Siyo wewe wa kwanza!
Kuna mmoja wamerudiana na mtu wake baada ya miaka tisa,
Kilichowatenganisha ni shida za kiuchumi, kubwa zaidi mrudishe mwenzako muishi naye kama amezaa nje mvumilie tu inawezekana hakupenda kufanya hivo{kuzaa nje} na kama ana mtoto asiye wako usiitumie kama fimbo kumchapia..
Usisikilize mawazo ya vitoto vya 2005, lakn jitahidi sana kuwa mpole, futa mawazo mabaya kumhusu, na usimuulze kuhusu mahusiano yake wakat hamkuwa naye.
Broo we ni mwanaume, mrudishe mke wako muishi.
Msamehe yote kwa moyo wako wote, usiyakumbuke ya nyuma, kama mna wazazi wenu wapo hai washirikishe wawabariki {namanisha wazazi wa kuwazaa, siyo ndugu, siyo marafiki na siyo walezi: wazazi ndo viumbe pekee wenye uchungu na nyie, mzazi ndo hawezi kukusimanga, wengne wote watakuchanganya}
RUDIANA NA MKE WAKO NA USIMUITE EX, HAKIKA UTAYAONA MAFANIKIO MAKUBWA..WEWE NI MAN.
NA AKIRUDI ACHANA NA MISHANGAZI ULIYOKUWA NAYO
SALINI NA KUOMBA KWA IMANI YENU.
MUNGU WETU NI MWAMINIFU.