Nataka kuachana na unywaji wa pombe, lakini sijui naanzia wapi

Nataka kuachana na unywaji wa pombe, lakini sijui naanzia wapi

Kwanza kabisa kabla hujajaribu kuacha andaa kundi jingine la kijamii ambalo mazungumzo yake na yako Kwa kiwango fulani yawe yanafanana ili kuwa mbadala wa kikundi cha wanywaji wenzio wa sasa.

Baada ya kulichagua kundi litakalokuwa kampani yako mpya,anza kidogo kidogo kubadili ratiba zako za out ukifuata ratiba za kundi lako unalotaka kuhamia.

Punguza unywaji na muda wa kujumuika na kundi lako la sasa na muda mwingi uegemeze kwenye kundi lako jipya.

Baada ya muda kundi lako la sasa litakuona umejitenga nalo na utapoteza mvuto kwao hawatakuita tena kushiriki meza. Hii itakuwa imekusaidia wewe kujiona hutakiwi kwenye kundi lako la sasa na wakati huohuo sayansi ya kundi lako jipya itakuona kama bado hauja qualify sawasawa kwenye kundi lao. [Hapa ndipo unapopatafuta].

Binadamu tumeumbwa kufaulu, hivyo na wewe ni binadamu kama wengine,lazima utajitahidi kuji tune ili ku qualify ama kuthibitisha walikuwa(kundi lako jipya) wanakuchukulia sivyo.

Unaweza ukajaribu.




MAGUFULI4LIFE.
 
Huenda unapoomba ushauri huu uko baa tayari au una chupa mkononi.!

Huwezi kuacha Pombe kwa kushauriwa. Unaweza kuacha Pombe kwa kuamua baada ya kijihoji mwenyewe kuhusu hasara unazopitia. Kwa Mimi nafikiri kule tu kukiri kwamba umeona Pombe inakurudisha nyuma ni mwanzo mzuri, anzia hapo Sasa kufanya maamuzi. Wiki 1 au 2 za mwanzo utapata shida Kidogo ila baada ya hapo uta move on.
 
Hello JF

Kama kuna mtu anaweza kunisaidia abc za namna ya kuacha unywaji wa pombe anisaidie tafadhali maana kila nikijaribu nakaa siku mbili narudia...
Usiache pombe mkuu.

Pombe ndo kila kitu kwa nchi km zetu hizi.

Yani ukiacha tu pombe utatusababishia kero nyingi sana km taifa kwa maana kodi ya nchi itapungua>>tutakosa hela zetu wenyewe>>tutakosa madarasa >>wanafunzi watakaa chini>>elimu duni>>umaskini wa kutupwa>>ujambazi/udangaji>>kukopa kwa mabeberu>>madeni kwa taifa>>masharti ya ajabuajabu km kukubali ugasho n.k

Yani kwa kifupi utakuwa umeuza nchi mkuu
 
Ni maamuzi yako tu haihitaji dawa wala ushauri wa mtu
Hata hiyo siku utakayoacha huwezi kuamini maana utakuwa unasema niliamka tu siku moja nikasema kuanzia leo basi sirudii tena

Hakuna anaejali afya yako na pesa zako zaidi yako mwenyewe
Kuacha ni maamuzi yako mwenyewe
Jaribu kupiga hesabu unatumia shillings ngapi kwa mwezi kwa ulevi na hata sigara kama unavuta
Halafu jipige Kofi Sema hivi wewe mpumbavu kiasi gani unatumia hela kwa hasara?
Sasa acha halafu hizo hela za pombe weka kama akiba au mtumie mama yako
Maamuzi ni yako
Kama unasema ukitaka kuacha unajikuta unakunywa tena hapo ujue haipo tayari kuiacha na bado unaipenda
 
Pombe ni moja kati ya vitu vinavyozidi kunirudisha nyuma.

Ukipata mbinu usisite kunishtua mkuu
Katika vitu ambavyo binadamu unatakiwa uwe na uwezo wa kuvi control ni pamoja na pombe na sigara, haitakiwi kabisa pombe au sigara ndiyo iwe inaku control, no ni wewe uwe na maamuzi kwamba wiki hii pombe sinywi au sasa sigara naacha... Ukikuta huwezi kuvi control basi jua huwezi kufanya very difficult decisions in life.
 
Kila kitu ni maamuzi tu. Amua mwenyewe sasa kuacha hiyo pombe! Na utaacha mara moja. Maana hakuna atakaye kunywesha kwa nguvu.
Exactly [emoji1666] [emoji1666] mimi nilikuwa mvutaji sigara sanaa but kuna siku baada ya kumuona jirani yangu anavyoteseka na kansa ya mapafu wodini, nikasema enough is enough, nilikuwa na paketi ya SM na kibiriti cha gesi mfukoni, nikasema hii ndiyo itakuwa my last packet of cigarette. Na kweli nikaacha kuvuta sigara mpaka leo, ni maamuzi tuu.
 
Mimi nlikuwa chatungi sio kidogo na nakumbuka nlianzaga tungi fom 4 Iyunga mbeya,na kama unavyojua mbeya ndio kituo Cha vikali,vitokavyo Zambia wakati huo viroba og ndio vinatoka.
Sasa nikisema nimeacha tungi na fegi hakuna anaye amini,bt ni kweli na ni baada ya kuvuta ndumu,yaani imenichagulia hobi nyingine kabisa kiasi kununua bia naona upuuzi.Sikushauri maana tunatofautiana vichwa mkuu,ila Bora ndum kuliko pombe na mafegi.
 
Chukua sigara uiwashe then imwagie pombe kidogo au maji kisha uiwashe unywe, hakikisha upo peke yako maana utatapika hadi uliyokunywa miaka mitatu iliyopita , au ikiwa ngumu hiyo tumia maziwa ya mama anayenyonyesha
 
Pombe huleta uraibu kama uraibu mwingine wowote ule. Hauwezi kamwe kushinda uraibu wowote kwa nguvu zako mwenyewe.

Utajikuta unarudia tu pombe kutokana na nguvu ya addiction. Kitu pekee kinachoweza kukutoa katika Huo uraibu ni nguvu za Mungu pekee.

Muombe Mungu akupe uweza wa kuacha pombe.. nguvu ya kufungua Kifungo cha addiction ya pombe. A day will come ambapo hautatamani tena pombe. Na utashangaa imewezekanaje? Ni nguvu za Mungu hizo.

Hii inahitaji self determination, nguvu isiyozuilika iliyomo ndani yako..nguvu ya maamuzi(will power). Hata kama ukiacha pombe na ukajikuta unarudia tena, usikubali kushindwa...Anza upya Tena.
Ameen
 
Pombe imevuruga mambo yangu mengi sana!
Halafu smts huwa najishangaa unajikuta tu mtu umekamatia jichupa la bia unaligugumia kiwendawazimu pasipo hata kuelea ilikuwaje yaani!

Nachoshukuru Mungu sinaga kiu ya pombe kwamba niikosa ntaumwa, lah ila hutokea tu unatandika glass kupoteza muda na story za hapa na pale.

Mkakati nilojiwekea; sitaki kampani ya pombe make kuna mafala wao kila iitwapo leo wanapenda kitonga tu. Wanataka kununuliwa utafikiri wanawake, hao ndo sitaki kabisa kuwaona.

Siku zote ukimudu kunywa pombe pasipo kampani mbona hutumii hela nyingi. Sana sana utamnunulia mhudumu bia mbili kunogesha meza then chap unajikataa na kurudi nyumbani kucheza na watoto.

Halafu kingine epuka kuwa mtu wa mawazo itapelekea kunywa kupitiliza na kukaribisha kampani za kiboya.
Punguza mdogomdogo na usipendelee kunywea bar moja. Futa hayo mazoea kuna wajinga kazi yao ni kuvizia mida hii jamaa atakuwepo kijiweni ngoja nimnyemelee nikastue nyongo mtu wangu hana baya... nyambaf!!
Tatizo langu mimi sihitaji na sina kampani ila nikianza kunywa na kunywa nyingi na nazimudu ila zinaniharibia utaratibu hata kama pesa ipo kwenye cm nitaitoa tu kesho naanza kujilani na kujilaumu sana sijawahi kuwa na hamu ya pombe na wala sinywi kila siku ila siku ya kunywa ni hasara tu
 
Chukua sigara uiwashe then imwagie pombe kidogo au maji kisha uiwashe unywe, hakikisha upo peke yako maana utatapika hadi uliyokunywa miaka mitatu iliyopita , au ikiwa ngumu hiyo tumia maziwa ya mama anayenyonyesha
Hii ya sigara nitajaribu
 
Amekutoa kiunoni kwake na hizo hizo pombe,,Khasara Zipo tuu na sio lazima ziletwe na unywaji wa pombe
Hakuna aliyekulazimisha usinywe pombe mkuu. Mimi nimesema sinywi, wala sio msemaji wa wengine.
Hizo hasara unazotaka ndio sizitaki sasa
 
Back
Top Bottom