Nataka kuondoka Tanzania na kwenda kuishi nje ya nchi

Nataka kuondoka Tanzania na kwenda kuishi nje ya nchi

Ingia dating sites mfano Tinder,nk utapata mwenza wa nchi utakayo wabongo wengi wameondoka kwa njia hii, tumia maajent certified wakutafutie kazi nchi utakazo kama we ni mtundu wa net ingia LinkedIn, indeed,live and study abroad,job in Canada nk utapata kazi zipo kampuni wanakufanyia viza na ticket ukiwa hapa hapa nchini ukifika kule wanakata cost zao kwenye salary,angalizo wapo scammer wengi ukitaka usahihi na usalama wa agent au kampuni kama ni halali au sio unawasiliana na police department ya nchi husika au embassy zao.
Maisha mtandaoni siku hizi.
 
Had kufikia maamuzi haya ya kutaka kuondoka inchi yangu kuna mbalimbali ambayo kila siku yananipa mawazo.

mambo yanayonikosea furaha

1. Ugumu wa kupatata ajira yenye mshahara mkubwa.

2. Wazazi wangu wote wamefariki ndugu nao kwangu hawaman msaada kwangu

3. Hata kwenye mapenzi napo bado naumizwa tu yaan mtu anisikilizi wala hanijali

5. Naona akiri yangu inadumaa tu kila siku elimu yangu niliyo nayo nimeshindwa kujiendeleza kwa sababu ya umaskini

Kwa hiyo nilikuwa napenda kupata abc za namna ya kufika huko nje ya inchi,namna ya kupata resident permit, jimbo gani au mkoa gani kwa huko nikifika nitapata kazi kwa urahisi,kodi za nyumba zipoje, gharama ya chakula na mengine nisiyoyajua

Elimu yangu form four passport ninayo na akiba yangu ni 3M

Binafsi nchi nazozipenda ni USA, CANADA, GERMANY, AUSTRALIA na kwa afrika ni MAURITUS

Wakuu karibuni munipe muongozo wa kufika huko
Ngoja Lucas Mwashambwa aje aweke neno hapo. Kama vipi akuingize UVCCM UDC nje nje....
 
Poland, Austria, Malta,Luxembourg ajira tele unaweza anzia nchi nyepesi kuingia hasa za viza free ukijipanga kuingia nchi hizo kubwa pia unakuwa imejengwa traveling history ukienda embassy kubwa kama umewahi safiri sana nje hawakunyimi viza wanaamini huwezi zamia nchini kwao.
Njia nyepesi zaidi ingia ya marriage wazungu wanatafuta sana watu toka Africa kwa sababu hzi.
Wanaume wengi wa kizungu walishahamia upande wa pili,hawana nguvu, wengine wapo bize na kazi hawawazi mapenzi hya ni mambo ya sisi masikini ndo tunawza ngono,wengine hawataki kuoa wanaamua kuwa single forever kule hakuna ya unaoa/ olewa lini au nizae mtoto aje anisaidie walishavuka stage hio ukiwa Mzee pension yako au serikali itakulea hadi ufe,
 
Ingia YouTube mchek black Singapore,EBM Mswahili,jack wa USA,dada Shena wa official dating assistants,mama franjo,huku yuesi,nk wabongo kibao walio nchi mbali mbali uzitakazo watakupa shule,huku jf zaidi ya ngono, zuchu, simba na yanga hizi mambo za maendeleo huku huwezi zipata.
 
Hapana kuhusu viza za huko ulaya na amerika sijui utaratibu wake ila nilifatilia nikaambiwa mauritus hauhitaj visa kwenda huko
 
Back
Top Bottom