Nataka kuanza ufugaji wa kuku kwa hatua ndogo

Kila la kheri,mimi nataka kuanza mwaka kesho...
Andaa kibunda cha kutosha ufugaji unaanza na maandalizi yaan kabla hujaanza chochote fanya mipango mikakati ya maandalizi ya mazingira ya sehemu yako utakapo fuga na hapa hela inatumika sio kidogo ni ndefu, ukikosea hapo ukaingia kichwa kichwa the rest is history utawasimulia waliokwambia kufuga ni rahisi
 
Una shida ya kiafya? Kwann usijichanganye mtaani mbona kazi za deiwaka nyingi? Kwann unaomba omba mtoto wa kiume? Alafu hii id nafananisha na attention seeker mmoja mjinga mjinga hv
Sina shida ya afya, nina akili ya kuchagua ninachotaka. Kuomba msaada si udhaifu—ila si kila anayesema sana huwa anaelewa sana. 🙂🙏
 
Umesema kweli mkuu, nimekupata. Hiyo 50K siioni kama mtaji wa kufuga kibiashara, ni mwanzo wa kujifunza mazingira kwa idadi ndogo. Sitaki kukimbilia kuku wengi kabla sijajiridhisha na chakula, chanjo na usimamizi. Asante kwa kunikumbusha upande huu.
 
Huwezi kujifunza na mtaji wa 50k hapo ni unacheza makida, kuku kumuhudumia anahitaji vitu mnooo 50k haiwezi kutosha ndio maana nakwambia utakua unacheza sio unajifunza
Inawezekana nisiwe na mtaji mkubwa, lakini sioni kama kuanza kidogo ni kucheza. Naanza kulingana na uwezo wangu, najifunza kwa vitendo na nikiona inawezekana, naongeza hatua kwa hatua.
 
Inawezekana nisiwe na mtaji mkubwa, lakini sioni kama kuanza kidogo ni kucheza. Naanza kulingana na uwezo wangu, najifunza kwa vitendo na nikiona inawezekana, naongeza hatua kwa hatua.
Haiwezekani acha ubishi au sikia sikio la kufa acha anaetaka kukupa akupe ila mimi nakwambia haiwezi kukufikisha popote ni ndogo mnooo
 
Wazo lako ni zuri ila haujalifanyia utafiti. chakukushauri mtafute mfugaji mkubwa mpe wazo lako halafu yeye akugawie vifaranga au uvinunue ila dawa na chakula utegemee kwake mje kulipana kwa kuongeza vifaranga vingine kwa awamu ya pili.

kuna gharama hazikwwpeki na kwa uchache wa kuku inakua ni hasara, mfano kuna chanjo ina gharama zaidi ya mtaji wako ambayo inaweza kutumika kwa kuku mpaka 100 hauoni ni hasara hiyo. huo ni mfano mmoja wapo tuu.
 
Haiwezekani acha ubishi au sikia sikio la kufa acha anaetaka kukupa akupe ila mimi nakwambia haiwezi kukufikisha popote ni ndogo mnooo
Nimekusikia mkuu, na naheshimu uzoefu wako. Sina nia ya kubishana; nitachukua ushauri wako, kisha nitaamua kulingana na uwezo na mazingira yangu. Kila la kheri.
 
Ushauri wako nimeupokea mkuu, hasa kuhusu chanjo na gharama ambazo hazipungui kwa idadi ya kuku. Nitalifanyia utafiti zaidi na kuangalia ushirikiano na mfugaji mwenye uzoefu. Asante kwa kunionyesha upande huu.
 
Nilitaka kusema ivo auze simu yake au kitu ambacho kina thamqn na hela anayohitaji

Pesa haitolew ovyo bila kuifanyiq kaz
Simu yako ina thamani gani? Weka bond acha kujiliza mitandaoni.. ulipewa kazi hutaki unataka pesa tu Kanye west bana.. unazeeka ujue
Nimekuelewa mkuu. Sitaki kuuza nilicho nacho; nataka kutumia nilichonacho kuanza kujenga.
 
Oya kilichoandikwa ni km mtu anataka kucheza mchezosupa au tatumzuka, unaleta mchezo kwenye vitu serious eti unajifunza vifaranga 10 unajifunza au unawachukulia kuku poapoa, vifaranga 10 = mayai 10 nakupa bure kabisa na najua unaenda kuwaua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…