Dar - Mbeya ni km 822.
IST full tank ni litre 45. Fanya yafuatayo pindi utapoanza safari yako;
1) Nakushauri anza safari atleast saa 10 alfajiri ili kuepuka msongamo wa morogoro road na hvyo waweza jikuta umetumia Masaa mawili tu kufika Moro.
2) Safiri siku ya jumapili kwa maana kutakuwa hakuna tochi nyingi wala usumbufu sana.
3) IST highway inaweza kula hadi litre 1 kwa km 18 kutegemeana na uendeshaji wako+ubora wa gari yako.
4) Endesha IST kwenye speed 100 - 120 chini ya Rpm 3, na juu ya Rpm 2. hapo utatumia mafuta kidogo sana
5) kwa km 822 za dar mbeya , hvyo waweza jikuta umetumia litre 45 yaani ukiweka full tank waweza kufika mbeya bila kuongeza, lakini ni ngumu. hvyo wastani wa mafuta waweza kuwa litre 1 kwa km 16 kwa sababu sio seheme zote waweza endesha kwa speed kati ya 100 - 120 ,hvyo jumla ya mafuta dar to mbeya yaweza kuwa litre 52 .
6) Ukifika Makambako ongeza mafuta ili kupata jumla ya litre 52.
7) IST ni gari nyepesi sana ina kg 1000. usiendeshe kwa speed zaidi ya 120 kwa maana waweza pata ajali, asikuongopee MTU na kukwambia eti yangu naendesha hadi speed 140, 160.
8) Heshimu sana alama za barabarani
9) kwa wastani wa hapo juu ukitoka dar SAA 10 alfajiri waweza fika mbeya saa 11 au kama utasimama sana njiani waweza fika saa 12. Usiweke vituo vingi sana njiani, ukitoka dar nenda kapumzikie Mikumi, then kapumzike Makambako then nyoosha mbeya.
10) Epuka kumpa lift mtu usiyemjua ukiwa safarini.
Bonus;
unaenda lini? kuna kamzigo nataka nitume huko unisaidie kukabeba