Nimepata kama mil 100 baada ya kuvuna vanila huko Bukoba. Sasa nahitaji nijiingize kwenye biashara ya usafirishaji na wazo langu ni kununua scania kama kwenye picha.
Nimepanga kuanza na moja kutokana na kiasi nilicho nacho.
Naomba wenye uzoefu, kama biashara ikienda vizuri, kwa mwezi naweza ingiza kiasi gani?
View attachment 1484199
Mkuu,
Nikupongeze sana kwa uthubutu huu.
Hii biashara ni nzuri ila ina changamoto zake za hapa na pale ila ina pesa.
Ili uweze kutoboa kwenye hii biashara jitahidi kumudu jazba zako kwa dereva wako tena hasa akiwa porini, Dereva ndiye mtu anayeweza kukufanya ufanikiwe na kukufanya ufeli mazima.
Trailer zipo za aina mbili,
Flatbed na Skelton
Kwa vile wewe ndiyo unaanza basi nakushauri uchukue flatbed kwa sababu kazi zote utabeba. Vilevile uchukue Trailer yenye (axles za BPW).
Kampuni zinazozalisha hizo trailer zipo nyingi hapo mjini, Superdoll, Simba na wengineo, Nashauri ununue trailer za mtumba.
Kikazi,
Kuna trip za local( za ndani)
Kuna trip za transit ( Nje ya nchi)
Trip za ndani sikushauri uzifanye kwasababu zinachosha gari na magurudumu. Ni bora ufanye hizo za Transit tu, tena za Dar - Lubumbashi tu.
Trip za Dar - Lubumbashi hazichoshi gari ingawa gari inachukua mwezi mzima au zaidi lakini pesa yake unaiona, Gari inaenda na mzigo na inarudi na mzigo (Copper)
Sasa ili uweze kufanya hizo trip za transit kwa mtu wa gari moja, nakushauri ufanye joint venture na mtu mwingine ambaye ana gari nyingi ili uweze kupata c28 ya TRA na hii itakusaidia kujikusanya na kujifunza mchezo.
Kwanini nasema hivyo, sijajua mfuko wako ukoje ila kuna mlolongo wa makadirio ya kodi, kukata vibali vya Zambia na mambo mengine, kwa gari moja ni story tu.
Mkuu, Magurudumu ya gari yako hakikisha umenote zile serial number na uwe mfwatiliaji wa kuyakagua kila baada ya trip.
Dereva mtaji wake ni Diseal na Magurudumu, akiishiwa huko njiani anayanywa fasta na yanauzika sana hapo Tunduma au huko Mpika.
Punguza wanawake (Mademu) magari ni kama Majini hayapendi uchafu wa mwili, na pia dereva asikuzooee sana maana wanakuwaga na vinasaba vya kiswahili unaweza kujikuta yeye ndiye kawa boss na wewe ukawa mfanyakazi wake. Zingatia Services ya gari, usifuge magonjwa kwenye gari!
Naomba niishie hapa,
Cheza na dola mkuu.
Shukrani