Nataka kuondoka Tanzania na kwenda kuishi nje ya nchi

Kuna memba anaitwa shibe kijijini sasa aliwahi kwenda afrika kusini naona kapotea jukwaani sijui jamaa kilimpata kipi.
 
Amesema atarudi kesho.

narudi kesho kila la kheri dogo. Fata unachokiamini.
 
Hata kuhama nchi nacho kipengele tu kama kusaka ajira,,,,husikii huko watu wanafia baharini ila bado wengine wanakomaa
Sijui nianzie wapi kumshauri huyu mtoa mada,yaani naandika nafuta naandika nafuta.
Ila kwa kifupi namuonea huruma na pili naionea huruma milioni 3 yake inavyoenda kutafunwa bure ambayo angeweza kuifanya mtaji akafungua biashara ya kuendesha maisha yake.
Maisha ya nje sio rahisi,maisha ya nje ni kwa ajili ya watu wenye roho ngumu,ni kwa ajili ya watu wanaorisk maisha,sio sehemu ya kwenda tu ukadhani unakwenda kula bata,kuna watu wanakufa kwenye process ya kusafiri kwenda nje mfano mzuri kuna wale Nigerians huwa wanavuka maji Libya,Morocco ili waende Ulaya boti zao huwa zinazama wanakufa wote yaani ambao wanafika ni kwa kubet.
Hapa kuna baadhi ya watu watanikosoa na kusema wale wametumia njia za panya ndio maana wamekufa anyway tuachane na hii kuna Nigerians wengine walienda kwa njia za halali wakafika hadi Canada sasa kwa sababu ya kutopata kazi kwa wakati hawakuweza kumudu gharama za kupanga chumba wakawa wanalala nje kwenye mahema wakafa kwa baridi,maana kule sio kwamba ukifika tu ndio unapata kazi muda huo huo kuna muda mrefu wa kusota kitaa na utakutana na watu wengi kitaani wanalala nje.
Na ukija kwenye upande wa social life kama masimango ya ndugu umeshindwa kuyahimili uka give up basi masimango ya ughaibuni ni mara 4 yake na hakuna mtu anakuchekea au kukudekeza hayo inabidi uyajue kabla hujainua mguu wako kwenda usidanganyike na content creators wanavyoonyesha maisha ya maigizo ukadhani wanaenjoy maisha.
Kila la heri
 
Mjomba milioni tatu hiyo hata tukisema kwa kufikia tu kule unakokwenda(ughaibuni) haitoshi..hiyo wenzio unakula wiki tatu tuuuu interms of Euro+dollar kule uendage una million kumi somehow
 
Wewe una msaada gani kwa hao ndugu zako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…