Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

vipi kuhusu hizi MAN naziona zimekuwa nyingi nyingi barabarani
 

Kwa swali lako, jitahidi kujifunza basics za biashara; kabla ya kuamua unawekeza wapi lazima ufanya utafiti binafsi na ujihakikishie binafsi unafanikiwa!

Biashara sio how much money I make only, hayo yanaathiriwa na:

  • Uwezo binafsi na busara ya kufanya biashara.
  • Mahusiano na wateja, dereva na jamii nzima.
  • Upatikanaji wa Biashara husika, namaanisha wateja.
  • Mamlaka husika na Sheria za uendeshaji wa hiyo biashara!

Haya ni ya muhimu kabla ya kusema naingiza ziku ngapi kwa siku! Huwezi ingiza kitu kama una gari jipya la Japan kama:

  • Hauna skills za biashara na namna ya kushughulika na dereva etc.
  • Hauna namna nzuri ya kutafuta na kushughulika na wateja.
  • Haujatafiti vibali na vitu gani unaitaji ili ufanya biashara kihalali.....
 
Mimi ninaipenda hii biashara ya usafirishaji ila kuna mdau alinishauri kwanza nianze na fuso ya kawaida ama tandam.
Ni kweli ila kwa kuwa bado ni mshamba kidogo na vyombo vya moto...nakushauri ungeanza na mkokoteni wa mizigo pale Kariakoo ama Temeke sokoni. Mdogo mdogo utafika tu,
 
bei za madalali zinajulikana sio rahisi kupigwa.vipi kuhusu 113?
 
bei za madalali zinajulikana sio rahisi kupigwa.vipi kuhusu 113?
Siishauri sana japo ni chombo ya kazi haswa, hii ikizingua unagonga nyundo mbili tatu chombo inakaa sawa.
Ila hizi gari z R series jamani kama ndio unaanza hii biashara USIGUSE narudia USIGUSElabda uwe mzoefu kwenye sekta hii. Chukua 124L auu 114 L utanishukuru baadae na hiyo 124 HAKIKISHA ISIWE RED DOT iwe 124 420 plain maana red dot itakubidi ukafumue mfumo wote wa upoozaji ili ikae kikazi
 
Ni kweli ila kwa kuwa bado ni mshamba kidogo na vyombo vya moto...nakushauri ungeanza na mkokoteni wa mizigo pale Kariakoo ama Temeke sokoni. Mdogo mdogo utafika tu,
Mnafungua id mpya,alafu mnaleta porojo.
Nishatoka kwenye ayo maisha ya mkokoteni miaka ya 2000,kwa sasa naweza kukulisha wewe na ukoo wako wote mpaka kijiji chenu.
Kama unabisha sema nianze kuwalisha.
 
wanasema changamoto ya 113 ni ulaji wa mafuta
 
wanasema changamoto ya 113 ni ulaji wa mafuta
Hivi umewahi kukutana na R iliyochanganyikiwa au 124 red dot iliyovurugwa??😁😁😁😁 siishauri 113 kwa sababu moja tu nayo ni kuwa imekua gari ya kizamani sana kiasi kwamba haina comforty kwa driver pia vipuli vyake ni mwendo wa used. Kuhusu mafuta ni kweli japo sio sana ukilinganisha na 124
 
Tanzania yapo magari mangapi?? yote yametumbukia ? biashara zote zina risk mkuu, na zote zina risk za kuhatarisha na kuua mtaji wote , ndio maisha yalivyo, tuna options mbili tu either tufanye au tusifanye
Kwamba ukizaa mtoto akifa unaacha kuzaa au basi na watu wengine pia wataacha kuzaa.
 
Sikiliza mkuu mimi sina dharau ila huwa naangalia mtu amenijibu vipi na mimi ndio namjibu kulingana na majibu yake.
Ukija vizuri nitakujibu vizuri na ukija vibaya nitakujibu vibaya accordingly yaani ni mtu napanda na kushuka.
Ila wewe ukitaka nikunyenyekee hapo kweli utaniona mimi nina dharau au jeuri.
 
Kifo hicho mkuu kwa nini usikope tractor la NewHolland au zile gari za tata.
 
Usimpangie mwenzako mkuu anajua anachokifanya hadi kuamua kununua gari la mizigo
 
Mayai yote (Hiyo mil 100)ukiweka kwenye kikapu kimoja (biashara moja)inaenda kula kwako!Hiyo hela igawe kiasi kwamba ufanye biashara zaidi ya mbili.
 
Huyo hajui systems za breki chief.
Siku nikipata muda, nitakuja nitowe somo la jinsi upepo unavyo fanya kazi kwenye systems za magari hasa Scania
Mkuu nakukumbusha ukipata muda toa somo tuweze kunufaika. Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…