Mtumaini Mungu
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 879
- 1,084
Nadhani unafahamu kuwa mfumo wa kuwapata mapdre wa kikatoliki sio sawa na ule wa "Uteuzi" aliofanya Yesu.Umeendika maelezo mengi sana, nilikushangaa kwa kusema hakuna Padri hoe hae.. huo sio utaratibu wa Mungu, mitume wa Yesu wengine hawakuwa wanajua hata kusoma..
Soma hapa kidogo utaelewa
1 Kor 1 : 27- 29
bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
Wao wana kanuni, sheria, taratibu na vigezo vyao.. KAMA WEWE NI MKATOLIKI utafahamu, vinginevyo vifungu vya biblia Kuanzia MWANZO mpaka UFUNUO hukuti hata neno "PADRE"
Sitakujibu tena, REJEA MAPOKEO YA WAKATOLIKI kisha usianisha na bandiko la huyu mtu.