Nataka kusafiri Dar-Mbeya kwa Toyota IST, nijuzeni haya

vipi swanga
IST ziko fresh sana..nimetoboa nayo mpaka Mpanda mara mbili kupitia Dar-Mby-Tndm-Swanga-Katavi. Ila hakikisha hupakii mizigo mizito na Dar ondoka Alfajir kama mida ya saa 11
vipi swanga-katavi kuna lami tayari
 
vipi swanga

vipi swanga-katavi kuna lami tayari
Last tmi kupita ilikua mwaka jana Dec na lami ilikua nusu bin nusu..nafkiri mpaka sasa watakua wametandiwametandika mkeka kipande kikubwa maana wanaweka nusu nusu.
 
Kaka
kaka upo vizuri saannnaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkuu umetisha, agiza moja baridi, nitalipia[emoji122] [emoji122]
 
Pongezi kwa maelezo yako, nadhani Countrywide ni jina lako sahihi.
 
Shukran kwa ufafanuzi na ushauri wako, nataraji kwenda mwisho wa Mwezi huu
 
JAMAA KAONGEA VIZURI SANA.HAKUNA HAJA YA KUONGEZA KITU WEWE MBEBE HAKO KAMZIGO KAKE TU!
Kasoro kwenye ushauri wa tochi amemshauri asafiri jpili kwa kuwa tochi ni chache amesahau kumwambia "TII SHERIA BILA SHURTI KWA KUTEMBEA BARABARANI KWA KUFUATA ALAMA ZA BARABARANI IKIWEMO VIBAO VYA 50"
 
IST ziko fresh sana..nimetoboa nayo mpaka Mpanda mara mbili kupitia Dar-Mby-Tndm-Swanga-Katavi. Ila hakikisha hupakii mizigo mizito na Dar ondoka Alfajir kama mida ya saa 11
Ulitumia muda gani hadi mpanda
 
Upo kamili mkuu ila umesahau kumweleza kuwa kipande cha barabara toka Mafinga kwenda mbele kukaribia Mbeya kipo kwenye matengenezo so be careful
 
Upo kamili mkuu ila umesahau kumweleza kuwa kipande cha barabara toka Mafinga kwenda mbele kukaribia Mbeya kipo kwenye matengenezo so be careful
Shukran kwa ziada ya angalizo
 
Mkuu,
Nimesafiri na IST Desemba mwaka jana toka Dar kwenda Mbeya. IST yangu ni cc1,500 na nilitumia lita 50. Utaratibu wangu huwa ni kijaza mafuta kila mkoa, so niliweka full tank Dar na nilipofika Moro nikajaza tena, nikaenda jaza tena Iringa lengo ilikuwa kujua kiwango cha mafuta ninachotumia toka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Dar niliondoka saa 11 na nilifika Mbeya saa 2 usiku (sema niliuweka sana Moro). Ukiheshimu alama za barabarani hutopigwa tochi na wala kusumbuliwa na askari njiani. Kwenye 50 nenda spidi 50 na unaporuhusiwa nenda hadi 120. Ukimaliza Kitonga kabla hujafika Ilula kuna kibao kinaruhusu zaidi ya 50 na ni eneo la makazi ya watu, askari hupenda kukaa hapo na huwa wanawakamata madereva kama wamezidi 50. Kuepusha shari, baada ya Kitonga piga 50 hadi Ilula then endelea na maspidi yako. Generally, askari wa Iringa ni wasumbufu kidogo ukilinganisha na mikoa mingine katika njia hiyo.
Nakutakia safari njema...usisahau kuja na 'kambani'...
 
Ulitumia muda gani hadi mpanda
Kwa vile nilikua na mwanangu wa mwaka mmoja na nusu nilitumia Siku 3 sikutaka kumchosha..Dar niliondoka saa 7 mchana nikaenda kulala Mafinga saa 5 usiku. IST yangu ni CC 1,500 na ina pumzi ya kutoboa kwa Siku 2 mpaka Mpanda.
 
Countywide kamaliza....ila kuanzia Ipogolo iringa hadi mbeya kuwa makini na vibao... Hilo eneo linaongoza kwa tochi Tanzania.
 
Mimi hupendelea kusafiri usiku maana hakuna usumbufu wa Tochi wala mkono. You may try it at your own risk, lakini kama gari unaiamini ondoka Dar kumi kama jamaa alivokushauri utafika mapema.

Kitu kingine ukikaa kwenye gari muda mrefu kuna mizuka flani huwa inakuja na kuanza kuhisi speed mfano ya 100 au 120 ni kama haitoshi hivyo kutaka kuongeza. Kemea hilo pepo lasivyo watakuimbia niagieni.

Hata hivyo kama njia haujawahi kuipita kabisa ukiwa unaendesha, jitahidi kwenda kwa tahadhari sana, kunakuwaga na mashimo ya papo kwa papo
 
IST dar moro utatumia litre 12.31 mpaka unafika msamvu IST mtandaoni imeandikwa full tank ni 45 litres ila ukijaza full tank ikifika litre 38-39 gari inakua imeshajaa...ushauri kwa safari ndefu usiruhusu mstari wa nusu tank kushuka chini ya nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…