Nataka kufunga biashara yangu naomba ushauri

Nataka kufunga biashara yangu naomba ushauri

Umeweka kinga hapo?
Kinga ya nini wakati tatizo ameshalitambua lakini hataki kukubali ukweli?
Tatizo bei tu.

Tatizo lake kuu hakuchagua vizuri aina ya wateja wake au location ya biashara yake ziendane na uchumi wa eneo husika na ubora wa huduma zake.

Pili angalia kama umeajiri watu ukiwapa nafasi wanauza chakula wanatia kibunda mfukoni wanapika kingine chap wanakwambia biashara ngumu.

Yalinikuta hayo wakati nimemaliza tu kidato cha sita miaka hiyo nilijaribu restaurant na kusambaza site za ujenzi. Nilifuatilia nikabaini janja yao nikapiga chini na kuwakata mishahara yao.
 
Mchawi bei Tu hapo mkuu , maswala ya uchawi usijarbu kuamini mkuu utateseka Sana , Acha akili ifanye kazi , akili ikikuambia kwamba hili ni tatizo basi lifanyie kazi , usiidharau akili ukakimbilia maswala ya cheap solution za waganga utakuwa confused...hyo biashara nishawahi fanya na nilifukuza Wafanyakazi wote wa kike , nikabakiza mmoja tuu binti bandidu Yule anapiga kazi kisawa sawa , wengine wote wa kiume...

Ule mtaa walinikubali mpak Leo nikipita huwa wanataka nifungue tena mgahawa , kitu kingine kama unaona kushusha bei ili uendane na wala Hoi wa hapo mtaani ni miyeyusho basi lenga kundi Fulani Tu la wateja , kuna wateja wao wanataka huduma Bora tuu , haijalishi mtoa huduma ni Nani wao hawajali , hao ndo uwatengeneze , itachukua mda Ila utawapata
Kwanini ulifunga huo mgahawa
 
Mimi ni kijana wa miaka 22 nimemaliza chuo mwaka huu nina degree ya kodi, baada ya kumaliza chuo kuna sehemu ya biashara nilipata ya mgahawa iko pwani.

Wiki mbili za mwanzo biashara ilienda vizuri lakini baada ya hapo kila tukipika chakula kikawa kinabaki maana kwenye suala la wateja baada ya kupika nlikua nazunguka kuchukua oder.

Usafi nilizingatia sana ila suala ambalo lilikuja kuniangusha nahisi ni kwenye bei maana chakula tulikua tunauza 1500/= ndiyo bei za huku baada ya mwezi ilibidi ugali niuze sh 2000 kutogana na gharama ambazo tulikua tunazitumia kwenye mboga, tangu tupandishe bei ya ugali mambo yamebadilika watu hawaji kula chakula kinabaki cha kutosha wale wateja nliokua nawafata wamerudi kwa watu wao walipokua wanakula zamani maana hapa nimezungukwa na mama ntilie kama watatu hivi.

Chakula kinabaki kingi inabidi niwe nakopa naongezea kwenye biashara ila madeni yanazidi kuongezeka nimekata tamaa na hii biashara ya chakula na hata nkisema niache!

Sijui nifanye nn jamani ni wiki mbili kila siku wali unabaki kama kilo mbili na ugali unakuta inabaki kama sahani saba hivi nisaidieni binti yenu jamani.
Punguza kipimo.

Kama wali unabaki kilo mbili, pika zinazoisha na ugali hivyohiyo.

Usikate tamaa mapema.
 
Niambie unauzia wapi ili niwe nakuja kununua chakula chote kinacho baki kilasiku, maana roho inaniuma sana mtoto mrembo kama wewe unapopata hasara...😊
 
Pole sana huenda bei ya chakula chako na ubora wake ni tofauti haviendani.
Mchawi ni bei tu,wabongo walio wengi wanaangalia bei tu hasa hasa ukizingatia yuko nje ya mkoa wa dar.
Mambo ya ubora ni migahawa iliyopo Posta,Kariakoo,Makumbusho,Sinza,Mwenge na sehemu zingine special kama kwenye Pub/bar kubwa,hotels na malls,nje ya hapo wabongo wanataka bei ya chini tu.
Na kwa vile kosa lake ameshalitambua mwenyewe hapo lazima bei ashushe kisha atabana matumizi kwenye sehemu zingine kwa mfano kama ana wasaidizi 3 abaki na 2 mmoja apumzike hadi hali itakavyotengamaa na kama ana msaidizi mmoja amlipe nusu mshahara kwa muda atake asitake vinginevyo biashara itamshinda.
Pia afanye uchunguzi ni wapi ataweza kupata soko wanalouza bidhaa za vyakula kwa bei rahisi hata kwa kuagiza mikoa mingine.
Akishindwa kufanya haya basi ni bora aachane na hiyo biashara afanye mambo mengine
 
Hapana huko atapotea mazima.. Mchawi bei hapo.. Watu wa uswazi hawataki ubora wanataka wingi kwa bei kitonga.. Ugali mboga 3 wanataka kwa buku jero.. Akishusha bei watarudi wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Pamoja na kuwa Mshana aliwah kuwa mlozi lakin huwa hashauri watu kufanya ulozi kwenye biashara zao

Nimekuwa nikikufatilia sana kwenye komment mbali mbali ili nione utajibu vipi lakin mara nying majibu yako yamekuwa tofauti na wengi tunavyotegemea

Zaidi utashauri kutumia maji chumvi,nilikuwa mara nyingi nakufatilia ili nione walau unashauri kwenda kwa waganga lakin naona unajibu tofaut

hAtimae na mimi nimeamua kutumia maji chumvi kwenye biashara zangu,nadekia maji chumvi na kunyunyiza ili watu wasinigundue kama niko natakasa

Kwenye vyombo vyangu vya usafir huwa navikojolea kwenye rim
 
Umefungua biashara kichwa kichwa bila maarifa/ufundi? ...waswahili hawawezi kukubali ufanye biashara mbele yao
 
Mimi ni kijana wa miaka 22 nimemaliza chuo mwaka huu nina degree ya kodi, baada ya kumaliza chuo kuna sehemu ya biashara nilipata ya mgahawa iko pwani.

Wiki mbili za mwanzo biashara ilienda vizuri lakini baada ya hapo kila tukipika chakula kikawa kinabaki maana kwenye suala la wateja baada ya kupika nlikua nazunguka kuchukua oder.

Usafi nilizingatia sana ila suala ambalo lilikuja kuniangusha nahisi ni kwenye bei maana chakula tulikua tunauza 1500/= ndiyo bei za huku baada ya mwezi ilibidi ugali niuze sh 2000 kutogana na gharama ambazo tulikua tunazitumia kwenye mboga, tangu tupandishe bei ya ugali mambo yamebadilika watu hawaji kula chakula kinabaki cha kutosha wale wateja nliokua nawafata wamerudi kwa watu wao walipokua wanakula zamani maana hapa nimezungukwa na mama ntilie kama watatu hivi.

Chakula kinabaki kingi inabidi niwe nakopa naongezea kwenye biashara ila madeni yanazidi kuongezeka nimekata tamaa na hii biashara ya chakula na hata nkisema niache!

Sijui nifanye nn jamani ni wiki mbili kila siku wali unabaki kama kilo mbili na ugali unakuta inabaki kama sahani saba hivi nisaidieni binti yenu jamani.

2000 sio kiwango wanachomudu, huwezi lazimisha, kuna targeted Market kwenye biashara, kama huwezi uza 1500/- hama.
 
Mchawi ni bei tu,wabongo walio wengi wanaangalia bei tu hasa hasa ukizingatia yuko nje ya mkoa wa dar.
Mambo ya ubora ni migahawa iliyopo Posta,Kariakoo,Makumbusho,Sinza,Mwenge na sehemu zingine special kama kwenye Pub/bar kubwa,hotels na malls,nje ya hapo wabongo wanataka bei ya chini tu.
Na kwa vile kosa lake ameshalitambua mwenyewe hapo lazima bei ashushe kisha atabana matumizi kwenye sehemu zingine kwa mfano kama ana wasaidizi 3 abaki na 2 mmoja apumzike hadi hali itakavyotengamaa na kama ana msaidizi mmoja amlipe nusu mshahara kwa muda atake asitake vinginevyo biashara itamshinda.
Pia afanye uchunguzi ni wapi ataweza kupata soko wanalouza bidhaa za vyakula kwa bei rahisi hata kwa kuagiza mikoa mingine.
Akishindwa kufanya haya basi ni bora aachane na hiyo biashara afanye mambo mengine
Ushauri mzuri kabisa wa kufuatwa
 
Achana na wanaosema ulozi, kifupi huja fanya analysis ya wateja wako, mtaani, km biashara yako haiko naeneo ya serikali basi ujue bei ya 2000 ni kubwa.

Mtaani ugari maharage buku, wao wanaangalia quantity sio quality, ndo mana wanawekewa hamira,

Si either uendane nao au utafute sehemu inayoendana na biashara yako.

Nasisitiza hapo hakuna uchawi,

Mnatype tu hamjafanya biashara na kinamama mtaani [emoji119]

Achana na analysis sijui kitu gani
Simama kwanza na imani yako kikamilifu
 
Izo wiki mbili waliokuja kula sio wateja ni watu waliokuja kukuchora kukudadisi....Hizi tabia nazionaga sana mtaani kwetu.Pakifunguliwa grosari basi wiki nzima hujaza watu.....baada ya hapo unaona wafukuza nzi tu mixa kusinzia....
Hao unaowapa sasa ndio wateja wako wale wa mwanzo ni wapelelezi wakujitolea.
Ushauri jaribu kuboresha kwa kadiri uwezavyo na chakula kiwe kitamu sio kujaza msahani utawapata bodaboda tu na ujiandae kukopwa tu...Chakula kitamu utapa oda za mtu kuja na rafiki yake kula chakula kizuri.
 
Back
Top Bottom