Nataka kujilipua na Volvo XC 90. Ushauri wenu wadau

Nataka kujilipua na Volvo XC 90. Ushauri wenu wadau

Volvo ni gari nzuri kwa usalama wako, mojawapo ya gari zenye rekodi nzuri kwenye ajari. Ndio wagunduzi wa seat belt na hawakuweka patent kila kampuni itumie.
Ukiachana na safety kwingineko sio nzuri sana na interior mara nyingi zinakuwa za kawaida
 
Volvo ni gari nzuri kwa usalama wako, mojawapo ya gari zenye rekodi nzuri kwenye ajari. Ndio wagunduzi wa seat belt na hawakuweka patent kila kampuni itumie.
Ukiachana na safety kwingineko sio nzuri sana na interior mara nyingi zinakuwa za kawaida

I think ziko reliable zaidi ya gari nyingi za ulaya, ila labda si comfortable na luxury sana kama nyingine. Zina balance nzuri tho ya hivyo vitu vingine (model za 2009 - 2015)
 
Itoshe kusema kwamba, Waswedish wanatengeneza vyombo vyenye uhakika katika mabasi na Malori kuna SCANIA NA VOLVO hawana mpinzani. kwenye SUV tunajua Japs na Germans wanachuana vikali lakini tunamuunderestimate huyu mnyama VOLVO XC 90

watakuja watu wa Subaru na Toyota, nataka muangalie hii video nayoiweka hapa chini mpaka Range kakaa, na hiyo TLC kakalishwa sasa inakuwaje kwa ndogo?

Team Volvo mnipe uzoefu wa hii gari? Reliability, Comfortability yake Safety na Upatikanaji wa spares zake

Angalia hiyo video 👉👉👉👉👉

View attachment 2480369View attachment 2480392View attachment 2480393View attachment 2480394
Hamna gari hapo utalia kaka magari ya kimarekani hayo speak zake utajuuutaa
 
Kwingineko kupi huko? Performance? Reliability? Prestige? Sustainability? Emissions?
Reliability sio kubwa sana na repairs & spare parts zina bei juu kidogo. Ratings zake ukiachana na safety haina the best performance. Ni brand nzuri lakini
 
Reliability sio kubwa sana na repairs & spare parts zina bei juu kidogo. Ratings zake ukiachana na safety haina the best performance. Ni brand nzuri lakini
Ukilinganisha gari zipi? Maana kama ni likes za Mercs, BMW na Audi, Volvo is way more reliable and maintenance cheaper. Performance, yes imezidiwa na hao.
 
Hamna gari hapo utalia kaka magari ya kimarekani hayo speak zake utajuuutaa

Unafahamu nini kuhusu hii gari, mbona ni kama hujui chochote kuihusu??! Volvo ni msweden mkuu siyo mmarekani. Na ni reliable kuhusu unavyofahamu
 
Chukua boss. Five years of owning one.

Ila nunua angalau la kuanzia 2011; ukiweza 2014. Hiyo 2nd generation kama pesa ipo chukua ya kuanzia 2016.

XC90 ni bonge la gari. Chukua diesel D5. Hii ni turbocharger na inaweza kufanyiwa stage 1 tuning.

Shida ni moja kubwa. Za kuanzia 2011 zote zinakuwa ni Euro 5 kwenye suala la exhaust emission regulations. Hivyo, kwa diesel zinakuwa na vitu vinaitwa diesel particulate filter (dpf) na exhaust gas recirculation (egr). Hii ni mifumo ya kuzuia uchafu wa mazingira kwenye magari ya diesel. Tatizo linakuja kuwa kama wewe siyo mtu wa kusafiri safiri sana (yaani mtu wa safari za home-work-home za mjini), D5 itakuletea shida. Kwani dpf na egr zitajaa na kuziba zile carbon soot/deposits. Dpf ni chujio la hizo gas mbaya na egr urudisha hizo gas mbaya ndani ya injini ili zisitoke kuchafua mazingira. Dpf na egr zikijaa carbon, hapo a spiral of problems ufuata. Una machaguo matatu manne ya kutibu. Moja ambalo ndiyo bora, uwe unafanya safari za mbali angalau mara kadhaa kwa miezi ili uruhusu exhaust kupata joto la kuchomq vizuri hizo carbon soots. Safari fupi fupi, exhaust haichemki vya kutosha kuchoma carbon. Mbili, kuna additives za kununua na kuweka kwenye mafuta, ambazo ufanya kazi ya kusafisha dpf na egr. Hii ni suluhisho lisilo la kudumu na la gharama, na kwa uzoefu wangu siyo la uhakika sana. Tatu, tumia hizi obd2 diagnostic machines kufanya forced regeneration ya dpf. Pata machine yenye function ya kuruhusu kuipa moto exhaust gari ikiwa imesimama, mpaka carbon soot utoka kwenye dpf. Hii nayo siyo ya kudumu, kwani gari nyingi zinaruhusu forced regeneration mara tatu tu. Nne, fanya dpf na egr deletes. Hizi ni reprogramming ya ecu (control box) ili kuifundisha gari kwamba dpf na egr hazipo tena. Hii inaenda pamoja na physical removal ya dpf. Mara nyingi egr inabaki lakini. Changamoto ya hii ni kupata mtaalamu wa uhakika wa kufanya remapping ya hizi ecu za European makes. Maana remapping yake inahitaji umakini mkubwa mno, makosa kidogo tu, upelekee a spiral of problems. Kwa mazingira yetu ya kibongo hii ndiyo suluhisho la kudumu endapo remapping itafanyika kwa usahihi. Kama pesa si shida unaweza kupelekea ecu Afrika ya Kusini au hata Ulaya. Maana remapping inaweza kufanyika hata kama gari halipo hapo.

Ukiona diesel pasua kichwa chukua petrol. Ila chukua T5 ya kuanzia 2011 au ukiweza T6 ya kuanzia 2016.

Utafurahia sana gari. Ila kuwa makini na mafuta. Jitahidi siku zote uweke kwenye vituo vya Total, Puma, Oryx na Engen tu. Maana European makes na mafuta machafu ni kujitafutia shida. Ingawa unaweza kufanya pia remapping ya kuruhusu gari iweze kuvumilia mafuta ya kiwango duni. Au utumie fuel treatment angalau mara 1-2 kwa mwezi.

Mafundi pia kuwa makini. Wengi wanaweza kusema wanaweza, kumbe ni makanjanja. Hapa ni muhimu kulijua gari lako vizuri haswa. Tembelea fora mbalimbali za Volvo. Cheki mafundi na watalaamu wa Volvo Youtube. Pia kuwa na obd2 yako ndogo ya kuangalia afya ya gari lako mara kwa mara.

Na daima lazima ufanye preventive maintenance. Mfano, ujue kama kuna part ambayo gari likifika umbali fulani, ni lazima ukibadilishe n.k.
Bro. Naomba fungua PM au start convo nikureply. Nitashukuru sana.
 
Yupo sahihi ndiyo na wala sipindi. Na ndivyo wanavyofanya watu wengi wenye uwezo mdogo. Na hiyo hasa ndiyo point yangu. Kujaribu kufanya hili kundi kubadilika kifikra. Kununua vitu kulingana na uwezo wao na siyo kuonyesha ufahari.
Kutaka kujua kitu sio ufahari wala uwezo mdogo pana watu vitu wanavijua kweli mimi napoulizia hicho kitu inanirahisishia kuelewa hapo sioni tatizo na gari sio Big ishu saana kama tunavyoaminishwa toeni madini ili watu waendeshe au waishi maisha rahisi kupitia kwa wanaojua...
 
Back
Top Bottom