Nataka kusafiri Dar-Mbeya kwa Toyota IST, nijuzeni haya

Hongera kwa kujitolea kutoa ushauri lakini sijui kwanini nilipata kafeeling utamalizia kuomba lifti.
service charge abebe hako kamzigo chenye mihadharati
 
Sijaelewa point namba 4 yako ufafanuzi maana sijuwagi maana yake
 
Heshima kwa mwanajf Countrywide jukwaa hili umetenda haki nafikiri ndio muongozo unaotakiwa kufuatwa hakuna utani wala masihala
 
Safi sana mkuu nimefurahi pia hako ka bonus
 
Mi nimeendesha Passo litre 40 from tukuyu to dar so kwa ist itakuwa simple
 
Aahahahahah hii design yako ya kuomba msaada nimeielewa. Unastahili tuzo ya mwanafasihi bora wa JF.
 
Huu ndo ushauri wa great thinker... Nimeupenda sana. Nimefurahi pia ulivyochomekea ombi lako hapo kwenye bonus!!!!!
 
[emoji23] Bonus
 
Niletee mfanya kazi wa ndani toka mbeya nasikia wana nidhamu sana
 
Kweli IST ni mkombozi wa watanzania. Yani elfu 60 tu full tank? Wakati kuna raia bila laki mbili mshale haugoti kwa F!
 
Mbeya <> Dar ina trafiki wengi kama kunguru kwenye dampo la mizoga...

Kuwaepuka hao raia ni kupiga kibati usiku unakutana na wale askari wa doria, Mikumi, Mikese, Makambako basi...
 
Umenikumbusha last month nilikuwa na ruti iliyoanzia mbeya-dar kwa ist,baada ya siku 2 nikanyooka to nachingwea baada ya 1 day nikarudi dar then mbeya....IST inajiweza iwe tuu njema cha msingi katika hiyo safari yako uwe tuu na PESA baaaasi bila kusahau mziki mnenee hapo itakuwa poa sana na MAOMBI kabla na baada ya safari.
 
Mkuu kwa majibu yako ubarikiwe. Mimi naomba msaada kutoka dar to bukoba kwa toyota brevis
 
JAMANI MSAADA HAPO KWENYE RPM 3, RPM 2.....tusaidiane wakuu!
 
JAMANI MSAADA HAPO KWENYE RPM 3, RPM 2.....tusaidiane wakuu!
Unataka usaidiwe nini?

Kwenye engine ya gari kuna chuma kijulikanacho kama crank shaft. Chuma hiki hushikilia piston zilizoko kwenye engine na kinatumika kubadilisha upward/downward movement za piston kuwa radial/rotational/ angular motion.
Kwa hiyo RPM ni revolution per minute au idadi ya mizunguko ambayo hiyo crank shaft inaweza ikakamilisha ndani ya sekunde sitini.
Kwa hiyo wakisema 2000 rev/min inamaana chuma hicho cha crank shaft kitazunguka mara elfu mbili ndani ya sekunde 60 au ndani ya dakika moja.
Kwa kadiri chuma hiki kinavyozunguka ndivyo ambavyo kunakuwa na uwezekano wa gari yako kukimbia mwendo mkali ikitegemewa na gia uliyopo.
Sasa wanapokwambia kuwa rev zisizidi 3000 wanamaana kuwa kwa kadri gari inavyounguza mafuta mengi sana kwa mda mfupi ili kuweza kufikisha hizo rev 3000, ufanisi wa uunguzaji wa mafuta ukilinganishwa na idadi ya mizunguko itakayozalishwa huwa unapungua na hivyo unaweza ukajikuta umetumia mafuta mengi kwa umbali kiduchu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…