Nataka kujiunga na Upadre ila kuna ufafanuzi ambao sijaupata

Nataka kujiunga na Upadre ila kuna ufafanuzi ambao sijaupata

Mkuu mimi kidogo nilipita hizo njia, zamani kulikuwa na mafundisho ya wito kwa wanafunzi wa shule ya msingi (wakatoliki). Na yalitolewa vigangoni (hapa utakuwa unaelewa kama ni mkatoliki). Darasa la saba kuna mtihani wa kwenda seminary. Ulikuwa ukifaulu vizuri wanakupeleka seminary (kuna za jimbo na mashirika) changamoto ilikuwa ada, ada zao zilikuwa juu sana hivyo wengine tukashindwa.

Lakini kwa waliobahatika kuendelea, unaanza pre-form one mwaka mzima. Then unaendelea na Secondary baada ya pre. Wakati wote inabidi ufaulu mitihani kwa passmark zao. Ukizingua wanarudisha home, na wako serious katika hilo. Tabia yako pia iwe njema, ndo maana wanaanza na wewe ukiwa shule ya msingi.

Baada ya secondary unaenda advance, shule zao tena. Huko sasa ndio wengi huwa wanafanya maamuzi ya kuendelea na upadre au kuishia mitini. Wengi wao hutokomea. Kama utafulu fresh advance na somo lao la dini unaenda Chuo, huko me sijui. Lakini kuna mambo mengi mengi. Kuna Theology, philosophy, baadae unakuja kuwa shemasi then flater au flater then shemasi (sikumbuki), na baadae utapewa daraja la upadre. Sio mchezo ndugu.

Kwa scenario kama yako sinahakika, tena wakijua umeshazaa nje ya ndoa ndo kabisa huwezi pata, labda ufiche.
 
Upadre naoutaka ni wa Kanisa Katoliki Mkuu.
Haya maswali nimeyaleta hapa ili kupata mwanga mahali pa kuanzia.
Kuandaliwa kuwa padre inaanza ukiwa mdogo..form one unaanzia seminary. Sasa wewe mwenzetu umeshaishi na mwanamke ukute umegonga wanawake kibao na kufanya starehe zote za dunia hii ndo unataka uende.
Wenzio hawalijui tendo la ndoa likoje (ingawa wanafanya kwa siri). Wewe utaweza kuacha kubanjuana?
 
Habari za wakati huu wanajamii.

Moja kwa moja kwenye swali langu la msingi.

Nahitaji kujiunga na Updare wa Kanisa Katoliki, ila kuna baadhi ya maswali sijaweza kupata ufafanuzi wake.

1. Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?

2. Je, ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?

3. Je, kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?

Nakuombeni ufafanuzi wa kina wandugu.
Nenda kwa katekista wako( kigangoni kwako) atakujibu maswali yako. Kama upo jirani na parokia nenda kwa paroko wako muombe ufafanuzi wa haya utajibiwa. Maana Kuna tofauti ya masharti kulingana na unakotaka kujiungia mfano Kuna mapadre wa Watawa na mapadre wa majimbo.
 
Sasa hivi ajira mtaaani hakuna watu wanawinda upadri zamani ulikuwa unakimbiwa Sasa hivi ma jobless yanataka upadri
nilitaka kusema hili,umeniwahi.
kanisa katoliki walishaliona hili toka zamani.

ndio maana wakaweka masharti magumu ya kiimani, kimaadili na kitaaluma ili kufikia level ya kuwa padre.

wengi wanaoingia kwa minajiri ya kuja kutafuta unafuu wa kimaisha huwa wanaishia njiani.
 
Habari za wakati huu wanajamii.

Moja kwa moja kwenye swali langu la msingi.

Nahitaji kujiunga na Updare wa Kanisa Katoliki, ila kuna baadhi ya maswali sijaweza kupata ufafanuzi wake.

1. Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?

2. Je, ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?

3. Je, kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?

Nakuombeni ufafanuzi wa kina wandugu.
Nachojua usister mpk uwe umefika form 4 tena kama miaka 10 iliyopita
Sijajua upadre
 
Ukifika darasa la Saba unafanya mitihani ya seminari ili kukuandaa kuingia kidato cha kwanza ,ukifaulu kwa alama wanazotaka basi unapewa fomu ya kujaza ,unalipa ada zao na ndipo tunaanza kidato cha kwanza ,suala la umri ukiingia kidato cha kwanza unasoma pre_form one mwaka mmoja,mpaka unamaliza sekondari unakuwa umetumikia miaka mitano lakini pia kuna mitihani ambayo unafanya hiyo mitihani ukipata chini ya alama 50 unarudishwa nyumbani kwa maana umeshindwa kuendelea na shule hivyo kama ulianza na miaka 14 utamaliza na miaka 19 ,mwaka wa mwisho wa masomo unachagua masomo yako matatu pamoja na Bible knowledge huku ukichagua shule za kidato cha tano ambazo zinahusika na seminari za kikristo pia unatakiwa ufaulu kwa kiwango cha division one au two zile za mwanzo hivyo ukifaulu unakwenda kusoma kwa miaka miwili yaani five na six ,jumlisha miaka 19 na hii miwili inakuwa miaka 21 baada ya hapo ukifaulu unakwenda chuo kwa miaka kama 6 hivyo mpaka unamaliza unakuwa na miaka 27,28,30 na ndani ya hiyo miaka 6 ndipo unaambiwa hakuna kuona wewe utahudumia jamii tu
Hapo kwenye chuo sio miaka sita ni saba, Falsafa 3yrs,theolojia 4yrs.
Hujamuweka mwaka wa malezi Na mwaka wa kichungaji

Kwa kifupi mtoa Mada hana sifa ya msingi ambayo ni useja maana ameshaishi na mwanamke na ana mtoto.
 
Yesu alichukuwa watu hoe hae kina Mtume Petro na wakawa bonge ya mitume...
Pole kwa kutonielewa..

Fuatilia radio maria, hili swali limetoka kuulizwa majuzi, this week na likajibiwa na padre mmoja yupo kagera.

Kuna tofauti kubwa sana ya kuwa PADRE KANISA Katoliki na kuwa Mchungaji, n.k katika KANISA jingine lolote.

KUNA JAMBO NILITAKA NIKUELEZE LAKINI ROHO WA BWANA Amenikataza kabisa, Na bila shaka wewe si mkatoliki.

Ubarikiwe
 
Kwa mkatolik pure lazima hayo mambo angekuwa anajua Yan unauliza maswali Kama wew n msabato au Muslim upadri n kwa ajili ya wakatolik
 
Process ya vetting huwa ndefu hasa si chini ya miaka kadhaa
ndugu yangu mmoja aliwafanyiwa vetting ndefu sana, wakamsubiri amalize degree yake ya falsafa.

alipokaribia kuanza masomo ya theology, wakampiga stop. wakamwambia waligundua baba na mama yake hawakufunga ndoa takatifu ya kikatoliki. na huo ndio ukweli.

basi jamaa ikabidi arudi mtaani. uzuri alifaulu vizuri sana masomo yake. yupo usalama wa taifa kwa sasa.

NB: vetting system ya kanisa katoliki ni zaidi ya vetting system ya TISS. jamaa wapo vizuri sana katika information gathering.
 
Hakuna umri maalum mkuu, hata uwe na miaka 80.

Kidato cha sita kwa ufaulu wa daraja la kwanza na la pili au walau stashada (Diploma) kwa ufaulu wa walau upper second na kuendelea.

Kama hamkufunga ndoa ya Kikatoliki unaruhusiwa lakini ulihakikishie Kanisa una utaratibu maalum utakaohakikisha mtoto anapata malezi yote (Kiuchumi) nje Kanisa.

Kila la heri mkuu.
Habari za wakati huu wanajamii.

Moja kwa moja kwenye swali langu la msingi.

Nahitaji kujiunga na Updare wa Kanisa Katoliki, ila kuna baadhi ya maswali sijaweza kupata ufafanuzi wake.

1.Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?

2.Je ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?

3.Je kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?

Mkuu; Kama uko serious fanya /uwe umetimiza au utimize mojawapo ya yafuatayo:
1. Uwe umesoma na kufaulu masomo ya Form six - (any combination) shule sio lazima Seminari. Omba kupitia Baba Paroko wako i.e Nenda kazungumze naye na umweleze nia yako hiyo na Uwe umeshafanya maamuzi ya dhati kwamba unapenda kuwa Padre wa Jimbo au wa Shirika na nini/kitu gani kinakusukuma ufanye hivyo.
au
2.Umesoma huko ulikosoma F6 hadi ukapata cheti kwa ufaulu mzuri ( Diploma au Digrii) na hata kama umeajiriwa, wasiliana na Paroko wako i.e. Omba kupitia Baba Paroko wako kama ilivyoelekezwa hapo juu Na. 1 utapewa maelekezo e.g. unaweza kuelekezwa kujiunga kwenye Nyumba ya Malezi 1yr n.k. and then Philosophy 3yrs then Theology 2yrs. (Hii ni kwa Mapadre wote - wa-Jimbo au wa-Shirika)
#3.Hatua hii ni MUHIMU sana na ndipo wengi hujikwaa. Uwe na TABIA NJEMA na Mtu wa Sala/Mcha Mungu, Hujaoa na ni Rijali. (Ss kwa mfano ww umeshazaa huko mtaani na unataka umwache mzazi mwenzio akihangaika na mtoto wako, hiyo mmmh!. cjui kama ni tabia njema (any way Watakusikiliza tu - ww jenga Hoja bro).
NB: Ili uwe Padre wa Kanisa Katoliki sikutanii wala kukutisha - shughuli yake ni pevu bro.
 
Kuandaliwa kuwa padre inaanza ukiwa mdogo..form one unaanzia seminary. Sasa wewe mwenzetu umeshaishi na mwanamke ukute umegonga wanawake kibao na kufanya starehe zote za dunia hii ndo unataka uende.
Wenzio hawalijui tendo la ndoa likoje (ingawa wanafanya kwa siri). Wewe utaweza kuacha kubanjuana?
Anawinda masista huyo pa kuwapata ndio anataka upadri
 
Pole kwa kutonielewa..

Fuatilia radio maria, hili swali limetoka kuulizwa majuzi, this week na likajibiwa na padre mmoja yupo kagera.

Kuna tofauti kubwa sana ya kuwa PADRE KANISA Katoliki na kuwa Mchungaji, n.k katika KANISA jingine lolote.

KUNA JAMBO NILITAKA NIKUELEZE LAKINI ROHO WA BWANA Amenikataza kabisa, Na bila shaka wewe si mkatoliki.

Ubarikiwe
Kifupi makanisa mengine hutafuta mtu aliyetenda dhambi sana akaokoka akatubu zile dhambi nyingi na kuziacha ndio humpa uchungaji nk lakini kanisa Katoliki hutafuta mtu asiye na mawaa kwenye maisha kuanzia family history nk ndio maana vetting yao huwa kali hasa na huchukua miaka Mingi hadi kufikia kumpa upadri
 
Kwa mkatolik pure lazima hayo mambo angekuwa anajua Yan unauliza maswali Kama wew n msabato au Muslim upadri n kwa ajili ya wakatolik
Yes upo sahihi hiki kijamaa kinauliza maswali ya kitoto kabisa.
Mkatoliki pure hawezi kuwa kama huyo mtoa post.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Ukifika darasa la Saba unafanya mitihani ya seminari ili kukuandaa kuingia kidato cha kwanza ,ukifaulu kwa alama wanazotaka basi unapewa fomu ya kujaza ,unalipa ada zao na ndipo tunaanza kidato cha kwanza ,suala la umri ukiingia kidato cha kwanza unasoma pre_form one mwaka mmoja,mpaka unamaliza sekondari unakuwa umetumikia miaka mitano lakini pia kuna mitihani ambayo unafanya hiyo mitihani ukipata chini ya alama 50 unarudishwa nyumbani kwa maana umeshindwa kuendelea na shule hivyo kama ulianza na miaka 14 utamaliza na miaka 19 ,mwaka wa mwisho wa masomo unachagua masomo yako matatu pamoja na Bible knowledge huku ukichagua shule za kidato cha tano ambazo zinahusika na seminari za kikristo pia unatakiwa ufaulu kwa kiwango cha division one au two zile za mwanzo hivyo ukifaulu unakwenda kusoma kwa miaka miwili yaani five na six ,jumlisha miaka 19 na hii miwili inakuwa miaka 21 baada ya hapo ukifaulu unakwenda chuo kwa miaka kama 6 hivyo mpaka unamaliza unakuwa na miaka 27,28,30 na ndani ya hiyo miaka 6 ndipo unaambiwa hakuna kuona wewe utahudumia jamii tu
Mwaka 2007 nilifanya mtihani wa la 7 pia nikachaguliwa kufanya mtihani wa seminary nikafaulu mitihani yote miwili,nikachaguliwa shule ya serikali na pia shule ya seminary

2008 nikiwa na miaka 14 ilinibidi nianze pre form 1 NAMUPA SEMINARY SCHOOL iliyopo Lindi

Na ili uchaguliwe ilikuwa kuna system inaagalia wanafunzi vichwa darasani na ambao familia anayotoka haina makandokando!!!..Kata mzima mm ndy nilifanya mtihani na nikafaulu..darasani mnakutana vichwa kwelikweli kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na darasa la pre form 1 kilikuwa halizidi wanafunzi 25,na ilikuwa si ajabu kumaliza form 4 watu 10-15

Ni shule iliyotoa vichwa Kama Hayati Benjamin Mkapa Benard Membe na Mzee wangu mwenyewe

To make the story short,hayo uliyoeleza yote ndy alipaswa afanye na Kwa sasa ameshachelewa..hawezi kuwa padre
 
Pole kwa kutonielewa..

Fuatilia radio maria, hili swali limetoka kuulizwa majuzi, this week na likajibiwa na padre mmoja yupo kagera.

Kuna tofauti kubwa sana ya kuwa PADRE KANISA Katoliki na kuwa Mchungaji, n.k katika KANISA jingine lolote.

KUNA JAMBO NILITAKA NIKUELEZE LAKINI ROHO WA BWANA Amenikataza kabisa, Na bila shaka wewe si mkatoliki.

Ubarikiwe
Umeendika maelezo mengi sana, nilikushangaa kwa kusema hakuna Padri hoe hae.. huo sio utaratibu wa Mungu, mitume wa Yesu wengine hawakuwa wanajua hata kusoma..

Soma hapa kidogo utaelewa

1 Kor 1 : 27- 29

bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
 
Back
Top Bottom