Nataka kughairi kufunga ndoa, zimebaki week 3. Nifanye nini kutimiza azma yangu?

Fanya hivi

Nenda pale Mbezi kwa Msuguri, vuka ile barabara kwa kukimbia huku ukiwa umefumba macho....

Harusi itajikanseli naturally
 
Mkuu, nadhani mpaka nimefikia hatua hyo unajua Mimi sio mtoto , Wala kavulana, bali Ni kidume!

Shda syo hiyo, shida Ni kwamba kadri muda unavyoenda kielekea tarehe husika nasikia uzito kias kwamba najiuliza Kuna Nini huko mbele ya safar?! Kitu kinachonipelekea nitafute mbni za kujinasua
 
Kama ni mtu wa rohoni waone viongozi wa dini na kama ni mtu wa Ndumba na ngai muone Mshana Jr kwa maelekezo zaidi.Siyo kila anayekuja kwenye harusi yako ni msherehekeaji,wengine ni walozi wanakuja kuharibu mambo na ndiyo maana unakuta wengine wanafunga ndoa lakini hawapati watoo,walozi wanapiga pini kizazi na wengine Bwana harusi unapigwa kizizi unakuwa na negative mind juu ya ndoa na hatimaye kuhairisha.Uwezi ukahairisha Jambo ambalo limepitia michakato yote kwa mara moja tu,hapo Kuna namna.
 
Ndoa ni jambo kubwa sana katika maisha hasa kwa wakristu, hutakiwi kuingia ukiwa mzito nafsini mwako. Mshirikishe kiongozi wako wa kiroho, atakusaidia bila kukuabisha.
Asante! Nmepokea wazo lako, ingawa nilihisi nkimshirikisha aidha ataniforce nifunge hivyo hivyo au ataniona msumbufu hivi!

Ila nitajaribu
 

Huwa unamwomba Mungu?
Huwa unaiombea ndoa yako?

Nakushauri uombe sana, ukeshe na kufunga ikiwezekana ili ujue huo msukumo wa kughairi unakotokea.
 

Hii ni hali inaitwa kwa kizungu "Cold Feet" yaani miguu kulegea na kushindwa kutembea ikikaribia siku ya ku wowa, ni dalili kubwa ya uoga.
Mkuu hayo maji umesha yavulia nguo, inabidi uyaoge tu, hatuwezi kuchanga hela zote hizo utuletee huo ujinga, utajua mwenyewe, "umeyakanyaga" - Mandoga.
 
Una umri Gani kwanza, then nikupe mbinu
 
Asante mkuu!
 

Namna ya kuahirisha ni kutoweka nyumbani na Kwenda unakojua wewe tu hadi pale tarehe ya harusi ipite. Ili kutowaweka wazazi kwenye presha kubwa acha ujumbe juu ya kile unataka kukifanya ila hakikisha simu yako iwie hewani. Unaweza kusajili laini mpya ambayo utakua unatumia kununulia bando ili usiwe mpweke.
Na kama moyo wako unasita, nikuambie acha tu Mkuu.
 
Listen to your intuition

Kusema ukweli hiyo hali kama ipo ni bora usioe

Lakini pia usisahau mambo mazuri huweza kuja kupitia mabaya (blessing in disguise)

Sikiliza nafsi yako lakini pia usisahau kumwachia Mungu awe mwamuzi wa mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…