Nataka kuachana na unywaji wa pombe, lakini sijui naanzia wapi

Nataka kuachana na unywaji wa pombe, lakini sijui naanzia wapi

Hello JF

Kama kuna mtu anaweza kunisaidia abc za namna ya kuacha unywaji wa pombe anisaidie tafadhali maana kila nikijaribu nakaa siku mbili narudia...
Pombe ukishaizoea huwa inaingia kwenye damu na inakuwa addiction. Ukitaka kuacha punguza idadi ya vilevi kama ilikuwa bia 5 kwa siku anza mbili mbiliha unapita kavu kavu. Badae unakuja moja moja hadi unazoea. Katika hicho kipindi jiweke mbali kidogo na marafiki zako mnaokunywaga wote, kuwa busy sana na kazi zako au tafuta kitu cha kupoteza mda kama games, fanya sana mazoezi mwili uchoke na ulale, pendelea vyakula vya kupunguza hangover Kama kachumbari n.k. njia nyingine watu wanatumia maziwa ya punda ukiyanywa na ukapiga pombe unasikia kichefuchefu kwahyo huwez tena Endelea.
 
Ishi huku mkuu.
1. Epuka watu watakaokushawishi kunywa pombe
2. Epuka mazingira yatakayokusababisha kunywa pombe.
3. Usiweke pombe nyumbani au sehemu unayokaa.
4. Wajulishe watu unaacha pombe
5. Tatua matatizo ya kihisia na kiakili.
6. Tafuta kitu mbadala cha kufanya.
7. Weka malengo tekelevu ya kuacha
8. Jipongeze wewe mwenyewe kwa kipindi ulichoweza kuacha pombe
9. Usikae na pesa za ziada
10. Jikumbushe na kutafakari madhara ya pombe
11. Tafuta usaidizi na ushauri wa kuacha pombe
 
Haina urith ni upuuz ni addiction tu ukinywa pombe inatoa hormone inaitwa dopamine inakupa furaha .Sasa ukiacha Pata furaha kwenye familia .watoto.umoja na waumini wa dini yako.mapenzi unajikuta pombe ni suluhisho zuri.
Ndo maana walevi wengi pia hawana ndoa nzuri.wanahistoria mbovu utoton . Wametokea kwenye umaskini.watoto wa kambo etc
Mkuu nakubaliana na wewe kuwa ni upuuzi mfano mimi shughuli zangu ni za kusafilisafili sasa nikiwa nyumbani hata mwezi mmoja, miwili nk sinywi pombe tena kwenye mabar naingia kama kawaida na nawahi zangu kuludi nyumbani

Tatizo nikiwa nje ya nyumbani nikikaa huko wiki,wiki mbili au mwezi basi lazima itatokea siku moja,mbili au tatu nitakunywa kila nikijalibu kuishindwa hiyo roho ya kipumbavu nashindwa sijui nifanyeje?

Mfano hapa ninapoandika kwa sasa Nina wiki mbili sijanywa ila utashangaa tu siku za mbeleni nakunywa naomba ushauli wako wa kitaalamu inawezekana kadhia hii ikaniondoka kwenye maisha yangu
 
Pombe huleta uraibu kama uraibu mwingine wowote ule. Hauwezi kamwe kushinda uraibu wowote kwa nguvu zako mwenyewe.

Utajikuta unarudia tu pombe kutokana na nguvu ya addiction. Kitu pekee kinachoweza kukutoa katika Huo uraibu ni nguvu za Mungu pekee.

Muombe Mungu akupe uweza wa kuacha pombe.. nguvu ya kufungua Kifungo cha addiction ya pombe. A day will come ambapo hautatamani tena pombe. Na utashangaa imewezekanaje? Ni nguvu za Mungu hizo.

Hii inahitaji self determination, nguvu isiyozuilika iliyomo ndani yako..nguvu ya maamuzi(will power). Hata kama ukiacha pombe na ukajikuta unarudia tena, usikubali kushindwa...Anza upya Tena.
 
Pombe imevuruga mambo yangu mengi sana!
Halafu smts huwa najishangaa unajikuta tu mtu umekamatia jichupa la bia unaligugumia kiwendawazimu pasipo hata kuelea ilikuwaje yaani!

Nachoshukuru Mungu sinaga kiu ya pombe kwamba niikosa ntaumwa, lah ila hutokea tu unatandika glass kupoteza muda na story za hapa na pale.

Mkakati nilojiwekea; sitaki kampani ya pombe make kuna mafala wao kila iitwapo leo wanapenda kitonga tu. Wanataka kununuliwa utafikiri wanawake, hao ndo sitaki kabisa kuwaona.

Siku zote ukimudu kunywa pombe pasipo kampani mbona hutumii hela nyingi. Sana sana utamnunulia mhudumu bia mbili kunogesha meza then chap unajikataa na kurudi nyumbani kucheza na watoto.

Halafu kingine epuka kuwa mtu wa mawazo itapelekea kunywa kupitiliza na kukaribisha kampani za kiboya.
Punguza mdogomdogo na usipendelee kunywea bar moja. Futa hayo mazoea kuna wajinga kazi yao ni kuvizia mida hii jamaa atakuwepo kijiweni ngoja nimnyemelee nikastue nyongo mtu wangu hana baya... nyambaf!!
 
Back
Top Bottom