Nataka kuanza maisha upya baada ya kukosea kuoa

Nataka kuanza maisha upya baada ya kukosea kuoa

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Mimi ni mtu wa umbo la wastani, niliyebahatika kuishi na mwanamke kijumba na kufanikiwa kupata watoto 2, nimebahatika kujenga nae kibanda na kuwa na kausafiri ka familia.

Kwa visa vya mama huyu na kwa hiyari ya moyo wangu naamua kumwachia vitu vyote na ninaanza upya, mke mpya na kila kitu upya. Naanza kwa kukodi chumba kimoja, kitanda sina, nitalalia mkeka kama ishara ya mwanzo mpya.

Karibuni wachumba wacha Mungu,umri kuanzia 28-32 yrs/Am 40.
 
Mkuu.. Kakufanyia visa gani? Weka hapa maswahibu aliyokufanyia huenda tukakushauri ukapara utatuzi...
 
Duuh. Sema alichokufanyia ushauriwe na kwa nin unahisi ulikosea kuoa?
 
kamani mcha Mungu unatakiwa usamehe saba mara sabini endelea na uliekua nae tatua tatizo lililopo ndio uanaume na si kukimbia matatizo..,
 
Sijakuelewa umeamua kutangaza rasmi unaachana na mkeo au unatafuta mke?

Niidhani kutokana na madhira uliyokutana nayo kwenye ndoa ungeamua kupumzika kupendana?
 
Acha mwanamke aitwe mwanamke tu, kuoa ni kubahatisha sana wengi wa wadada siyo wazuri katika kuishi maisha ya ndoa au ya wawili. Mara nyingi huprentend ukiwa bado hujaamua kuishi nao.

Nakushauri achana naye acha kutesa moyo wako.
 
Kama mkeo ni mshirikina au ni msaliti huna budi kumuacha lakini hana tabia hizo basi usimuache
Dah! Umeongea point lakini kuna vitu vinakela sana sometimes hata kama siyo mshirikina au msaliti.
 
Kilichokufanya umkimbie huyo mkeo ni nn hasa..?
 
Back
Top Bottom