Nataka kununua mabasi ya kusafirisha abiria mkoa mmoja hadi mwingine

Nashauri aina ya bus yutong ruti ifanye ya Dodoma hadi Mtwara au Masasi.Kama inawezekana tafuta basi ambalo lina choo ili kusiwe na tatizo la kusimama Mara kwa Mara abiria wakichimba dawa.Ruti nyingine ni Nachingwea to Morogoro.
Mkuu hapa kuna umuhimu ukatoa maelezo hasa mifano ya kampuni bus la baraka linafanikiwa moro-masasi, maning nice, pia ukadadavua potentiality ya Nachingwea in one? Baraka Ana Bus aina ya HIGHER. briefs kuhusu abiria, Nauli Zake fluctuations za passengers, motivational factors za flow btn Point A na B Predominant livelihood activities kama stimuli ya kibiashara na etc.
 
Yutong barabara ya vumbi ni moto wa kuotea mbali,root ya Isangawana ~ lupa ~ makongorosi ~ chunya to mbeya hiyo sehemu wanapiga hela sana, hiyo barabara kuna abiria wengi kuliko mabasi yaliyopo.
Kuhusu bei wananzengo wataendelea kukujuza.
 
Ukishamaluza process zote njoo inbox nikupe mchongo wa ruti Babu kubwa,ni ya kijania.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
Karibu sana kwenye biashara pasua kichwa na ya uhakika kupata pesa kwa siku.

Ushauri wangu: Anza kujenga moyo wa chuma ili usije kufa kwa stress ndo utafanikiwa saaaana
 
Shukran mkuu, nmechukua ushauri wako
Nmegundua wenye ruti fupi fupi wanafanikiwa sana kwenye business
Mfano kama Shabbiby ama Abood wanakaa kwenye soko kwa muda mrefu kutokana na uwekezaji wao wa ruti ya Dom to Dar sio ndefu ni fupi,basi linapata muda mwingi wa kupumzika na kufanyiwa service,sasa wewe unapeleka chombo Mwanza kinaingia Usiku saa 5,Halafu saa 11 alfajiri chombo ichoicho kinageuza dar kwanini mpaka hapo usifirisike.
 
Weka route ya Sumbawanga-Dodoma via Mbeya and Iringa.

Pia weka njia ya Kigoma-Mbeya via Mpanda and Sumbawanga.

Mwisho weka njia ya Sumbawanga-Songea-Mbinga.

Mwisho weka route ya Mbeya-Sumbawanga- Mpanda.
 
Hiyo route imeshajaa tena yapo yanaanzia hadi mbinga.

Pia kuna mwamba anapiga Songea Mwanza via Dom.
 
Nashauri aina ya bus yutong ruti ifanye ya Dodoma hadi Mtwara au Masasi.Kama inawezekana tafuta basi ambalo lina choo ili kusiwe na tatizo la kusimama Mara kwa Mara abiria wakichimba dawa.Ruti nyingine ni Nachingwea to Morogoro.
Hizi ruti via wapi?
 
Karagan iringa dar alikuwa nazo mbili zilipukutika
 
Hujui raha ya kukaa na pisi kali siti moja utatamani usifike
 
Hii ni biashara nzuri lakini adui mkubwa wa hii biashara ni kama ifuatavyo
1)madereva wa Tanzania ni wa hovyo kama huamini muulize Sumry
2)unazi na ushabiki wa kijinga
3)usipende ligi wala kushindana na mtu
4)Waambie madereva wako wafate sheria waende na muda
5)Dar-iringa Dar-morogoro Dar-Singida Dom - mikoa ya kusaini Dar-Mbeya tafuta ruti ambazo ni lazima watu wataenda huko.
6)Unazi acha unazi na ushabiki na mambo ya wapiga debe tafuta wasimamizi na dereva mzuri
7) Jitahidi uwe na mafundi wako na gereji yako ya uhakika hakikisha gari inapata sevisi mara kwa mara itaifanya idumu kama unabisha muulize Abood na Kilimanjaro express zile gari zao za zamani tena namba ni A zinapatje nguvu ya kuopiga ruti ndefu kama dar-mwanza
8)Tafuta gari ambayo spea zake zinapatikana kwa urahisi

MAGARI
~scania hizi ni gari imara sana kama huamini muulize city boy ya dar- Karagwe na spea zake zipo na uhakika
~ TATA hapa nazungumzia TATA ultra star bus kama bara bara ni ya vumbi hizi chombo ni hatari na nusu (TATA zote kwa ujumla ni roho ya paka)
~Kuna zile zinachongwa hapa hapa Tanzania na zenyewe ni hatari kama unabisha muulize MAJINJAH na Simba mtoto
~HIGER
~leyland,MAN na IVECO [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kama unataka gari za kazi kazi ndio izo roho ya paka izo kazi kazi miaka kama yote kikubwa matunzo

Kama unataka gari luxury sana chukua za wachina
~Asian Star
~Golden dragon
~zhongtong
~Yutong

NB:mimi sio mnazi wa Sauli [emoji2509] wala golden deer [emoji3069] nimetoa ushauri tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Maendeleo hayana chama
 
Hyo namba 4 naikataa,,fatilia imekuwaje BM akateka soko la kaskazini alaf uje hapa uongee

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Moshi Mpwapwa? Hiyo route akipata abiria wengi ni watatu.
 
Kila anaeshindwa biashara ya bus, lawama wanatupiwa madereva wa kitanzania..

Sasa sijui kampuni zenye mafanikio bus zao zinaendeshwa na waturuki?

Darlux madereva walipelekwa mpaka China kwa ajili ya training, lakini bado bus zao zililaza watu njiani! Unajua ni kwanini?

Jifunzeni namna sahihi ya kuendesha hii biashara!! Inashangaza kukuta mmiliki au msimamizi halafu hajui hata vitu ambavyo ni basic sana..

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…