Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nimepata kama mil 100 baada ya kuvuna vanila huko Bukoba. Sasa nahitaji nijiingize kwenye biashara ya usafirishaji na wazo langu ni kununua scania kama kwenye picha

Nimepanga kuanza na moja kutokana na kiasi nilicho nacho

Naomba wenye uzoefu, kama biashara ikienda vizuri, kwa mwezi naweza ingiza kiasi gani?
View attachment 1484199


Swali la nyongeza 24 June 2020
Vipi biashara ya kusafirisha
Mafuta vs Mizigo
Ikiwa Vanilla inaweza kukupa 100 Million unawazaje kuiacha na kukimbilia ambayo huijui? Nikupe ushauri achana na biashara ya logistic kwa sasa changa hele yako kwa kuiwekeza kwenye kilimo zaidi. Watu mnahangaika na vitu ambavyo hamna ilihali mlivyo navyo mnaviacha... komaa na kilimo ndio karama yako ilipo.
 
Ikiwa Vanilla inaweza kukupa 100 Million unawazaje kuiacha na kukimbilia ambayo huijui? Nikupe ushauri achana na biashara ya logistic kwa sasa changa hele yako kwa kuiwekeza kwenye kilimo zaidi. Watu mnahangaika na vitu ambavyo hamna ilihali mlivyo navyo mviacha... komaa na kilimo ndio karama yako ilipo.
Eeh
 
Kwa pesa ya kwanza nakushauri tafuta 113, 124 na kisha zifanyie matengenezo ya kutosha ndipo uweke barabarani.

Tatizo la R420, R440 zinahitaji uwe na akiba walau isiyo pungua 30millions just for emergency. Pia spare zake ni ghali sana pale SubScania, na hata sisi mafundi tunawachinja sana wamiliki wa R.

Mwisho nikukumbushe tu usisahau kukata bima kubwa yasije yakakutokea kama yule mama.

Pia biashara ya usafirishaji unapo ianza ni vyema ukaisimamia mwenyewe kwa ukamilifu na kila hatua, hii itakusaidia kupata uzoefu wa magonjwa ya magari pia jinsi ya upataji mizigo pasipo kupitia madalali.
Hapo kwenye kuwaepuka madalali sio poa,dalali hakwepeki na ukifanya bila dalali biashara yako hutoifanya kabisa
 
Japo sipo kwenye mood ya kuandika, lakini nikipita kimya nitakua sijakutendea vema wala kuitendea vyema nafsi yangu.
Nina uzoefu niseme wa kutosha kuweza kutoa 'expart opinions' kwa mtu anyetaka kuanza biashara ya usafirishaji kwa kumiliki malori.
Nawapongeza wachangiaji wenzangu kwenye uzi huu, ila kuna mawili matatu nimegundua toka kwa hao wenzangu japo kuu hasa ni hili.
-Wengi hawana taarifa kamili na sahihi juu ya bei na uhalisia wa aina anuai za magari pia uhalisia katika sekta nzima ya usafirishaji hapa nchini.
Wengi wameshauri na umeonesha kuridhika na ushauri juu ya kuanza na Fusi-tandam. Mimi kwa uzoefu wangu sikushauri kuanza na tandam kwa sababu zifuatazo;
+ Gharama. Ununuaji na ubireshaji wa tandam huweza kufika 80-100mil hii ni gharama kubwa sana kwa gari ya tandam ukilinganisha na performance yake barabarani.
+Matunzo. Tandam ina gharama kubwa sana katika matunzo hasa hasa engine. Ukumbuke ile ni engine yenye HP kama 200 hivi lakini inabebeshwa tani 18 hivyo injini huchoka haraka na kuhitaji kubadilishwa. Ni kawaida kwa life span ya injini kwenye tandam kuwa miaka minne japo mara nyingine huweza kujikongoja hadi 8 kutokana na nidhamu yako ya kuibebesha mzigo
+Mifumo ya uendeshaji. Tandam nyingi hasa hasa nikiwa ni mzigo hata tani 12 tu ujue haina uwezo wa breaking za ghafla so katika kipengere hiki tegemea neema ya Mungu na kuthibitisha hili fuatilia ajali za tandam kugonga gari nyingine kwa nyuma utaambiwa sababu.

Kama utaamua kuanza na gari toka ukoo wa mzee Mitsubishi basi achana na tandam ila chukua fuso kipisi beba tani zako 7au 8 baas. We mwenyewe jiulize tu gari ulikua designed kubeba tani 5 ila Bongo Pasua Kichwa Engineering wanaifanya ibebe tani 18.
USHAURI WANGU SASA.
Kwa mtaji wa milion 100, anza na gari ambayo gharama ya manunuzi yake hadi kuingia road yaani horse na trailer yake isizidi 80ml.
Hapa utaona kipi rahisi kwako either kuagiza used ulaya au used ya kibongo bongo, ambapo kwangu naona ni sawa tu japo hakikisha kama ni used ya kibongo bongo usichukue iliyoingia nchini zaidi ya miaka miwili nyuma.
Hapo ukitaka kuagiza ni vema ukaanza na gari ambazo ni rafiki kwa mafundi na vipuri vyake mara ipatapo faida. Nashauri Scania series 4 yoyote kati ya 114 au 124 horsepower yoyote hamna shida najua hiyo hadi inakaa road itakugharimu kwenye 60ml hivi na trela lake ni 20ml tu.
Anza na safari za local na kwa kuwa wewe ni mgeni basi kichwa chako ni halali ya Dalali na atakupiga sana katika miezi mitatu ya kwanza hadi kichwa kikukae sawa utengeneze wateja wako. Route zinatofautiana na msimu kwani kuna wakati nyanda za juu kubalipa na kuna wakati kanda ya ziwa kunalipa.

Oya nimechoka kutype, ntaendelea kesho
Kiongozi nimekuelewa sana. Upo vizuri kwenye udadavuzi
 
Mtoa mada kama kweli kilimo cha vanilla kimeweza kukupatia mil 100 nakushauri endelea tu na kilimo.

Kuhamia kwenye biashara ambayo huijui tena ya magari hii inaweza kuwa ndo downfall yako na baadaye kwenda kwenye uzi uleeeee wa waliowahi kushika pesa ndefu halafu gafla zikapotea.

Hili ni wazo tu lakini maana kuna wengine wameweza kubadili biashara pia wakafanikiwa.
Ninahisi Mkuu hamaanishi kwamba anaacha biashara ya Vanila anaendelea nayo huku akiwekeza mtaji kwenye maeneo mengine.
 
Mfumo wako wa biashara ni upi? Au unamuachia dereva ndio akuamulie? Wengi wanaanza biashara bila maamuzi ya uendeshaji wa biashara. Wananaachia madereva wawaamulie.
Mfano.
Biashara ya pikipiki na bajaji na teksi kwa sasa ina mifumo 2 mikubwa.
1. Mkataba. Unamnunulia, mnakubaliana hesabu kwa wiki na muda, say mwaka na nusu baada ya hapo chombo kinakuwa chake. Wakati wote kinakuwa kwenye bima kubwa.
2. Hesabu kwa siku ila malipo kwa wiki. Hapa chombo ni chako hivyo matengenezo ni juu yako. Hapa unachochochunga vi hesabu na uzima wa chombo.

Ukiwa tajiri wa chombo cha moto kama dereva anatunza chombo na analeta hesabu usimuonee wivu.
Matajiri wengi hawaki kumuona dereva akibadilika hata kama kila kitu kiko sawa.
Kila mtu anahitaji maendeleo. Ni pamoja na dereva wako.
Umesomeka Mkuu.
 
Kama utaamua kuanza na gari toka ukoo wa mzee Mitsubishi basi achana na tandam ila chukua fuso kipisi beba tani zako 7au 8 baas. We mwenyewe jiulize tu gari ulikua designed kubeba tani 5 ila Bongo Pasua Kichwa Engineering wanaifanya ibebe tani 18.
Ila wabongo, aaaah wabongo balaa tupu
 
Bora hiyo hela ujenge lodge Dodoma utapiga hela sana
 
Mimi hii kitu naijua nje ndani yani mkuu kuanzia kuendesha nilijipatia uzoefu najua mipigo ya madereva najua faida najua vimeo

Na ni kweli inawezekana kuanza na gari moja mie nilianza na Tani 2 ya Mazda Titan miaka Mingi nikaja Kenta 3.5 Fuso Tandam/Kipisi ambacho saiz ni Mende na nna Semi za Howo . Mungu akisaidia ntatafuta Pulling ila sio Scania
Kwanini sio scania mkuu?
 
Back
Top Bottom