Nataka kununua mchele wa mwaka huu halafu niuuze baadaye

Aisee ...wewe itakuwa umezoea biashara ya kubet,bangi au Unga....yaani Hapo huoni ni faida!????
Ukitaka kupiga hesabu rahisi, chukua hyo 1000 kanunue box la viberiti uza kila siku box moja kwa muda sawa na ambao sawa na kuweka stock mchele.......

Uone hyo elfu moja itakuwa imekuingizia sh ngapi ndani ya huo muda then ulinganishe na biashara ya kuweka stock uone km INA tija!

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Kuna biashara zingine mtu kwa siku 7 anauhakika wa kupata laki 8 faida...every week...sasa kwa mwez huyu ana 2.4m...sasa ww umeweka mchele wako kwa miez hiyo yote uje uambulie 700@kg! Sijajua kwanini watu hatutaki badililka..wewe nunua mchele uza ..nunua uza hata ukipata faida ya 200@/sio mbaya!umedadavua vyema kbs
 
Umeona eeh ...wabongo wengi hatujui umuhimu wa cashflow inayozunguka kwa kasi! .....tunapiga mahesabu ila tunasahau kitu muhimu zaidi kuliko hta hela which is TIME!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point, hizo Mia mbili mbili atazikusanya nyingi Sana ndani ya miezi sita kuliko asubirie 700 kwa miezi sita. Wahindi wametajirika na biashara za faida 200-300 zenye mzunguko
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi natafuta soko la mchele nianze kununua,nikipata connection naanza mzigo
Soko kubwa liko dar ,,kupeleka nje kwasasa imekuwa tabu,sababu ya Hawa wanaofunga funga mipaka
 
Mchele baada ya miezi mitatu, kuna wadudu weupe wa mchele wataanza kuingia!!! Kama una tunza ni bora utunze mpunga.
 
Hivi unanunua mchele let say kwa 1000@kg! May...then dec uje uuze kwa 1800-2000@kg! Means nahangaikia 1000@kwa miezi yote hiyo!!!!!!!!
Unafikiria kunua kilo moja tu? Mwenzako labda anafikiria kununua magunia 500. Manake ni kilo 100*500=50000. Hapo kwa shs 1000 ya faida, jumla kwa hizo kilo ni shs milioni 50 kwa mwaka. Umempata sasa? MILIONI 50 faida kwa mwaka. Kazi kwako kutafakari
 
Unafikiria kunua kilo moja tu? Mwenzako labda anafikiria kununua magunia 500. Manake ni kilo 100*500=50000. Hapo kwa shs 1000 ya faida, jumla kwa hizo kilo ni shs milioni 50 kwa mwaka. Umempata sasa? MILIONI 50 faida kwa mwaka. Kazi kwako kutafakari
Kuna jamaa yangu kaweka milioni 500 ya kukusanya mpunga tu,,yaani mwaka huu watu wenye pesa ndefu nao wameingia kukusanya mpunga
 
Nina uzoef sana na hiyo biashara,mwaka jana nlinunua gunia 200 mwezi wa sita kwa sh 60000@ gunia nikauza mwezi wa pili mwaka huu kwa 90000 kwa gunia,kwakweli faida yake ni ndogo ukitoa cost zote japo huwezi kupata hasara!
Mkuu hilo gunia ulilonunua kwa 60000/kuuza90000 ni gunia la debe sita?
 
Watu wanakimbilia kuona soko la mchele Dar lakini kuna maeneo mengi ambayo hawalimi mpunga kama una mtaji mzuri unafungua store ya kuuza jumla na rejareja. Hii inamaana kuwa badala ya kuweka stock tu.

Pesa inakuwa inazunguka pale unapouza na ku replace mzigo unaouza. Kama kuna mtu serious na hii idea aje Pm nimpe location tuyajenge.
 
Nina uzoef sana na hiyo biashara,mwaka jana nlinunua gunia 200 mwezi wa sita kwa sh 60000@ gunia nikauza mwezi wa pili mwaka huu kwa 90000 kwa gunia,kwakweli faida yake ni ndogo ukitoa cost zote japo huwezi kupata hasara!
200×30000=6,000,000 kwa miezi 12 ni sawa na kujilipa 500,000 kila mwezi.Sio mbaya inalipa kama sio mtu wa tamaa za vikubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…