Nataka kuanza ufugaji wa kuku kwa hatua ndogo

Nataka kuanza ufugaji wa kuku kwa hatua ndogo

Mkuu pambana uongeze hiyo capital uanze na atleast 40-50 na uwe serious kwelikweli. Sasa ukianza na hao kumi bado hawajafa kadhaa utabakiwa na nini Biashara kichaa hiyo labda kama unafanya for leasure! Nyumbani tuliwahi fuga broiler wa nyama kama 80-100 kuna msimu Ugonjwa ukapita nao Salalee tulikuwa tunagawa kwa majirani maana unakuta umeamka asubuhi unakuta robo ya banda chali wengine wanasinzia na ukiwaacha mpaka kesho yake hawatoboi. Wewe kama unataka kufanya poultry agriculture Jifunze kwenye vitabu ujue magonjwa yao tiba nk ndio uanze kufuga. Ni biashara nzuri ukiwa na soko. Unakula kuku karibia kila siku šŸ˜‚šŸ˜‚
 
Nimekupata mkuu, asante sana kwa ushauri. Nitakwenda kuchukua kijijini kwa bei ndogo, naamini kwa hiyo 50K nitapata zaidi ya hao 10. Ushauri wako nimeupokea vizuri sana šŸ™
 
Hujaelewa comment yake, wanawake wa mjini wale Wazuri Wazuri wanapata hela nyingi za kupewa na matajiri haya y serikali Kuu, lakini huwa hawafiki popote kwa sababu ni za kupewa
Easy come easy go mkuu hili ni kweli kabisa. Pesa ambayo hujaipambania kuipata hata matumizi yake huwa si ya msingi sana.
 
Nilitaka kusema ivo auze simu yake au kitu ambacho kina thamqn na hela anayohitaji

Pesa haitolew ovyo bila kuifanyiq kaz
pesa ngumu sana na hiyo ya kusaidiwa huwa haikai aingie mtaani vibarua vipo akiwa siriazi atapata zaidi ya hiyo 50K
 
Nataka kuanza ufugaji wa kuku kwa hatua ndogo

Habari wakuu,

Nimeamua kuanza ufugaji wa kuku kama njia ya kujiajiri. Nimesomea mifugo, kwa hiyo nina msingi wa elimu ya ufugaji, changamoto yangu kubwa kwa sasa ni mtaji wa kuanzia.

Sina mpango wa kuanza na kuku wengi. Nataka kuanzia chini kabisa, nijenge mfumo kwanza halafu niongeze taratibu.

Nimepanga kuanza na vifaranga 10.

Kwa hiyo TSh 50,000 nikiipata, mpango wangu wa mwanzo ni:

  • Vifaranga 10: TSh 25,000
  • Chakula cha kuanzia: TSh 15,000
  • Chanjo/dawa za msingi: TSh 5,000
  • Chombo cha maji na chakula pamoja na mahitaji madogo: TSh 5,000

Banda sitajenga jipya kwa sasa. Nitatumia nafasi niliyonayo na kuifanyia marekebisho ili iwe salama, yenye hewa na rahisi kusafisha.

Hatua yangu ya kwanza ni kuandaa banda kabla ya kununua vifaranga. Baada ya hapo nitatafuta vifaranga kutoka sehemu inayojulikana, kuhakikisha vinapata maji, chakula na joto linalohitajika, kisha kufuata ratiba ya chanjo na usafi.

Nataka kuanza na idadi hii ndogo kwa sababu sitaki kutumia pesa nyingi kabla sijajenga uzoefu wa vitendo. Nikiona mfumo unaenda vizuri, nitaanza kuongeza kuku kwa kutumia sehemu ya fedha nitakayokuwa nimepata badala ya kuanza kila mara kutoka sifuri.

Kwa kifupi, lengo langu la kwanza si kuwa na kuku wengi. Lengo ni kuanzisha kundi la kwanza, kulisimamia vizuri na kutengeneza msingi wa kuongeza ufugaji hatua kwa hatua.

Mtaji ninaolenga kuanzia ni TSh 50,000. Kama kuna mdau ataweza kunisaidia kufikisha kiasi hicho nitashukuru, na ushauri wa kuboresha mpango huu pia unakaribishwa.

Nataka kuanza na nilichonacho, kisha kazi ndiyo iongeze uwezo wa mradi.
Wazo ni zuri lakini wewe mwenyewe ni mpumbavu! Yaani umekalisha ma nanihii yako hapo unasubiri mtu aje akuwezeshe elfu 50? Hebu kuwa na aibu mtoto wa kiume!
 
Back
Top Bottom