Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu pole kwa maswahibu, nina rafiki wakike mtu wa bara, ambaye ana gari ya kawaida tu, amepanga mbweni na ana kikampuni cha mfukoni tu japo ana vibali vyote hence analipa kodi, kazi yake anapokea watalii na kuwapangia safari, na hii kazi amejifunza mwenyewe bila msaada wa yeyote, mwaka wa 4 huu yuko kwenye game. Changamoto gari yake ni ya kawaida/ haiko licensed kubeba abiria/wageni, lakini anakomaa nayo tu, hata akikamatwa na matrafiki “yanazungumzika”.
Wewe ambaye umetoka kwenye reputable organization, una experience nzuri, una support system (your former Boss) una gari nzuri, naona uko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri, unless una tatizo lingine au umepamiss kwenu.
Wazanzibar hawa ni wakuishi nao hivyo hivyo tu, samaleko nyingi ilimradi yako yanaenda.
Usikate tamaa, binafsi naona ukiamua kukomaa utafanikiwa, tena una pakuishi kabisa. Labda kuna mengine haujayasema.
Jibu zuri ...Wako watanganyika wengi sana wanamiliki ardhi na biashara kubwa hapa Unguja. Asante pia kwa ushauri
Siitikii hiyo ni mtego! 😀Samaleko mrembo kiziwi. 😎
-Kaveli-
Mganga wa nini😳Kila sehem ni mapambano. Dunia uwanja wa vita! Uzuri wa Zanzibar uchumi wake ni hybrid yani sio wa kitanzania Moja kwa Moja. Huyu akirudi dsm anaenda kupambana na uchumi wa mtanzania halisi... Kabla ya yote kwanza atafute mganga
Waafrika wenyewe, wabara ukiwawekea biashara watakupoteza dakika sifuri tu. Zanzibar biashara nyingi target ni wazungu... Hasa zile zilizo katika center ya jiji (mji mkongwe mpaka malindi) na maeneo mengi yaliyokamatana na fukwe.. Ofkooz zimesimama vizur na hazipigwi mafataki/manyukiliaMganga wa nini😳
Wewe upo unguja?Waafrika wenyewe, wabara ukiwawekea biashara watakupoteza dakika sifuri tu. Zanzibar biashara nyingi target ni wazungu... Hasa zile zilizo katika center ya jiji (mji mkongwe mpaka malindi) na maeneo mengi yaliyokamatana na fukwe.. Ofkooz zimesimama vizur na hazipigwi mafataki/manyukilia
Yah Niko katika vitongoji vya stone townWewe upo unguja?
Sawa mkuuYah Niko katika vitongoji vya stone town
Siitikii hiyo ni mtego! 😀
Mi sijambo sijui wewe, been ages!!!!
Vizuri kusikia uko salama Kaveli.Kwamba umesanuka chap hako kamtego 😄. Wacha nifanye reshuffle of my strategies. Next time around lazima unase. 😎
Yes rafiki, kwakweli it has been a while without retouching our base. Unaadimika sana hapa na kuleeee 🤫.
Mie pia am doing fine and healthy. Many thanks to the almighty.
-Kaveli-
Zanzibar ukiondoa utalii hakuna biashara ya halali utafanya MTU wa bara ikutoe sababu ya ubaguzi. Ukiweka duka hawanunui kwako wenyewe wanaita CHOGO au WANYAMWEZI. Bakhresa mzanzibari lakini kakimbia kwao yupo Oysterbay
NB.ACHA ujinga mkuu!!
Usirudi Bongo Huku michosho!!
Kaza huko huko!!
Hiyo alphard.iendeshe mwenyewe sio kuwapa madereva!
Baki huko huko!
Pole sanaNdugu wana JF poleni na kazi na mihangaiko ya maisha.
Mimi ni kijana wa miaka 29 mzaliwa wa Morogoro na kukulia DSM hasa maeneo ya Tandika! Nilipohitimu masomo yangu pale UDSM 2017 nilikuja Unguja mwezi wa 7 mwaka huo huo kujaribu bahati yangu, kilichonileta ni soka na alieniunganisha na hio timu ni rafiki yangu. Lkn ligi ya Unguja hailipi kwa mwaka huo ilikuwa ni kujitolea tu.
Mwishowe nikaongea na mwenye timu kuwa maisha ya soka yamenishinda narudi nyumbani, yule tajiri aliuliza kinachonisibu na mimi nikamueleza, Lkn alishangaa sana kusikia mimi ni muhitimu wa chuo kikuu na nimekosa kazi mpaka nimeamua kuja kucheza mpira ili nipate kula.
Yule tajiri alitokea kunielewa sana, akanambia nisiondoke na pale kwenye nyumba ya timu mtaani atanihamisha nitakaa peke yangu na atanitafutia kazi na kweli alitimiza, Mwaka uliofata yaani 2018 mwezi wa 8 niliajiriwa kwenye taasisi moja inayojishughulisha na masuala hapa Unguja.
Ile taasisi ilinibadilishia maisha yangu sana kwani ndani ya muda mchache nilikuwa miongoni mwa wafanyakazi tegemezi pale kwenye taasisi, elimu yangu ikanisaidia kupata nafasi nzuri na mshahara mzuri zaidi kwani wengi wa waajiriwa walikuwa hawana elimu kubwa na wengi ni mabeach boy tu wa mtaani.
Maisha yalibadilika sana ndani ya muda mfupi safari za Dar, Arusha, Zenji kwa mwewe ilikuwa kawaida sana kwangu, nilipata pesa nyingi pia nje ya mshahara wangu, Nyingi zikiwa ni tips toka kwa wageni tukiwa safarini.
Mimi napenda sana watoto na wageni wengi wenye watoto walikuwa hawawezi kuniacha hivi hivi maana watoto wao walinipenda kwa muda mfupi na mara nilipojua hili shimo nililishikilia kweli kweli japo corona ilifanya taasisi ikayumba kidogo na baadhi ya wafanyakazi kupunguzwa lkn nashukuru sikuwa miongoni mwao.
Wakati wa corona mabosi walishindwana (Nasema mabosi kwa kuwa taasisi ni share older ya watu watano), Baadhi walitaka kampuni ifungwe kupisha janga la corona na wengine walisisitiza kazi ziendelee hata kama ni kwa hasara Ila jina la kampuni liwe midomoni mwa watu, Mvutano huu ulipelekea muanzilishi mmoja wa kampuni kujitoa na kudai share zake na akapatiwa na kuletwa share holder mwingine (Huyu aliyejitoa ndio aliyenipa kazi baada ya kuuganishwa na yule jamaa mwenye timu)
Kutokana na changamoto ya corona, mshahara ulipunguzwa sana na tukawa tunalipwa kama posho tu. Hali hii ilifanya niingie bank kucheki balance yangu na nikakuta nina namba nzuri tu kwenye account zote mbili (Ya Tsh na Dolar) nikaamua kununua viwanja vitatu hapa Unguja, nikanunua Alphard pia nikampa mtu aifanye private hire na nikawa nampa wageni wa pale kazini wanaotaka usafiri kwa siri kubwa maana hairuhusiwi taasisi ina magari yake pia inakodisha. Nilibakiwa na pesa kidogo sana kwenye acc kw ajili ya kula na matumizi madogo madogo maana ardhi ni ghali sana Unguja hasa maeneno jirani kama Kisauni, Mbweni, Kiembe Samaki, Chukwani, Fuoni, Kwerekwe nk!
Penye rizki hapakosi fitna wahenga walisema, kuondoka kwa yule bosi mmoja ikiwa kama kinga niliyokuwa nayo pale kwenye taasisi imeondoshwa na hapo nikaanza rasmi kuoneshwa mm sistahili kuwa pale, kwanza nikondolewa nafasi niliyopewa kwa kigezo kuwa mimi sijasomea masuala ya utalii japo hakuna yeyote aliyesomea wengi wamesomea lugha tu Kifaransa, Kipoland, Kirusi, Kitalina nk, kuondoshwa kwa hiki cheo kukafanya nibaki nategemea mshahara tu though haukuwa mdogo mana ni tarakimu 7 lkn nilipoteza pesa nyingi nilizokuwa napata kwenye kuandaa safari za ndege, hotel, chakula, sehemu wanazotembelea wageni nk
Wageni wengi walinizoea na walikuwa wanatoa recommendation nzuri dhidi yangu hiyo hata ofisini nikawa sikosi mia mia nje ya mshahara, lkn kadri muda ulivyokuwa unaenda nilianza kuona visa na mikasa, ubaguzi wa wazi wazi dhidi yangu! Mtu anakuchokoza kwa kukuita kafiri kisa tu muda wa kuswali umefika na wewe hujaenda kuswali ama hujasitisha huduma, wengine wanakuita ukawa timu pinzani, wengne wanasema aliyekuleta kaondoka wewe unafanya nini ilimradi tu ujibu ukatwe mshahara ama usimamishwe kazi nk
Haya tote yalianza kunikinaisha na ile kazi maana sasa nilikuwa simalizi miezi 6 bila adhabu kusimamishwa bila malipo ama kukatwa mahahara hata “Akijamba Mwantumu naambiwa nanuka mm” hii hali ilinikera sana. Lkn mtoto wa maskini hadeki niliendelea kuhustle kama kawaida nikijituma huku na kule na mwaka jana mwanzoni nilifanikiwa kujenga nyumba kwenye moja ya viwanja vyangu, Nyumba ya vyumba vinne viwili vikiwa ni master, jiko sebule na dining na stoo nikaipiga fence tamu sana nikaiacha ikiwa inahitaji finishing ndogo sana za ndani lkn rangi madirsha milango tiles mafeni gypsum tyr kifupi ni complete house
“Barabara hata iwe ndefu vipi haikosi kona kona, mwaka Jana mwez wa 6 yule dereva wangu nilimpa wageni 7 wanataka kuzunguka shamba (Shamba ni eneo nje ya mji hapa Unguja, Huko kuna mahotel na starehe nyingine nyingi) wale wageni wakaomba waongozane na mmoja wa mwenzetu pale ofisini, Hapo ndo kitumbua kiliingia mchanga kwani wakiwa njiani yule mwenzangu aliisifia gari kuwa inatunzwa vizuri iko fresh sana na yule dereva wangu ndipo akaropoka kuwa gari ya boss wako X hii.
Jamaa akachimbwa na yule mwanamke akamfungukia kuhusu nyumba na mengne mengi anayoyajua kuhusu mimi. Kesho yake nikaitwa na boss kuulizwa kwanini wageni hawakodi magari ya ofisi na badala yake gari fulani linaonekana kubeba sana wageni wa kampuni hasa wale wanaopita kwenye mikono yangu!
Nilijitetea sana kwamba yule jamaa bei zake ni nusu ya zetu na wageni wengi ni vishuka (hawana pesa) ndo maana nampa yeye kuiepusha taasisi na hasara lkn maelezo yangu hayakufaa kitu! Boss alikuwa anajua kila kitu na mwsho akanipa barua ya kunisimaisha kunifukuza kazi. Nilimsihi sana anisamehe lkn haikufua dafu sana alisistiza nilipokula na kuihujumu taasisi pametosha.
Wakati huu sikuwa na akiba yoyote bank maana ndo nilitoka kumalizia ujenzi nikabaki nasubiri pesa za kwenye gari niwe nakula lkn jamaa nae akwa analalamika kukosa wageni hivyo pesa ikazidi kuwa ngumu na tayari nilikuwa nawasaidia ndugu zangu wengi hivyo nikaanza kuona pengo sasa.
Nikauza kiwanja kimoja mwak jana mwezi 10 ili nijitafute lkn imeshindikana ile pesa nimeishia kuila tu na kusaidia ndugu! Sasa nimebakiwa na kiwanja kimoja ambacho nilikinunua 18M thamani kwa sasa inaweza kufika 25M mpk 22M, 20M ikawa bei ya chap kwa haraka, nina Alphard japo biashara haiendi nimechoka kugombana na madereva, na nina nyumba ambayo thamani yake inaweza kufika 100M kwa hapa Unguja.
Wazo langu ni kuuza hv vyote walau nipate 150M to 140M Kisha nikanunue nyumba 3 Tandika za 15M each, 2 nizipangishe na moja niifanyie ukarabati niweke flem zangu Tatu nifungue duka la chakula na mahitaji yote ya nyumbani na nje niweke genge, flemu ya pili nifungue glosary ya kawaida ya mtaani na nje niweke chips na flem ya Tatu nifungue mama lishe!
Hili ni wazo langu naomba ushauri zaidi hata ulio nje ya huu wana JF.
NAWASILISHA.