Nataka kujilipua na Volvo XC 90. Ushauri wenu wadau

Brother, huo wimbo wimbo kwenye hiyo video unaitwaje? Wimbo mzuri mno!.
 
Shida ya Volvo XC90 ya 2005 na 2014 unaweza usione major exterior differences.
Ni rahisi kujua; kwani kuna tofauti sana kwenye designs za tail lights, front grill Volvo logo, Volvo emblem (large lettering ya rear logo) ya nyuma na parking sensors etc.
Shida ya Volvo XC90 ya 2005 na 2014 unaweza usione major exterior differences.
2005 model



2014 model

 

Attachments

  • 1688553910428.png
    217.3 KB · Views: 28
  • 1688553955486.png
    264.8 KB · Views: 25
MKUU MAELEZO YAKO YANAONESHA HIZI GARI UNAZIJUA VEMA SANA......ILA PIA UMEKIRI UNAMILIKI VOLVO KWA MIAKA 5 SASA...NAOMBA UNISAIDIE GARAGE UNAYO
TENEGENEZEAGA-NITASHUKURU UKINIPATIA NAMBA ZAO. ASANTE
 
MKUU MAELEZO YAKO YANAONESHA HIZI GARI UNAZIJUA VEMA SANA......ILA PIA UMEKIRI UNAMILIKI VOLVO KWA MIAKA 5 SASA...NAOMBA UNISAIDIE GARAGE UNAYO
TENEGENEZEAGA-NITASHUKURU UKINIPATIA NAMBA ZAO. ASANTE
Sijui upo wapi.
Kwa Dar, cheki Modo garage, Kigamboni. Pia kuna garage moja ipo kule Mbezi kwa Zena (Mwai Kibaki Rd) maeneo karibu na bar ya Amsterdam. Jina limenitoka, ila ukiulizia tu utafika.
Kwa Arusha na Dodoma, cheki Denso garage.
Kwa Dodoma, cheki pia Kyando garage, Kizota.
 
HII REMAPING INAFANYIKA HAPA HAPA BONGO MKUU?TUPE LOCATION BASI KAMA NI HAPA BONGO
Bongo ukimaanisha Darisalama? Kama ndiyo, cheki Outmax wapo Mwananyamala au pia Automax wapo Mikocheni karibu na Sekondari ya Alpha.
 
Nashukuru mkuu...nilipata nyingine pia ipo opposite na mataa ya ITV.....Kama uanatokea bamaga ni upande wa kushoto,wanapaita kwa BIG....au kwa engneer.
 
Yupo sahihi ndiyo na wala sipindi. Na ndivyo wanavyofanya watu wengi wenye uwezo mdogo. Na hiyo hasa ndiyo point yangu. Kujaribu kufanya hili kundi kubadilika kifikra. Kununua vitu kulingana na uwezo wao na siyo kuonyesha ufahari.
Wewe ndo uwezo mdogo , swala la mtu kutaka kununua kitu na kuuliza sio baya anataka kupata uzoefu ilikufanya maamuzi sahihi , kama ulikuwa huna cha kuchangia ungekaa kimya ...

Hao matajiri unaowasema hawakurupuki kununua gari sababu tu wanapesa wanafanya research pia kulingana na interest zao...

Kingine sio kila mtu anunua gari kama chombo cha usafiri ingekuwa hivyo kila mtu angenunua IST , kuna watu magari wananunua kama hobby au starehe .... Acha negative thinking....
 
Ndugu akili kisoda mbona unadandia vitu vilivyokuzidi uwezo? Kuna kuuliza kwa aina nyingi na unapouliza mambo ya gari huku ukiwa na hofu juu ya gharama basi wewe ni mjinga kwa sababu unataka kubena mzigo unaokuzidi uwezo. Sikushangai sana kwa sababu hata magari ya mtumba yalipoanza kuingia kwa wingi, kuna wengi walikimbilia kununua ma-Ranger Rover lakini walipaki baada ya miezi michache kwa kushindwa gharama. Hayo ndiyo manyumbu wanaowaza kununua magari ''kwa hobby'' kama wewe.
 
Ningekushauri ujisomee gazeti la What Car hao wako vizuri sana kwa kupambanua magari ya kila aina kuanzia ubora mpaka mapungufu yake

Kwa kweli Volvo aina zote nimeendesha zikiwa mpya kabisa na ni ngumu kuelezea sana ila 60 niliipenda ilikuwa imetulia sana
 
Hii kauli ya dunia Ni Kijiji hua Ni rahisi sana kuisema,ila kwny utekelezaji hua inaponza sana.
Shipping inatutofautisha kati ya wao na sisi.... u buy a spare lkn when its comes kwenye shipping unajikuta u paid 150% zaidi!.....
 
Unabidi uelewe kitu kimoja unaweza kuwa na pesa ya kununua gari lolote lile na kuhudumia lakini sababu huna elimu ya hilo gari , connection ya mafundi na info nyingine ikafanya gari usidumu nalo ..

Inawezekana hata kumiliki gari ujawahi na unaandika huo upuuzi ukiwa umekaa kwenye kochi la baba ako unasubili Mama apike Ugari ule... Ila kama ulifika hata chekechea wahenga walisema " kuuliza sio ujinga" ...

Kutokana na swali la mdau unaona watu walivyotoa madini na uzoefu wao , hata wewe chizi umejifunza kitu hata ikitokea umeokota gari utajua garage ya kwenda kufanya service......
 
Kwenye malori na mabus hakuna wa kumfikia mswiden

Gari dogo sina experience nalo, kabla hujalinunua uliza kwanza spea zake and services

Ushauri wangu NUNUA MJAPAN, hapa ni mwisho wa maneno🙌
 
kwa wengi wasichokijua tu ni kuwa Volvo ana branch yake kabisa Tanzania. wapo along Nyerere road kama unaedna Airport. acheni kudanganyana eti spare hamna! we huna uelewa
 
kwa wengi wasichokijua tu ni kuwa Volvo ana branch yake kabisa Tanzania. wapo along Nyerere road kama unaedna Airport. acheni kudanganyana eti spare hamna! we huna uelewa
Niliwahi kwenda pale 2019 kwa ajili ya service, wakasema wanajishughulisha na trucks tu.
 
Volvo kodi yake sio kubwa pia TRA wanaangalia gari zilizo kwenye soko ndio wanaongeza kodi Volvo unaweza kupata ya miaka ya karibuni tu na ukalipa kodi nafuu tofauti na kampuni zingine kama Toyota...
Ni gari nzuri zina Confort,speed ipo na balance..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…