusoma chio kingine ili upewe ruhusa
Ahsante kaka haya ndo mawazo nnayo tafta, na Vipi nkirudi mwajiri akaniomba hyo bacherol ya ualimu ntajibu Nini?
 
Yani kama kwenye ualimu umeshaajiriwa ni bora upambane hukohuko huku ukianzisha miradi ya kukuingizia pesa na hiyo pesa ya kwenda kulipia chuoni. Maana utamaliza utateseka kwenye kutafuta ajira, na hata ukipata mambo yatakua vilevile tu.
Asee
 
acha dhihaka njoo field hapa Posta, njoo IFM ma-bos wa BOT wana

njoo field uncle , mjini mipango wenzio mtaji ni kitambaa , sponji na sabuni FOMA, jioni anafunga 50,000/-
wewe endelea na white collar job.
Kumbuka reliability ya chanzo cha kipato chako, je siku ukiumwa walau mwez mmoja utaendelea kukunja hiyo 50 kwa siku?
Hakikisha kazi unayofanya inakuungizia kipato wakat ukiwepo ww mwenyewe au usipokuwepo bado mzunguko utaendelea. Tofaut na hapo na hatari sana
 
Nyie motivation speakers huwa mnaongea tu.nani akupe elfu 5 kwa siku kwa kuosha magari tu?kwanza hayo magari 10 unayosema ya kuosha unayapata wapi kila siku?
Labda atayafuata magari barabarani umesahau kale kamchezo kwenye foleni magari yakisimama kwa red light Jamaa anakuja na kibrash na kisado cha maji anaanza kusafisha kioo cha mbele akimaliza anakuja kukinga mkono dirishani alipwe
 
Back
Top Bottom