Nataka kununua mabasi ya kusafirisha abiria mkoa mmoja hadi mwingine

Nataka kununua mabasi ya kusafirisha abiria mkoa mmoja hadi mwingine

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Palipo na nia pana njia

Ni ndoto yangu ya muda mrefu ya kuwa na kampuni kubwa ya mabasi ya usafirishaji abiria.

Hivyo basi pamoja na maombi yenu ninaomba pia tusaidiane kushirikishana je ni ruti ipi ambayo ina uhitaji mkubwa wa mabasi au ruti ipi ambayo nitapiga hela kisawasawa.

Baada ya mapendekezo nitakuja kuleta mrejesho na kampuni yangu mtaijua.

Hilo la kwanza, jambo la pili, kwa sasa kampuni ipi nzuri ya kuagiza ama kununua mabasi (luxury), je YUTONG, au ZHONGTONG, pia naomba unapotaja ruti ya basi, pia pendekeza njia hio je YTONG itaweza au zingine, pia na bei zake. Na ni namna gani ya kuagiza.

Shukrani.
 
Kila la heri mkuu.

Mimi sio mzoefu wa magari ila ni abiria wa mara kwa mara. Mabasi ya kichina hayatofautiani sana ki ubora, nadhani suala la basi kuwa luxurious unaongea tu na manufacturers wa hayo magari ili waya customise kulingana na mahitaji yako.
 
Kuna jukwaa la magari hapa JF, nenda huko ukapate mwanga.

Hayo ya kichina yanafaa njia za lami, dar to moro.
Unamuona abood ameyajaza kama njugu,
Nawe mtaalamu wa magarii🤣😂😂🤣
 
Kama hujamaliza kuzaa watoto usijiingize kwenye hiyo biashara.

2. Pia kama una pressure jiepushe na hiyo biashara

3. Usipeleke hati ya nyumba zako bank ukachukua mabasi ya biashara

4. Kama huna biashara zingine za kukuingizia kipato usijiingize kwenye hiyo biashara tena kwa kukopa

5. Bima kubwa ni muhimu kwa mabasi unayotarajia kununua

6. Wapigadebe ni adui namba moja wa hiyo biashara, waepuke

7. Epuka ushabiki wa kununua mabasi bila kufanya utafiti wa kutosha

8. Mchina bidhaa zake mungu anajua, kimbilia scania mpya

9. TRA , sumatra, trafic, wapigadebe, agents, ni adui zako kuanzia siku ya kwanza kununua mabasi

10. Epuka kununua mabasi yaliyotukika nunua mabasi mapya, gari iliyotumika ni mke au mume wa mtu.

11. Usisikilize wapiga debe ukaamua kununua mabasi, fanya utafiti wako mwenyewe
 
Chukua higer ndo gari zilizopo sokon zinanzia mil 300, root anzisha dodom to songea kuna kipind kulikuwa hakuna hii ruti lkn pia ksakazin anzisha mosh to mpwapwa/kongwa/ ushindan sio mkubwa na pia ni lam tupu, kuhusu uagizaj kuna jamaa namjua huwa anafanya hiyo mishe ya kununua gar na anazileta tz

So kwa kifup biashara ya mabasi usitegemee basi moja, kukuletea mengine, angalau uwe na hata matatu ya kuanzia, kuna mtu alianza na tata moja toka tanga to dar, lilipoanza kusumbua alipaki ikawa hasara mwingine pia alikuwa njombe alikuwa na basi kubwa mbili za dar zinapishana njian, badae moja iliharibika ikawa inapiga moja, abiria walikuja kupukutika kama majan

So jipange kuanzia tatu angalau bila pressure kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom