Nataka kuanza maisha upya baada ya kukosea kuoa

Nataka kuanza maisha upya baada ya kukosea kuoa

Nadhani mkuu hukuoa hiyo inaitwa " sogea tukae" kama huna kifungo cha ndoa oa mwingine tu maisha yenyewe mafupi haya.
 
Mimi ni mtu wa umbo la wastani,niliyebahatika kuishi na mwanamke kijumba na kufanikiwa kupata Watoto 2, Nimebahatika kujenga nae kibanda,na kuwa na kausafiri ka familia /.
kwa visa vya mama huyu,na kwa hiyari ya moyo wangu.
NAAMUA KUMWACHIA VITU VYOTE,NA NINAANZA UPYA,MKE MPYA NA KILA KITU UPYA.
NAANZA KWA KUKODI CHUMBA KIMOJA,KITANDA SINA,NITALALIA MKEKA KAMA ISHARA YA MWANZO MPYA.
KARIBUNI WACHUMBA WACHA MUNGU 28-32 YRS./
AM 40.
kibooooooooo
 
Huwa nawaonea huruma sana wanawake kwa mfano hapo kama jamaa Ana kazi take basi ni rahisi kwake kuwa na future nzuri kuliko huyo mke anayetaka kumuacha. 1. Nani huwa anaoa watalaka wanawake kwa sasa hata kama anakipato kizuri? Lakini
2. Wanaume waliowahi kuishi na mke ni rahisi kwao kupata mke na kuishi nae kama ana kazi yake ya kumingizia kipato.

Kazi kwenu mnaoachana kwa sasa!
 
Mimi nadhani utulize akili kwanza...safiri hata kwa week mbili...kama unafanya kazi omba likizo ya week 2, kafanye kutafakari kwa kina...katika kipindi hiki jiulize mambo mengi ikiwemo utakavyowasaidia watoto wako kukua katika misingi uliyotamani wakue.
1) Jiulize kwa nini ni sasa na si kabla hukuondoka?...
2) Je kama ulivumilia kipindi chote hicho, kwa nini umeshindwa sasa? ndo imefika kikomo, yaani huwezi tena? sababu ni zipi...maisha ni kupanga/kuchagua, kama ulizoea mfumo fulani wa maisha, jaribu kuubadilisha hata hapo kwako...mabadiliko yawe chanya,
3) Vitimbi vimezidi na kama vimezidi kwa nini?
4) Jiulize kwa kina namna utakavyoanza maisha upya, utakavyoweza kutatua changamoto utakavyokutana nazo katika hayo maisha...
5) Jiulize utakubali yatakayotokea? Lakini pia, ni vizuri hiyo nyumba na gari ukawarithisha watoto...andika wosia kabisa ili...na hata kadi ya gari weka jina la wanao.

Jaribu kumshirikisha mwenzako hata kama unaona itakuwa hasara, wakati mwingine hawa viumbe wanajifunza kwa vitendo na si kwa maneno...kula hasara hata mara 3. Uone kama atajifunza, ndo mwenzi wako uliyemchagua!!
We unaweza kua ndugu yangu kabisa...ukenyenge ya shy au
 
Umesema unatafuta nini? Mke mpya? Kama uko serious, pole!
 
Huwa nawaonea huruma sana wanawake kwa mfano hapo kama jamaa Ana kazi take basi ni rahisi kwake kuwa na future nzuri kuliko huyo mke anayetaka kumuacha. 1. Nani huwa anaoa watalaka wanawake kwa sasa hata kama anakipato kizuri? Lakini
2. Wanaume waliowahi kuishi na mke ni rahisi kwao kupata mke na kuishi nae kama ana kazi yake ya kumingizia kipato.

Kazi kwenu mnaoachana kwa sasa!
***
Una akili nyingi sana/ thank you!,Mali kitu gani?,endapo una elimu na mshahara wa uhakika./
 
Na wengi wamekuwa wakikimbilia Tatizo bila kuangalia nini kimesababisha.,na Chanzo ni nn..?,anaanza kuhukumu.
Anaangalia alipoangukia badala aangalie amejikwaa wapi akaanguka! Na ndo maana ndoa nyingi zikivunjika jamii nzima inamyooshea kidole mwanamke hawajui kama wanaume wengine ni makorokocho vyuma chakavu
 
--kwa nini wengi huachana na wake zao?,tunao hata viongozi wakubwa na wenye nyadhfa serekalini na hata wafanya biashara wakubwa!.
....ask / je wanakosea?
mi hata sitaki kujua sababu za huko njoo tulisongeshe, kuachana kunasaidia wengine tulio singo tupate wapenzi
 
Wewe unasema umeshafunga naye ndoa kwa sisi wakristo ukifunga ndoa kutengana hakuna mpaka kifo kitakapo kutenganisha ndipo unakuwa huru kuoa mwanamke mwingine sasa wewe unasema ni mkristo mlokole unampenda Yesu hapa ninapata wasiwasi maandiko yanasema samehe saba mara sabini huyo ni mkeo tu kwa kuwa mmekula kiapo mbele ya kanisa na Mungu anashuhudia Mimi huwa nawaambia ndugu kwamba kosea maisha ila usikosee kuoa maana ndoa ni mara moja kinachotenganisha ndoa ni mmoja wapo anapofariki ndipo unapokuwa huru kuoa mwingine sasa wewe kwa imani yako utaoa mwingine na kimaandiko wewe utazini tu na mwanamke huyu uliyefunga ndoa mara ya pili mkeo ni yule wa kwanza ambaye mbingu inamtambua!!
 
Back
Top Bottom