Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Ikiwa Vanilla inaweza kukupa 100 Million unawazaje kuiacha na kukimbilia ambayo huijui? Nikupe ushauri achana na biashara ya logistic kwa sasa changa hele yako kwa kuiwekeza kwenye kilimo zaidi. Watu mnahangaika na vitu ambavyo hamna ilihali mlivyo navyo mnaviacha... komaa na kilimo ndio karama yako ilipo.
 
Eeh
 
Hapo kwenye kuwaepuka madalali sio poa,dalali hakwepeki na ukifanya bila dalali biashara yako hutoifanya kabisa
 
Kiongozi nimekuelewa sana. Upo vizuri kwenye udadavuzi
 
Ninahisi Mkuu hamaanishi kwamba anaacha biashara ya Vanila anaendelea nayo huku akiwekeza mtaji kwenye maeneo mengine.
 
Umesomeka Mkuu.
 
Kama utaamua kuanza na gari toka ukoo wa mzee Mitsubishi basi achana na tandam ila chukua fuso kipisi beba tani zako 7au 8 baas. We mwenyewe jiulize tu gari ulikua designed kubeba tani 5 ila Bongo Pasua Kichwa Engineering wanaifanya ibebe tani 18.
Ila wabongo, aaaah wabongo balaa tupu
 
Bora hiyo hela ujenge lodge Dodoma utapiga hela sana
 
Kwanini sio scania mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…