Nataka kujiunga na Upadre ila kuna ufafanuzi ambao sijaupata

Nataka kujiunga na Upadre ila kuna ufafanuzi ambao sijaupata

Uwe na elimu ya form six na ufaulu usio chini ya daraja la tatu au uwe umetoka chuo na uwe huna mtoto... utaenda mwaka wa malezi mmoja ... ukionekana unafaa unaenda MAFUNZO miaka mi 3 ya falsafa then miaka 4 ya TAWHID ukitoka hapo unaweza ukapewa Hilo Daraja ...
 
Habari za wakati huu wanajamii.

Moja kwa moja kwenye swali langu la msingi.

Nahitaji kujiunga na Updare wa Kanisa Katoliki, ila kuna baadhi ya maswali sijaweza kupata ufafanuzi wake.

1. Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?

2. Je, ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?

3. Je, kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?

Nakuombeni ufafanuzi wa kina wandugu.
Wewe kamanda kama vipi endelea tu ku Banjuka huko mtaani! Mambo ya upadre yanahusiana na wito. Na kwa bahati nzuri huna dalili hata moja ya huo wito.

Hivyo ukiwa padre uta Banjuka sana wewe!!
 
Ukifika darasa la Saba unafanya mitihani ya seminari ili kukuandaa kuingia kidato cha kwanza ,ukifaulu kwa alama wanazotaka basi unapewa fomu ya kujaza ,unalipa ada zao na ndipo tunaanza kidato cha kwanza ,suala la umri ukiingia kidato cha kwanza unasoma pre_form one mwaka mmoja,mpaka unamaliza sekondari unakuwa umetumikia miaka mitano lakini pia kuna mitihani ambayo unafanya hiyo mitihani ukipata chini ya alama 50 unarudishwa nyumbani kwa maana umeshindwa kuendelea na shule hivyo kama ulianza na miaka 14 utamaliza na miaka 19 ,mwaka wa mwisho wa masomo unachagua masomo yako matatu pamoja na Bible knowledge huku ukichagua shule za kidato cha tano ambazo zinahusika na seminari za kikristo pia unatakiwa ufaulu kwa kiwango cha division one au two zile za mwanzo hivyo ukifaulu unakwenda kusoma kwa miaka miwili yaani five na six ,jumlisha miaka 19 na hii miwili inakuwa miaka 21 baada ya hapo ukifaulu unakwenda chuo kwa miaka kama 6 hivyo mpaka unamaliza unakuwa na miaka 27,28,30 na ndani ya hiyo miaka 6 ndipo unaambiwa hakuna kuona wewe utahudumia jamii tu
Hii taarifa si sahihi.
 
Mafunzo + malezi si chini ya miaka 7 ila wengi wanapiga 8 mpka tisa
 
Ndio nimeishi na mwanamke lakini sikufunga Ndoa Kanisani na tumeachana.
Yani unadhihirisha dhambi ya uzinzi wazi wazi,wewe Kwa lugha ya kanisa ni suria
Pia umesema Una mtoto, huwezi kuwa mseja Huku una mtoto
 
Mkuu!kuwa Baba wa familia ndio utumishi Bora zaidi!!Acha kujiunga na kikundi cha kijasusi cha ulimwengu cha watawa ambao sio watawa Bali waongo zaidi!!kikundi cha siri cha utumishi wa shetani kwa kisingizio cha mungu!!!ACHANA NAO HAO WANAFANANA NA CIA,FBI!!!!NA WANA TABIA MOJA INAYOFANANA NAYO NI KUTOKUA NA FAMILIA YAANI MKE NA WATOTO!!!
 
Umenikumbusha kuna kaka wa rafiki yangu alikuwa Mwalimu pale Green acres, amekula vitoto vya shule hadi kachoka then akawa anataka kusoma master's nje ya Tz, wakatiana 30+ eti akaenda ili awe padre, akaenda Morogoro then Dodoma kwaajili ya recruitment.......akafail huko na kurudishwa.....now ana mke na watoto
 
Hayo ni mawazo yako Mkuu, ila kwa maelezo ya awali ni kuwa kama umefunga Ndoa kanisani haiwezi kubadilika na kutumikia Kanisa, ikiwa una mtoto Kanisa linakutaka kulihakikishia malezi ya Mtoto mpaka atapofika 18years. Mengineyo yatajulikana wakati ukiwa katika mchakato.
Ukatekista utakufaa zaidi maana huna sifa ya kuwa padri. Sifa kuu ya kuwa padri ni kutokuoa na kutofanya tendo la ndoa. Uishi maisha kama ya yesu.
 
Umeendika maelezo mengi sana, nilikushangaa kwa kusema hakuna Padri hoe hae.. huo sio utaratibu wa Mungu, mitume wa Yesu wengine hawakuwa wanajua hata kusoma..

Soma hapa kidogo utaelewa

1 Kor 1 : 27- 29

bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
Washatia Kambi wazee wa kusoma mstari mmoja na kuishi nao[emoji23]
 
Habari za wakati huu wanajamii.

Moja kwa moja kwenye swali langu la msingi.

Nahitaji kujiunga na Updare wa Kanisa Katoliki, ila kuna baadhi ya maswali sijaweza kupata ufafanuzi wake.

1. Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?

2. Je, ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?

3. Je, kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?

Nakuombeni ufafanuzi wa kina wandugu.
Kamuulize paroko au askofu wako
 
Ndugu yangu uwe na sababu ya Msingi kujiunga na upadre.
Kama sababu yako Ni changamoto ya nguvu za kiume ili ukajifiche parokoni , jipange Tena. Mtihani wa kwanza kule Ni Kama inafanya kazi vizuri.
 
Je? Umehifadhi Biblia kwa moyo tena yote mimi ni Muislamu lkn nakusaidia kdg anza hapo au wafuate kina Mazinge watakusaidia jinsi gani walihifadhi hiyo Biblia.
 
Andiko lako linadhihirisha jinsi ulivo mbali na jumuiya yako, mambo yote yanaanzia chini, kama una wito muone mkurugenzi wa miito wa shirika lolote la kitawa au wa jimbo ulipo, majibu utapata. Ila kama una mtoto ni ngumu
 
Ngoja nikienda nitaleta mrejesho sababu huku nilipo nipo mbali na maeneo ya jumuiya yangu. Asanteni.
 
Back
Top Bottom