Nataka kuachana na unywaji wa pombe, lakini sijui naanzia wapi

Nataka kuachana na unywaji wa pombe, lakini sijui naanzia wapi

Hello JF

Kama kuna mtu anaweza kunisaidia abc za namna ya kuacha unywaji wa pombe anisaidie tafadhali maana kila nikijaribu nakaa siku mbili narudia...
Kwa kila glasi tano za maji moja iwe ya maziwa fresh. Hakikisha kila wakati umekunywa maji na maziwa hayo ambayo ni kama glasi 2-3 kwa siku. Fanya kwa siku 30 halafu uniambie nikupe nini kingine cha kufanya.
 
Dunia hata sio mbaya walimwengu ndo wabaya .ipo dawa ya kienyeji unakunywa siku 3 maji ya mizizi siku ya nne anakuaruhusu kalewe yaan pombe zinakuwa na radha ya mikojo ya choo cha stendi .ila wanaojua wanataka hadi hela wako tayari jamii ife sio wakose hela
 
Kila kitu ni maamuzi tu. Amua mwenyewe sasa kuacha hiyo pombe! Na utaacha mara moja. Maana hakuna atakaye kunywesha kwa nguvu.
Mkuu Tate maamuzi unakuwa umeshachukua wakati mwingine unamaliza hata miezi mitatu ujagusa lakini sijui shetani gani anakupitia unajikuta unakunywa tena
Sasa mpaka unashindwa kuelewa ni kuendekeza moyo,nuksi,mikosi au ni nini hasa maana kitu ukipendi unakichukia lakini unajikuta kinakuzidi nguvu unakitumia
 
Dunia hata sio mbaya walimwengu ndo wabaya .ipo dawa ya kienyeji unakunywa siku 3 maji ya mizizi siku ya nne anakuaruhusu kalewe yaan pombe zinakuwa na radha ya mikojo ya choo cha stendi .ila wanaojua wanataka hadi hela wako tayari jamii ife sio wakose hela
Mkuu tufahamishane hiyo dawa maana mimi katika starehe nisiyoipenda ni pombe lakini nitakaa wiki,wiki mbili au mwezi inatokea siku nakunywa najilani kweli kweli kuwa sitoludia lakini wapi mpaka nikafikia kujisemea moyoni au hii kwangu ni dhambi ya kurithi?
 
Pombe ni kitu cha kipumbavu sana...ninasema hivyo kutokana na experience yangu ya kunywa Pombe za aina mbali mbali for fucken 30 years.....niliamua kuacha bila kushauriwa baada ya kuzidiwa na pombe nikiwa kitandani na kuzima hivyo kukimbizwa hospitali...
Nilipata aibu sana..I will never forget mpaka naingia kaburini..
Mungu nisaidie..
 
Nyie ndio wale mnakunywa pombe kama mnakimbizwa. Pombe inatakiwa unakunywa taratibu-aste aste
 
Mkuu tufahamishane hiyo dawa maana mimi katika starehe nisiyoipenda ni pombe lakini nitakaa wiki,wiki mbili au mwezi inatokea siku nakunywa najilani kweli kweli kuwa sitoludia lakini wapi mpaka nikafikia kujisemea moyoni au hii kwangu ni dhambi ya kurithi?
Haina urith ni upuuz ni addiction tu ukinywa pombe inatoa hormone inaitwa dopamine inakupa furaha .Sasa ukiacha Pata furaha kwenye familia .watoto.umoja na waumini wa dini yako.mapenzi unajikuta pombe ni suluhisho zuri.
Ndo maana walevi wengi pia hawana ndoa nzuri.wanahistoria mbovu utoton . Wametokea kwenye umaskini.watoto wa kambo etc
 
Ingependeza ukaweka full detail ya matumiz yako ya pombe mfano pombe gani unatumia, kwa siku unakunywa kiasi gani, mahali, unapendelea kunywa peke yako au na marafiki ukifunguka zaidi naamin watu watapata pa kuanzia na utaweza kushauriwa na kusaidiwa
Nakunywa hizi za kawaida tu mfano konyagi na bia.huwa sometimes nakunywa na washkaji au mwenyewe
 
Back
Top Bottom