Nataka kujilipua na Volvo XC 90. Ushauri wenu wadau

Nataka kujilipua na Volvo XC 90. Ushauri wenu wadau

Nimeanza kwa kusema kwenye SUV tunawaona Germany na Japs ndio wanatangazwa Sana na tunasahau kuwa Sweden hawatoi kazi mbovu.

Hii gari iko underestimated sana
Gari ngumu hii acha mzee.
 
Mkeka wa TRA unasoma kama 31 milioni hivi gari utajua utanunua bei gani ila bei plus kodi inaweza kuwa around 70 milioni.

Hii ni toleo la kuanzia 2018. Tanki ya hii gari inabeba around 76 lita za mafuta.

Hii gari inakuja na option ya petrol na ya diesel.

Ya petroleum ni CC 1900 na diesel hadi cc2000 inauwezo wa kutembea Km 17.5 kwa lita moja ya petrol na 18.7 kwa lita ya diesel.
 
Volvo kodi yake sio kubwa pia TRA wanaangalia gari zilizo kwenye soko ndio wanaongeza kodi Volvo unaweza kupata ya miaka ya karibuni tu na ukalipa kodi nafuu tofauti na kampuni zingine kama Toyota...
Ni gari nzuri zina Confort,speed ipo na balance..
Kodi ni milioni 31 kwa toleo hili.
 
Nilitakaga kujilipua na XC 60 toleo la 2011 - 2013. kuna owner mmoja akanikatisha tamaa kwamba lake lilisumbua na fundi akamalizia engine. ila nazipenda hasa mwonekano mpaka sasa.
Gari zote za miaka hii ya sasa zinakuja na advanced features na tech which can be a good thing or bad kwa upande mwingine. Bado nchi zetu tunastruggle kupata huduma nzuri za mafundi pale unapopata tatizo hasa kwa modern cars.
Sina hakika pia kama mchina anayemiliki Volvo hajacomplicate chochote kwenye design na manufacturing ya haya magari. Naamini bado anatembelea falsafa ya mswede yeye akibaki kuwa shareholder mkubwa
 
Itoshe kusema kwamba, Waswedish wanatengeneza vyombo vyenye uhakika katika mabasi na Malori kuna SCANIA NA VOLVO hawana mpinzani. kwenye SUV tunajua Japs na Germans wanachuana vikali lakini tunamuunderestimate huyu mnyama VOLVO XC 90

watakuja watu wa Subaru na Toyota, nataka muangalie hii video nayoiweka hapa chini mpaka Range kakaa, na hiyo TLC kakalishwa sasa inakuwaje kwa ndogo?

Team Volvo mnipe uzoefu wa hii gari? Reliability, Comfortability yake Safety na Upatikanaji wa spares zake

Angalia hiyo video 👉👉👉👉👉

View attachment 2480369View attachment 2480392View attachment 2480393View attachment 2480394
Pata kitu roho inataka...
 
Nilitakaga kujilipua na XC 60 toleo la 2011 - 2013. kuna owner mmoja akanikatisha tamaa kwamba lake lilisumbua na fundi akamalizia engine. ila nazipenda hasa mwonekano mpaka sasa.
Gari zote za miaka hii ya sasa zinakuja na advanced features na tech which can be a good thing or bad kwa upande mwingine. Bado nchi zetu tunastruggle kupata huduma nzuri za mafundi pale unapopata tatizo hasa kwa modern cars.
Sina hakika pia kama mchina anayemiliki Volvo hajacomplicate chochote kwenye design na manufacturing ya haya magari. Naamini bado anatembelea falsafa ya mswede yeye akibaki kuwa shareholder mkubwa

Mafundi wapo, hata modern Toyota zitawashinda kwa maana hiyo. Nunua kitu roho inapenda, ukiwa na wasiwasi chukua IST tuu
 
Mafundi wapo, hata modern Toyota zitawashinda kwa maana hiyo. Nunua kitu roho inapenda, ukiwa na wasiwasi chukua IST tuu
Toyota na Nissan wana wakala hapa hata ununue latest model una uhakika. Jamaa gari yake waliua mafundi ikawa inataka 11 milion. So tahadhari siyo jambo baya wakati mwingine. Au angalau ukijua mafundi wazuri. Kuoenda kitu ni jambo moja na uwezekano wa kulimiliki hustle free ni jambo jingine. Bado nalipenda tho na natamani kupata uzoefu zaidi toka kwa wengine especially waliomiliki used (sio brand new).
 
Kuna awamu fulani ilikuja na kilimo kwanza ghafla BRN🤣😀
 
Bro naomba leads ya hao Mafundi nawahitaji tafadhari.
Mkuu una uhakika? Umeona XC90 zilivyojaa hapa mjini? Nimeishi na Volvo tangu 2007 mpaka 2014. Mafundi wapo na Volvo ni gari moja simple sana kwenye matengenezo. Nazijua inside out hasa za mpakq mwaka 2012. Sasa hivi zimeanza kujaa xc60 za kuanzia 2012 na kuendelea nyingi ukiona inasumbua ujue mmiliki nae sio makini.
l
 
Toyota na Nissan wana wakala hapa hata ununue latest model una uhakika. Jamaa gari yake waliua mafundi ikawa inataka 11 milion. So tahadhari siyo jambo baya wakati mwingine. Au angalau ukijua mafundi wazuri. Kuoenda kitu ni jambo moja na uwezekano wa kulimiliki hustle free ni jambo jingine. Bado nalipenda tho na natamani kupata uzoefu zaidi toka kwa wengine especially waliomiliki used (sio brand new).
Mkuu hata European brands wakala wapo hapa pia, mfano Landcruiser v8 1VD ukiua injectors bei itakuja huko huko 11m, kila modern automobile ni gharama sana maintanance, usione latest toyota au nissan ziko barabarani, watu wamelipia invoice za kutosha maintanance.

Nimetumia baadhi ya local fundi naona wako vizuri, wacheki instagtam autoronics_solutions au car_diagnostics_solutionstz , wengine wataleta list pia
 
Hiyo cx90 bei yake ni around ya 100m na zaidi
Utakua na pesa ndefu we jamaa
 
Kukuongezea tu madini, hii gari ina version za tofauti ukitazama kizembe unaweza jua ni aina moja. Kwa mfano hii uliyopost ni Volvo XC90 T8, ila kuna T7, T6, na T5. Zinafanana sana kimuonekano na usipokuwa mdadisi unaweza hisi ni gari moja.

Ila zina utofauti sana especially kwenye design ya Dashboard, engine, consumption ya mafuta na kadhalika.

Mfano nitakuwekea hapa chini picha za T5 kisha uzilinganishe na hiyo T8 uliyopost utagundua nje ni kama zinafanana kila kitu ila ndani kidogo dashboards zinatofautiana padogo sana. Ila eneo la engine hii ya T8 nadhani ni hybrid kwa maana inatengemea umeme na mafuta kwenye kutembea na kufanya shughuli zake na ndio maana ina low consumption rate ya mafuta.

Anyways, details zipo nyingi bado, nitaendelea kushare zingine panapo majaliwa.

0207234A30231213W00101.jpg
0207234A30231213W00107.jpg
1715838048608.jpg
 
Kwa gari kama hizi za kisasa ukiamua kujivika mabomu kuiagiza ni vema ukazijua mapema kabla ya kuanza kuzitumia ili uweze fahamu functionality zake na namna ya kuzihandle.

Usiagize ukitegemea likileta shida basi utamuachia fundi 100% responsibility ya kuimaintain. Lazima na wewe uwe umeji equip na DIY technical know how knowledge ili usisumbuliwe. Otherwise subiria wakulungwa tuagize unifunze namna ya kuishi nazo.

Subaru, Nissan Dualis, Xtrail habari ilikuwa hivyo hivyo watu walijipanga kwa kujifunza na kuwaachia malegendary watengeneze njia kwanza kabla ya kuvamia kuyanunua kwa speed.

Magari haya ya kisasa yanataka some intellect ownership yenye usomi ndani yake. Madereva wengi wa Tanzania ni wazembe sana hata katika sheria za barabarani unaona namna wanavyopwaya so usishangae wakawa wazembe hata kwenye smaller car maintenance na handlings.

Gari za sasa ni half computerized so zinataka knowledge synchronous kind of bond mentality kati ya dereva/m'miliki na gari. Ukitaka kuleta utegaji gari itakuchukia na kuanza kuleta drama. Ukiipenda na kutaka kuifahamu vema then hapo ndipo utashangaa nayo inaanza kukusikiliza kubond na wewe na mtadumu muda mrefu sana hadi watu watahisi yako haijatokea japan.

Kumbuka hakunaga gari mbovu ila kuna dereva asiyejua namna ya kutunza na kuishi na gari mbovu.
 
Back
Top Bottom