Nataka kujiunga na Upadre ila kuna ufafanuzi ambao sijaupata

Nataka kujiunga na Upadre ila kuna ufafanuzi ambao sijaupata

Wewe unatafuta ajira si utumishi wa Mungu.
 
Wewe unatafuta ajira si utumishi wa Mungu.
Hayo ni mawazo yako Mkuu. Kanisani hakuna ajira mzee, kama shida yangu ni ajira gharama zitazotumika kwanini nisifanye mtaji wa kujiari mwenyewe? Badala ya kuwenda masomoni karibia miaka 14.

Sisukumwi na changamoto yoyote Mkuu.
 
Habari za wakati huu wanajamii.

Moja kwa moja kwenye swali langu la msingi.

Nahitaji kujiunga na Updare wa Kanisa Katoliki, ila kuna baadhi ya maswali sijaweza kupata ufafanuzi wake.

1. Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?

2. Je, ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?

3. Je, kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?

Nakuombeni ufafanuzi wa kina wandugu.
Usije kuwa umeutamani kisa baba paroko anaendesha ndinga Kali na anaishi kwenye bangalow upadri siyo ajira ni utume na unatakiwa kuacha yote ya Dunia kama hujakulia kwenye mazingira ya useminari hautauweza umeshaonja Raha za Dunia vya kutosha ukimuona mtu kavaa Ile kanzu anaongoza misa usimchukulie poa
 
Umenikumbusha kuna kaka wa rafiki yangu alikuwa Mwalimu pale Green acres, amekula vitoto vya shule hadi kachoka then akawa anataka kusoma master's nje ya Tz, wakatiana 30+ eti akaenda ili awe padre, akaenda Morogoro then Dodoma kwaajili ya recruitment.......akafail huko na kurudishwa.....now ana mke na watoto
Walimjuaje?
 
Kifupi makanisa mengine hutafuta mtu aliyetenda dhambi sana akaokoka akatubu zile dhambi nyingi na kuziacha ndio humpa uchungaji nk lakini kanisa Katoliki hutafuta mtu asiye na mawaa kwenye maisha kuanzia family history nk ndio maana vetting yao huwa kali hasa na huchukua miaka Mingi hadi kufikia kumpa upadri
Nani kakwambia watu hutubu dhambi na kuacha kabisa? Wanapewa makanisa na matokeo yake wanakula kondoo wao. Na wengine hujianzishia makanisa yao wenyewe. Unakuta yeye ndi mchungaji, askofu na wakati mwingime hujiita nabii. Mahubiri yao ni umbea tu kanisani. Mf. Huyu mwanasiasa, unasema aliacha dhambi huyu?
 
KUNARAFIKI YANGU ALIKUWA ANATAKIWA APEWE UPADRE WIKI IJAYO NIKASHANGAA NAPISHANA NAYE MJINI JUMAMOSI KWENDA SIMUONI SIJUI NINI KILIMKUTA NA ALIKUWA SHEMASI

POPOTE ALIPI MUNGU AWE NAYE NI MIAKA MINNE SASA ILA
HUYU

TISS ISAAC AMANI ATOLEWW U ASKOFU ANACHOMA WATU NA WENZAKE KWA SERIKALI

ET HACHEKAGI CHEKAGI KUBWE JASUSI NDANI YA BARAZA LA MAASKOFU NA BALAA WAMEMPA UKUU ARUSHA DA VATICAN INAFAIL WAPI SUJUI
 
Mkuu; Kama uko serious fanya /uwe umetimiza au utimize mojawapo ya yafuatayo:
1. Uwe umesoma na kufaulu masomo ya Form six - (any combination) shule sio lazima Seminari. Omba kupitia Baba Paroko wako i.e Nenda kazungumze naye na umweleze nia yako hiyo na Uwe umeshafanya maamuzi ya dhati kwamba unapenda kuwa Padre wa Jimbo au wa Shirika na nini/kitu gani kinakusukuma ufanye hivyo.
au
2.Umesoma huko ulikosoma F6 hadi ukapata cheti kwa ufaulu mzuri ( Diploma au Digrii) na hata kama umeajiriwa, wasiliana na Paroko wako i.e. Omba kupitia Baba Paroko wako kama ilivyoelekezwa hapo juu Na. 1 utapewa maelekezo e.g. unaweza kuelekezwa kujiunga kwenye Nyumba ya Malezi 1yr n.k. and then Philosophy 3yrs then Theology 2yrs. (Hii ni kwa Mapadre wote - wa-Jimbo au wa-Shirika)
#3.Hatua hii ni MUHIMU sana na ndipo wengi hujikwaa. Uwe na TABIA NJEMA na Mtu wa Sala/Mcha Mungu, Hujaoa na ni Rijali. (Ss kwa mfano ww umeshazaa huko mtaani na unataka umwache mzazi mwenzio akihangaika na mtoto wako, hiyo mmmh!. cjui kama ni tabia njema (any way Watakusikiliza tu - ww jenga Hoja bro).
NB: Ili uwe Padre wa Kanisa Katoliki sikutanii wala kukutisha - shughuli yake ni pevu bro.
Kumbe siyo lazima nipitie seminary ambazo ni kwa ajili ya kuwaanda vijana kuwa mapdre wa kanisa Katoliki? Nimepata mwanga sasa.
 
Huo ni utume, watumwa wa utume huo wanao wito... Swali la kwanza je, wewe una wito huo au unataka?

Wito huu unahakikiwa kuanzia seminary ndogo mpaka juu huko, sio rahisi kuchukua "hoehae/mangumbalu" toka mtaani.. Je, wewe umewahi kupita kwenye malezi ya kitume?

Unataka (kadiri ya maandishi yako) kujiunga upadre, je washirika/jimbo?

Haloo, sikukatishi tamaa, lakini una asilimia 0.98% za kuupata.

Mimi sijui lolote, nimelopoka tu.
Hana hata hiyo 0
 
S
Habari za wakati huu wanajamii.

Moja kwa moja kwenye swali langu la msingi.

Nahitaji kujiunga na Updare wa Kanisa Katoliki, ila kuna baadhi ya maswali sijaweza kupata ufafanuzi wake.

1. Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?

2. Je, ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?

3. Je, kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?

Nakuombeni ufafanuzi wa kina wandugu.
Ukiuliza swali la tatu, utakuwa umeukosa automatically.Kumbuka Wana filosofia ya juu sana usizani unaenda kuongea na watu wa kawaida.Wale jamaa ni kama CIA
 
Huingii bila vetting. upadre sio tu kulipa ada
huyu kwa kuwa na mahusiano ya kingono wanaita kuzini na kujaliiwa kupata mtoto tayari keshapoteza sifa ya njee ya kuwa padri. Fanya jitihada za kulea mtoto na sio kondoo wa Bwana. Rafiki yangu mmoja alikua anasoma seminari ndogo akatia mimba binti kule kijijini kwao wakafanya Siri. Wiki moja kabla ya kupata ushemashi ikajulikana, jamaa alitimuliwa bila huruma na Sasa Yuko mtaani bosi kampuni fulani ya serikali na Ana watoto Tisa sasa na maisha yanaendelea
 
Mkuu ushakula mbususu hadi ukapata mtoto ndio unataka kua padre? Mbususu za masista zitakua salama kweli?
 
huyu kwa kuwa na mahusiano ya kingono wanaita kuzini na kujaliiwa kupata mtoto tayari keshapoteza sifa ya njee ya kuwa padri. Fanya jitihada za kulea mtoto na sio kondoo wa Bwana. Rafiki yangu mmoja alikua anasoma seminari ndogo akatia mimba binti kule kijijini kwao wakafanya Siri. Wiki moja kabla ya kupata ushemashi ikajulikana, jamaa alitimuliwa bila huruma na Sasa Yuko mtaani bosi kampuni fulani ya serikali na Ana watoto Tisa sasa na maisha yanaendelea
Mzee ata mm rafiki hivyo hivyo na wiki moja kabla wewe ilikuwa mkoa gan?
 
Back
Top Bottom